yusuphfrancis
JF-Expert Member
- Oct 26, 2016
- 433
- 361
Mwanzoni baada ya Daudi Albert Bashite kubainika kuwa anatumia vyeti ya mtu mwingine anayeitwa Paul Christiani M, ambapo aliiomba mahakama aape kubadili hiyo M kwenye jina hilo na kuwa Makonda, yaani aitwe Paul Christian Makonda, watu walisema Daudi Albert Bashite achukuliwe hatua kwa kutenda kosa hilo la kuupotosha umma kuwa yeye anaitwa Paul Christian Makonda kwa kuapa kwa jina hili.
Hivi karibuni waziri Angela Kairuki ametangaza majina ya watumishi wa umma wanaosadikika kuwa wameghushi vyeti vya taaruma zao na wanatakiwa waondoke kazini kwa hiari hao wenyewe bila kusubiri kufukuzwa au kuchukuliwa hatua za kisheria, lakini watu wamelalamika kwamba serikari haijafanya vizuri kuwaambia waondoke kazini bila kuwalipa mafao yao na baadhi wameenda mbali kwa kuwashauri wasiondoke ila wafike mahakamani kudai haki zao.
Swali,
a) Kwanini watu wanamtaka Daudi Albert Bashite achukuliwe hatua kwa kutenda kosa la kutumia cheti cha mtu mwingine wakati huo huo wanawatetea watu zaidi ya 9000 kuwa wameonewa ili hali wametenda kosa la namna ile ile kama la Daudi Albert Bashite?
b) Kwa kuwatetea hawa zaidi ya 9000, je, msingi wa utetezi huu umejengeka katika kudai haki kuwa kama Daudi Albert Bashite ameachwa kuchukuliwa hatua basi na hawa zaidi ya 9000 waachwe pia?
KARIBUNI!