TUJADILIANE: Je Elimu ina umuhimu gani kwenye mahusiano?

ladyfurahia

JF-Expert Member
May 10, 2011
14,699
9,461
Habari wadau wangu wa ukweeeeeeeeeeeeeeeeeeee

Leo nimeleta kwenu MADA ambayo inahusu kujadiliana hivyo unachangia kile ukionacho wewe na sio kuponda wengine kuhusu Swali hili: JE ELIMU INA UMUHIMU GANI KWENYE MAHUSIANO YA NDOA, WENZI, MARAFIKI NA WACHUMBA?

Elimu inaweza kuleta maendeleo ya penzi lenu au inaweza kufarakanisha? Je ukiwa na mtu asiye na elimu hasa ya darasani ataweza kukabiliana na changamoto za maisha ya mahusiano yenu kimantiki au kimakinikia? au atakuwa ana perekeshwa tu na yule mwenye elimu ya kidarasa?

Je kwa yule mwenye elimu atawezaje kumsaidia mwenzi wake asiye na elimu au itakuwa ni parakanyiko baina yao? Je elimu itawafanya waendane Kimawazo/ au kimaendeleo?

Haya wadau mabestito karibuni kutoa maoni yenu hapa .

Wasalaam
Ladyf
 
Elimu kuchangia kufarakanisha mahusiano? sidhani mtu anatakiwa awe anamuelewa mwenzake tu anapokosea, mambo kumwendea kombo au anapofanya kitu ambacho hapendi,
Hii haihusiani na kiwango cha elimu cha mtu, naona ni haiba na malezi ... kuna watu wana elimu kubwa tu ila ni watu wa gubu, lawama, wako very demanding, uncompromising, blunt, irresponsible etccc....
Japokuwa kuna correlation fulani kati ya watu 'vilaza' na mambo kama hayo,
 
Elimu haina nafasi kubwa katika mapenzi mtu anayekwambia mm nataka mtu mwenye degree ndio awr mwenza wangu ujue huyo anaangalia mambo ya kiuchumi kwnz....wapo watu hawana elimu lkn wanadumu kwny mapenzi sn


Mtu akikupenda,akakuheshimu na kukujali inatosha sn kwa mtazamo wangu mimi
 
Mwenye elimu nzuri anategemewa kuwa na mipango bora ya maisha na hivyo kuwa na familia bora kiuchumi.
Mfano
Msomi anategemewa kupata kazi yenye maslahi mazuri
Au
Msomi anategemewa kutumia elimu yake kuanzisha kampuni au mradi utakao mwingizia mapato mazuri na pia kuweza kuajiri watu weredi na hivyo kuboresha maisha ya jamii yake, na maisha ya familia kwa ujumla.
Mwanamke msomi hawezi kuolewa na kijana asiyesoma labda huyo kijana
awe tajiri.
Sijawahi kuona mwanamke aliyemaliza chuo kikuu akaenda kwao kijijini na akaolewa na mkulima wa jembe la mkono ambaye ana elimu ya darasa la saba.
Mwanamke anapenda kuolewa na kijana anayemzidi au elimu ama utajiri.
Ndivyo hali ilivyo.
 
Elimu haina nafasi kubwa katika mapenzi mtu anayekwambia mm nataka mtu mwenye degree ndio awr mwenza wangu ujue huyo anaangalia mambo ya kiuchumi kwnz....wapo watu hawana elimu lkn wanadumu kwny mapenzi sn


Mtu akikupenda,akakuheshimu na kukujali inatosha sn kwa mtazamo wangu mimi
Wise words

What goes around always comes around
 
Kwenye mahusiano ya Ndoa, Mchumba na Rafiki Elimu haina nafasi, sana sana kinachotakiwa ni maelewano ya wahusika.
 
Haiwezekani eti mimi msichana nina degreee yangu na pengine zaidi ya hapo eti nije kuolewa na mtu ambae hana hata degree.......mi siwezi kwa kweli labda kwa wengine na Mungu anisaidie nije kupata mume mwenye elimu yake
 
Jamani, tutasema mengi sana hapa lakini ukweli tabaki kuwa "hakuna kitu kizuri kama mkikutana wote mnaelimu ya level flani hivi hata maongezi yenu yanakuwa rahisi, mawazo yanakuwa yanaendna na ni rahisi sana kufika muafaka katika mambo tofauti tofauti pasipo mmoja kuonewa au kuwa mnyonge kwa mwenziye".
In short...everything becomes easy!

But....upendo ndiyo kitu cha msingi kuliko vigezo vingine vyovyote vile.
 
Back
Top Bottom