Tujadili ushiriki wa rais kwenye matamasha kama mgeni rasmi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili ushiriki wa rais kwenye matamasha kama mgeni rasmi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ntemi Kazwile, May 6, 2011.

 1. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #1
  May 6, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kikwete ameweka rekodi kama Rais wa kwanza kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la kwaya pale alipoalikwa kwenye tamasha la pasaka lililoandaliwa na Msama Promotions.

  Sijui kama haya yalikuwa maoni yangu pekee lakini nilishituka zaidi pale ambapo kitendo hiki hakikuhojiwa na waandishi wetu kwenye magazeti... binafsi naona kama kilikuwa kitendo cha kudhalilisha "Urais" kama taasisi kwani ni nadra sana kwa waandaaji wa matamasha kama haya kuweza hata kufikilia kumwalika Rais ambaye yuko busy na akahudhulia. Naomba nikosolewe lakini kitendo alichofanya Kikwete ni cha kujishusha mno ili kujaribu kupata kuungwa mkono na makanisa ambayo yamekuwa yakituhumiwa na mashehe na watu wengine wanaounga mkono serikali yake kuwa hayampendi na yanataka aangushwe....

  Je ni sawa kwa kiongozi mkuu kama Rais kushirikishwa kwenye matamasha ya namna hii??? Mimi nasema si sawa, Rais ana mambo mengi ya muhimu awaachie wasaidizi wake na yeye ashughulike na mambo makubwa ya saizi yake!
   
 2. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  sioni tatizo!! yeye ni Rais wa watanzania wote wa dini zote na makundi yote so lazima ratiba ya shughuli zake iakisi (reflect) hivyo. Labda uniambie kama anahudhuria matamasha kama haya too much hadi majukumu yake mengine yanaathirika otherwisw ni matter ya ratiba tu.
   
 3. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Rais wetu sharabaro, yuko bize na matamasha anaacha uchumi ukiporomoka
   
 4. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Shida yangu ni kuwa tamasha kama la pasaka ni dogo sana kwa level ya Rais na yeye kukubali kuwa mgeni rasmi siyo sawa. Kama akialikwa kwenye kanisa kwa mfano kule Mwanza wakati AIC inatimiza miaka 100, sawa, au shughuli nyingine yenye muonekano wa kitaifa zaidi siyo kikundi fulani kidogo cha wajasiriamali tu wanataka kutangaza biashara zao
   
 5. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  mimi nakubaliana na wewe mkuu! HATAMIMI SIKUPENDA MKUU KUHUDHULIA HUKO SI ANGECHAGUA HATA MWAKILISHI!?
  but nadhani leno lake lilikuwa ni kujisafisha asionekane mdini! wakati yeye ndo kaleta udini!
   
 6. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Huyu Mr nadhani hata utoto wake alikua ni mtu wa kupenda kutumwa tumwa km si kwenda gengeni on behalf of dada zake...na kwa kufuata historia yake wenye hela zao wakamweka kwenye kiti cha ukuu km kivuli ili waendeshe nchi kwa remote!
   
 7. W

  WildCard JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Mzee wetu Mwinyi alikwenda kumuangalia KandaBongoMan miaka ile ya mwanzo wa '90. Mkapa alijifanya kuwa ofisini muda wote akaibuka na Kiwira, EPA,......
   
 8. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Hajui hata umasikini wa tz unasababishwa na nini ataachaje kwenda kwenye matamasha? Mwalikeni Billicanas kwenye uzindizi wa albam ya bongo flava uone kama hajatia timu!
   
 9. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Anatekeleza irani ya uchaguzi ya CCM ya 2015; ndo kazi aliyo nayo sasa hana kazi nyingine....
   
 10. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  anatekeleza irani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 - 2015; kaishiwa nyimbo hajui hata la kufanya sasa ye alifikiri kuongoza nchi ni mchezo; si unajua waswahili hawaachi jadi kwenda ngomani kwa sana.
   
 11. Ciril

  Ciril JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 5,536
  Likes Received: 1,468
  Trophy Points: 280
  Tamasha la Pasaka!!!?
   
 12. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180

  mkuu,kwa ukweli ni udharirishaji wa kiakili. nakuhakikishia ktk matamasha ya wanakwaya yoyote tanzania huwa wanaalikwa maparoko au watawa au wachungaji na kamwe hata ASKOFU mkuu hawezi kukubali mwaliko kama huu, mara nyingi akiona umuhimu wa kwaya iyo atakubali mwaliko ila siku ya siku anamtuma mwakilishi kwa kusema mh askofu amepata dharuram ila kwa kuwa rais wetu ameshasema akili za mbayumwayu au akili za kuambiwa changanya na zako basi muache na akili za mbayuwayu azitumie. Mwinyi kwenda kumuona msanii yeyote ni mapenzi binafsi hata mimi nisingeweza kumshangaa rais kama angeweza kwenda hata kutazama ze Comedy pale sleep way wakati ule waanza comedy, lakini kukubali mialiko kama iyo au ya kufungua shule za primary , chekechea ni aibu kwa taasisi ya juu kabisa. Huwa najiuliza watu kama mugabe au Obama aseme kuna mwaliko wa kwenda kufungua primari kama rais alifanya kule bagamoyo nadhani ingekua fedhea kubwa kwa taif lao, najiuliza mfano kuna tukio kama kuvamiwa na magaidi alaf msafara wake ukadhurika akitoka kwenye kwaya na ikarushwa ktk vyombo vya kimataifa ingekuwa aibu kwa taifa na tangu hapo sijui ni nchi gani ingekuwa na hamu ya kumwalika mtu wa aina yake.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  May 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Urais ni taasisi sio mtu binafsi hivyo ili aweze kufanya kazi na kuleta maendeleo ya nchi ni lazima Rais kuwa karibu za taasisi zote za kisiasa, kiuchumi, kidini na nyinginezo.
   
 14. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #14
  May 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  katika kipindi hiki ambacho baadhi ya watanzania wanaendekeza udini ni muhimu sana kwa Rais kuwa mgeni katika matamasha kama hayo ili kusaidia kupunguza udini miongoni mwetu.
   
 15. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #15
  May 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Rais Mkapa na hata Nyerere wamewahi kualikwa kwenye sherehe za maulid na Idd kwa waislamu na tuliwaona wakitoa hotuba ni jambo jema kwa mshikamano wa kidini nchini kwa msingi huo kuwepo kwa Rais bila kujali dini yake kunaongeza mshikamano wa taasisi za dini.
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  May 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ukitaka nchi isitawalike ukiwa Rais jaribu kujitenga au kukaa mbali na taasisi za kidini. Taasisi za kidini zina wafuasi wengi ambao ni muhimu kwa maendeleo ya nchi ........wakitengwa nchi itayumba.
   
 17. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #17
  May 6, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Napendekeza Rais apunguziwe miariko ili aweze kupumzika na kufanya mambo mengine lakini hoja ya kwa nini alikubali kwenda kwenye tamasha haina msingi.

  kwa watu walio karibu na Rais Kikwete wanasema ni msikilizaji mzuri wa nyimbo za injili pamoja na kwamba yeye ni mwislamu na ndio maana alipokuwa katika tamasha hili hakusika kuchezesha kichwa kulingana na midundo ya nyimbo na alinunua DVD kwa ajili ya kwenda kusikiliza. Lakini pia inaweza kuwa hii imechangiwa na yeye mwenyewe kukiri kwamba amekulia kwenye jamii ya kikristo zaidi wakati wa ujana wake. Kwa mfano, anasema baba yake mzazi mzee Mrisho Kikwete alipokufa akiwa bado mdogo alianza kuishi na baba yake Michael Kikwete ambaye ni mkristo kwa imani ndiye alishiriki kwa kiasi kikubwa ku-shape maisha yake kwa maana ya kuwa baba mlezi.
   
 18. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #18
  May 6, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tofautisha Maulid au kitu kingine cha kitaifa, hili lilikuwa tamasha ambalo halina sura ya utaifa yoyote na kwa rais kuwa mgeni rasmi ni kuudhalilisha urais!
   
 19. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #19
  May 6, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mbu sugu Malaria sugu, raisi rahisi wa kukubali mialiko ya minuso wanafanana fanana ati. Matendo yanasema akili zetu.
   
Loading...