Tujadiliane kama tija ipo hapa kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadiliane kama tija ipo hapa kwenye uteuzi wa wakuu wa wilaya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mageuzi1992, May 10, 2012.

 1. m

  mageuzi1992 JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2012
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 2,512
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Habari kubwa leo katika magazeti mbalimbali ni juu ya uteuzi wa wakuu wa wilaya. Baada ya kuanzishwa wilaya mpya, idadi yote ya wakuu wa wilaya sasa imetimia 133. Je, nafasi hii inaumuhimu ghani katika maendeleo ya Taifa letu. Ni kiasi gani cha gharama ambazo walipa kodi tunabebeshwa ili kuhudumia ofisi hizi na je, kunadhamani inayopatikana? Hapa tayari kuna V8 au VX 133 kama kila moja ni 180,000,000.00 jumla ni shs. 23,940,000,000.00 yaani bilioni 23 na milioni 940. Mfano kuna wilaya mpya inaitwa NyangwÂ’ale natumai ipo huko usukumani kama dawati ni shs. 80,000/= gari la mkuu wa wilaya linatosha kununua madawati yapatayo 2,250. Tujadiliane, ukiachilia gari la Mkuu wa wilaya ni gharama zipi zingine zinatokana na uwepo wa ofisi ya mkuu wa wilaya?
   
Loading...