Tujadili: Uwepo wa Ujamaa wa kisasa ama Ubepari

Babeli

JF-Expert Member
Jul 20, 2015
6,660
3,233
JF
Nimeona nianzishe uzi tujadili hili maana nimeona minyukano ya pandehizi mbili na matusi juu wakati huu hasa baada ya kuondokewa na Rais wetu mpendwa Magufuli...RIP..
Mi nadhan kwanza wanataka kumyumbisha Rais wetu Mama Samia na utawala wake...sidhani hawaelewi kwamba wananchi majority zaidi ya 85% ndio waliichagua ccm ichukue dola...wale wengine walipigwa kule..inamaana kwamba wananchi wanataka itikadi ya ccm iendeshe nchi.ambayo Ni Ujamaa na Kujitegemea..Ujamaa huu Ni wa kisasa sio ule wa enzi zile..Ujamaa huu unataka njia kuu za uchumi kumilikiwa na umma..keki yoyote ya nchi inaenda equally kwenye huduma kama barabara, hospital, shule..n.k. biashara huria ilimradi iwe halali na ulipe Kodi forodhani..uwepo wa Demokrasia ya kweli...Na wananchi wanahimizwa kujenga chumi zao ili wajitegemee..wasiwe ombaomba...tatizo liko wapi.?.labda tujadili tueleweshane..kwa sababu naamini wananchi wanachoamua wanakielewa sana..Miaka yote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Ubepari ndo mzuri kwa kujenga uchumi kwanza unaruhusu ushindani baina yetu.Kinachotakiwa serikali isiruhusu "pure capitalism" badala yake iwe ni "mixed economy" nadhani uchumi utakuwa sana,ujamaa unalemaza
 
Nilipofika hapo kuwa 85% ya wananchi ndio waliochagua ccm, nikajua maelezo mengine yote yanafuata ni utoto mtupu. Ule haukuwa uchaguzi, bali maonyesho ujinga wa mtu mweusi kwenye box la kura fullstop.
 
How to control mixed economy jomba ...naona Kuna shughuli...kwani ujamaa wa kisasa Ni kitu gani unakwamisha...kama biashara ruhusa..tena huria..ruhusa kufanya biashara yoyote halali..
 
Na wananchi wanahimizwa kujenga chumi zao ili wajitegemee..

Kama mtu mwenye masters anakubali kuwa mlamba nyayo pia mshika pembe ili apate teuzi, vp kwa mwananchi aweze haya???
 
Huo ndio uhalisia kwenye record zetu jomba..hatuna alternative data zozote zilizosema otherwise..hakuna hata kesi ya mahakama ya kupinga..matokeo..basi hiyo ndio data tunayo. Hatuwez argue kwa kutumia akili tu zetu then ikawa aunthetic data au information
 
Na wananchi wanahimizwa kujenga chumi zao ili wajitegemee..

Kama mtu mwenye masters anakubali kuwa mlamba nyayo pia mshika pembe ili apate teuzi, vp kwa mwananchi aweze haya???
Daaa hapa sijaelewa mwongozo tafadhali
 
How to control mixed economy jomba ...naona Kuna shughuli...kwani ujamaa wa kisasa Ni kitu gani unakwamisha...kama biashara ruhusa..tena huria..ruhusa kufanya biashara yoyote halali..
Shida ya sera za kijamaa kwa Tanzania ni tabia ya viongozi kuwa na mamlaka ya kujitwalia mali za watu binafsi walizotafuta kwa jasho na miaka mingi....

Unapomnyang'anya mtafutaji unamvunja moyo wa kutafuta zaidi. Pia kunakuwa hakuna uhakika wa mazingira ya biashara kutanuka na kuwa kubwa sababu sheria hata kama zipo haziheshimiwi maana serikali ndio inakuwa na last say badala ta mahakama na mamlaka husika.

So nadhani tunaweza kuboresha huu ujamaa wetu kama tutaweza kurekebisha baadhi ya sheria ambazo zitaweza kulinda raia na mali zao.
 
Hangaikeni sanaa ila ccm ni ya wale wale....wanarithishana wenyewe, nyie wengine mtaashia kuvaa kofia na tshrt tu
 
Ubepari ndo mzuri kwa kujenga uchumi kwanza unaruhusu ushindani baina yetu.Kinachotakiwa serikali isiruhusu "pure capitalism" badala yake iwe ni "mixed economy" nadhani uchumi utakuwa sana,ujamaa unalemaza
kama unapenda unapenda ubepari usiwe mmoja wa walio lalamika bei ya vifurushi,
 
Mara hatutaki ujamaa, mara serikali punguza bei za vifurushi,." Tanzania kuna watu hawajui wanachokitaka"
 
How to control mixed economy jomba ...naona Kuna shughuli...kwani ujamaa wa kisasa Ni kitu gani unakwamisha...kama biashara ruhusa..tena huria..ruhusa kufanya biashara yoyote halali..
Ujamaa ndio njia pekee itakayomkomboa Mwafrika...

asilimia 90 ya Watanzania hawawezi kuishi upebari...

Marekani kuna vyama viwili vinavyopokezana madaraka Democratic na Republicans.

Democtratic(American Socialist) ni Kama CCM kwa mbali na Rebulicans ni Kama Chadema.

Hivi vilikuwa chama kimoja ila kulikuwa na mambo machache ambayo waasisi wake hawakukubaliana

1. Kodi
2. Huduma za Jamii
3. Namna Serikali itajenga miundombinu
4. Mipaka ya Free Market

Kwenye Kodi Republicans wanaamini kuwa matajiri hawatakini kulipa kodi kubwa na badala yake mzigo wa kodi upewe middle class na lower class, sababu ni kuwa tajiri ana weka equity kubwa kwenye uchumi hivyo ana take risk kubwa kuliko makundi mengine, na pia kama utawapunguzia kodi watajiri watazalisha kwa wingi.

Democratic wao wanaamini Sio sawa tajiri alipe kodi ndogo na middle-class wawe na mzigo wa kodi, jamii itakuwa na matabaka yasiozuilika

Kwenye huduma za jamii Republicans wao wanaamini kuwa Huduma za jamii kama afya na bima hazipaswi kugharamiwa na Serikali badala yake kila mmoja ajigharamie, kwa serikali kugharamia huduma za Afya ni kuifilisi serikali na kumuondolea mtu machaguo katika afya yake

Democratics wanaamini serikali inapaswa kugharamikia huduma za jami ili ziwe nafuu kwa watu wote

Kuhusu soko Huria.
Repulicans wao hawakubaliani na government regulations kwenye free market wanataka biashara ziwe free as they can be, ndio maana wanaamini serikali kuwa katika mikataba kama ya Carbon emission inachangia kufifisha biashara na hata Trump aliwahi kujitoa.

Binadamu ni mjamaa kiasili ila mazingira ndio yanamofanya ajifunze tabia za kipebari, Waafrika tutafanikiwa kama tutaweza kuendeleza ujamaa na kujitegemea.
 
sidhani hawaelewi kwamba wananchi majority zaidi ya 85% ndio waliichagua ccm ichukue dola...wale wengine walipigwa kule..inamaana kwamba wananchi wanataka itikadi ya ccm iendeshe nchi.ambayo Ni Ujamaa na Kujitegemea..Ujamaa huu Ni wa kisasa sio ule wa enzi zile.
Unaleta mada MAKINI ili ijadiliwe kwa umakini wake; halafu hapo hapo mwenyewe unaifanyia mzaha!

Unataka watu wajadili upuuzi?
 
Ujamaa ndio njia pekee itakayomkomboa Mwafrika...

asilimia 90 ya Watanzania hawawezi kuishi upebari...

Marekani kuna vyama viwili vinavyopokezana madaraka Democratic na Republicans.

Democtratic(American Socialist) ni Kama CCM kwa mbali na Rebulicans ni Kama Chadema.

Hivi vilikuwa chama kimoja ila kulikuwa na mambo machache ambayo waasisi wake hawakukubaliana

1. Kodi
2. Huduma za Jamii
3. Namna Serikali itajenga miundombinu
4. Mipaka ya Free Market

Kwenye Kodi Republicans wanaamini kuwa matajiri hawatakini kulipa kodi kubwa na badala yake mzigo wa kodi upewe middle class na lower class, sababu ni kuwa tajiri ana weka equity kubwa kwenye uchumi hivyo ana take risk kubwa kuliko makundi mengine, na pia kama utawapunguzia kodi watajiri watazalisha kwa wingi.

Democratic wao wanaamini Sio sawa tajiri alipe kodi ndogo na middle-class wawe na mzigo wa kodi, jamii itakuwa na matabaka yasiozuilika

Kwenye huduma za jamii Republicans wao wanaamini kuwa Huduma za jamii kama afya na bima hazipaswi kugharamiwa na Serikali badala yake kila mmoja ajigharamie, kwa serikali kugharamia huduma za Afya ni kuifilisi serikali na kumuondolea mtu machaguo katika afya yake

Democratics wanaamini serikali inapaswa kugharamikia huduma za jami ili ziwe nafuu kwa watu wote

Kuhusu soko Huria.
Repulicans wao hawakubaliani na government regulations kwenye free market wanataka biashara ziwe free as they can be, ndio maana wanaamini serikali kuwa katika mikataba kama ya Carbon emission inachangia kufifisha biashara na hata Trump aliwahi kujitoa.

Binadamu ni mjamaa kiasili ila mazingira ndio yanamofanya ajifunze tabia za kipebari, Waafrika tutafanikiwa kama tutaweza kuendeleza ujamaa na kujitegemea.
Mkuu umetoa somo la kutosha hapo kwa mfano huo; hata kama umeurahisisha sana.

Ninakubaliana kabisa na maneno ya mwanzo uliyoweka kwenye mstari wako wa mwisho.

Mwisho: hebu cheki hii ya hao hao wamarekani uliowachambua hapa>

Janga la COVID-19 - Trump anasema "Go Big" yaani wananchi wapewe pesa kiasi kikubwa zaidi ya zile $400 walizopewa kwenye awamu yake. Na Trump, ni CAPITALIST as CAPITALISTS come!

Halafu akaingia Biden, Democrat (pengine liberal); yeye akagawa kwa wananchi wake na watoto $1400.

Na mwanzo watu hao hao walipewa $1,200, ili kusaidia kuendesha maisha yao wakati wa corona.

Marekani ndio mfano wa juu kabisa, inapozungumziwa capitalism!

Lengo langu la kuyaandika haya hapa, ni hii kasumba tunayo okoteza bila hata kujua maana ya mifumo hii ya kiuchumi.

Ukimkuta mTanzania anayejinadi yeye anafurahia zaidi Ubepari, utadhani ni yeye aliyeuvumbua; kumbe maskini wa mtu hajui kitu.
 
Watu mdomoni wanasema wao wajamaa
Wakati kwenye maisha yao wanaishi kibepari

Ova
 
JF
Nimeona nianzishe uzi tujadili hili maana nimeona minyukano ya pandehizi mbili na matusi juu wakati huu hasa baada ya kuondokewa na Rais wetu mpendwa Magufuli...RIP..
Mi nadhan kwanza wanataka kumyumbisha Rais wetu Mama Samia na utawala wake...sidhani hawaelewi kwamba wananchi majority zaidi ya 85% ndio waliichagua ccm ichukue dola...wale wengine walipigwa kule..inamaana kwamba wananchi wanataka itikadi ya ccm iendeshe nchi.ambayo Ni Ujamaa na Kujitegemea..Ujamaa huu Ni wa kisasa sio ule wa enzi zile..Ujamaa huu unataka njia kuu za uchumi kumilikiwa na umma..keki yoyote ya nchi inaenda equally kwenye huduma kama barabara, hospital, shule..n.k. biashara huria ilimradi iwe halali na ulipe Kodi forodhani..uwepo wa Demokrasia ya kweli...Na wananchi wanahimizwa kujenga chumi zao ili wajitegemee..wasiwe ombaomba...tatizo liko wapi.?.labda tujadili tueleweshane..kwa sababu naamini wananchi wanachoamua wanakielewa sana..Miaka yote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.

Mkubwa sijui kama kweli wewe ni mtanzania. Ukiangalia waliopiga kura sidhani kama walikuwa ni asilimia 85 ya watanzania. Nadhani asilimia 85 unaowataja ni wapiga kura, na si wananchi wote wa Tanzania.

Lakini pia sijui kama unajua maana ya ujamaa, na kuwa ni mfumo wa uchumi na hauna uhusiano na siasa, na sijui kama kwenye unajua kwamba njia kuu za uchumi za Tanzania zinaweza kumilikiwa na watu binafsi na hata makampuni.

Na pia sijui kama kweli unaamini keki ya serikali inagawiwa sawa na kuliwa sawa. Hata ukiangalia shule, hospitali, na barabara ziko tofauti sana...hii ina maana kuwa hiyo keki ina mapande makubwa na madogo.

Na maamuzi ya nchi hii hayajawahi kufanywa na wananchi, kuna watu waliopewa madaraka ya kufanya hivyo.
 
Tofautisha Anti-trust/ competition law na Market structure. Hta US kuna soko huria lakini bado anti trust policies zinakua enforced.
Soko Huria maana yake waache matajiri wafanye chochote...

Market and Economy regulation ni lazima na ni muhimu

Ngoja nikuulize, sijajua itachukua muda gani kujibu

1. Cryptocurrency
Blockchain inaondoa central administration ya kila kitu ambapo inakotumika, it is free and legit technology na hii ndio imetumika kutengeneza Bitcoin, etherium n.k Kwa nini bank kuu zinazikataza ikiwemo benki kuu ya Marekani moja ya Taifa kubwa na Kibepari na linalohamasish free market?

Katika Katiba ya CHAUMA wanasema hawakubaliani na aina yoyote ya soko huria
 
Back
Top Bottom