Tujadiliane na kushauriana namna ya kupunguza tatizo la ajira nchini!

chakii

JF-Expert Member
Sep 15, 2013
19,673
22,615
Habari wanaJamvi.


Tatizo la ajira limekuwa likishika kasi kila kukicha huku jitihada za Serikali zikionekana waziwazi kugonga mwamba.Wasomi wanaongezeka kila siku huku hakuna mfumo ambao utawasaidia kupata ajira ya Uhakika, inafikia kufanya kazi ambayo huna ujuzi nayo ilimradi mkono uende kinywani maana umri nao unakwenda.


Miaka michache ijayo nchi yetu tutakuwa na idadi kubwa ya watu wasiokuwa na ajira na hii itarudisha sana maendeleo ya nchi nyuma sana maana nguvu kazi kubwa itakuwa vijiweni na katika shughuli za kiuhalifu.
Naomba kupitia huu uzi tujadiliane namna ya kutatua tatizo hili ambalo hata viongozi wetu wa kisiasa wamediriki kuliita BOMU linalosubiria kulipuka.Naamini wapo wengi watakaofaidika na michango itakayotolewa hapa na hatimaye tutakuwa tumeisaidia jamii yetu.
Karibuni.
 

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
549
182
mmh! hii ngumu, haina hata wachangiaji?

Pengine ndio maana hata hili tatizo linakuwa kubwa kwa sababu hatujui hata tufanye nini kupambana nalo. kwa mustakabali huu litaendelea kuwa kubwa...
 

Kitumbo

JF-Expert Member
Jun 16, 2010
549
182
Jana nilikuwa naongea kwa sim na mpwa wangu. Alinieleza kuwa amemaliza kidato cha sita na yupo njiani kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria. Niliwaza mengi sana. Niliwaza, "hivi ni kweli kwa kuwapeleka vijana JKT kwa wakati huu Serikali inatumia rasilimali zilizopo –ikiwa ni pamoja na nguvukazi ya vijana kwa usahihi? Je, hakuna njia nyingine mwafaka ya kutumia rasilimali hizi kupambana na tatizo la ajira ambalo linaendelea kuwa kubwa?

Nilikumbuka nikiwa form six mwaka 1990 niliwahi kuongea na "room mates" wangu kuwa "JKT ni mzigo kwa taifa na nawaambia Serikali tuliyonayo sasa ina watu wanafikra za kujenga uchumi, hawatakubali kuendelea kulibebesha taufa mzigo huu. Naamini JKT haitadumu kwa miaka mitano ijayo." Na kweli, mwaka 1993 ilisitishwa! Sasa JKT imerudi tena. Je, kuna uboreshaji wowote umefanyika ili kutatua kero za maendeleo za nchi hii?

Kuna swala la kuwajenga vijana kulijua taifa lao (nationalism). Hii kwakweli inabaki katika maelezo lakini si kwa vitendo. Kuna haja ya kulifanya hili kwa vitendo.
Sasa kama ni muhim sana kuwa na JKT leo hii, kwa maoni yangu, ningeshauri yafuatayo:-

· Badara ya kuchukua vijana wanaomaliza form six, tuwapeleke vijana wanaomaliza vyuo mbali mbali ambao tayali wana ujuzi maalum

· badala ya kuyafanya makambi haya kuwa ni ya kutumia fedha tu yafanywe kuwa vituo vya uzalishaji.#
· Tutumie watu wetu wenye ujuzi kuandaa michanganuo ya miradi. Kila kambi lichague production line inayoendana na resources zilizopo katika maeneo husika. Mfano: Mlale-agricultural production, Ruvu-Animal/poultry production, sehem zingine- small scale industries etc
· Serikali itoe rasilimali za kufanya mass production. Vijana watoe nguvu kazi ambayo pia itawasaidia kupata practical training ya yale waliyojifunza vyuoni.
· Production ilenge masoko ya ndani na nje na kila kambi lipewe jukumu la kuzalisha kiasi ambacho litajiendesha lenyewe

Ninawaza tu!
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom