Tujadili udereva wa wana Dar es Salaam

Escrowseal1

JF-Expert Member
Dec 17, 2014
4,533
4,498
Salaam wana Jamvi leo nimeona niwahusishe issue ya uendeshaji wa magari yetu jijini na Tanzania kwa ujumla. Wote tunajua Tanzania yetu ilivyo Taifa bingwa kwa Ajali za barabarani ila naamini mambo madogo madogo yanaweza kuepusha Ajali hizi.

Kuna Jambo moja nimejifunza kwa uendeshaji wetu wa vyombo vya moto na hii mi naichukulia very serious.sijapata kuelewa ni kwa nini sisi watanzania tukisha kaa nyuma Ya usukani almost 90 percent tunabadirika na Kuwa na mtazamo wa Kuwa na haraka wakati in reality si kweli? Kwa nini nasema hivi? Sijaelewa kwa nini kama wote mko mwendo wowote, uwe wa chini wa Kati ama wa juu, mko mlimani, kwenye kona, ama sehemu yenye hali yoyote dereva wengi hawapendi kuona gap ama nafasi mbele Ya gari iliyomtangulia?

Kwa vyovyote vile ata overtake tu .hivi ni kweli kila dereva awae yote huwa yuko na haraka? Haya ni mambo madogo mno ila jamii yetu haina uvumilivu kitu ambacho mi naona ni kama ugonjwa ama si dalili Nzuri kwa jamii yetu na katika kukabili Ajali za barabarani.

Na sielewi kwa nini uharaka wetu pindi tukiwa nje Ya vyombo vya moto hauendani Ya zile haraka tukiwa nyuma Ya usukani.
 
Salaam wana Jamvi leo nimeona niwahusishe issue ya uendeshaji wa magari yetu jijini na Tanzania kwa ujumla. Wote tunajua Tanzania yetu ilivyo Taifa bingwa kwa Ajali za barabarani ila naamini mambo madogo madogo yanaweza kuepusha Ajali hizi. Kuna Jambo moja nimejifunza kwa uendeshaji wetu wa vyombo vya moto na hii mi naichukulia very serious.sijapata kuelewa ni kwa nini sisi watanzania tukisha kaa nyuma Ya usukani almost 90 percent tunabadirika na Kuwa na mtazamo wa Kuwa na haraka wakati in reality si kweli? Kwa nini nasema hivi? Sijaelewa kwa nini kama wote mko mwendo wowote, uwe wa chini wa Kati ama wa juu, mko mlimani, kwenye kona, ama sehemu yenye hali yoyote dereva wengi hawapendi kuona gap ama nafasi mbele Ya gari iliyomtangulia? Kwa vyovyote vile ata overtake tu .hivi ni kweli kila dereva awae yote huwa yuko na haraka? Haya ni mambo madogo mno ila jamii yetu haina uvumilivu kitu ambacho mi naona ni kama ugonjwa ama si dalili Nzuri kwa jamii yetu na katika kukabili Ajali za barabarani. Na sielewi kwa nini uharaka wetu pindi tukiwa nje Ya vyombo vya moto hauendani Ya zile haraka tukiwa nyuma Ya usukani.
Ninakubaliana nawe asilimia 100%. Ni 'utamaduni' wa uendashaji. Utamaduni mbaya, umejengeka lakini unaweza kubadilishwa kwa kubadilisha jinsi asakari wa barabarani wanavyotekeleza majukumu yao. Pendekezo langu la kwanza linahitaji mtaji mkubwa lakini kwa jitihada za JPM za kupunguza ufisadi, pesa itapatikana. Idara ya usalama barabarani ipewe magari na pikipiki za kupatrol sehemu ambazo maadreva wanashawishika kuvunja sheria - iwe ni mijini au barabara kuu za mikoani. Askari wabane kwenye sehemu hizo na wawasimamishe waliovunja sheria kwa kutokea nyuma wakiwa na hivyo vyombo vya patrol (badala ya kuwapungia mkono kana kwamba wanaomba msaada wa lift). Wakiishasimamishwa faini iwe ni kubwa sana kiasi kila atakayekamatwa ataogopa kurudia hilo kosa na yule amabye hajakamatwa ataogopa kujikuta analipa faini hiyo. Utamaduni wa kuheshimu sheria za barabarani utaanza kujengeka na kizazi kijacho kinatafikiri Mwenyezi Mungu ndivyo alivyoumba dunia!

Pendekezo la pili ni kuanzisha usalama barabarani shirikishi ambapo kila mpenda kuona unajengwa utamaduni mzuri kama mleta mada, atapiga picha namba za gari husika na tukio zima kwa kutumia smartphone yake kila akiona madareva wanaokiuka sheria za barabaranai na kuipeperusha moja kwa moja kwa namba ya simu ambayo mkuu wa idara atakuwa ameitoa kwa ajili ya matukio hayo ili wahusika wakamatwe.
Ninafikiri wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo mikoani wameishaanza kushiriki kutunza usalama barabarani kwa kuwatahadharisha madereva kuwa wakienda kwa mwendo kasi au ku-overtake kwenye sehemu hatari, watawaripoti kwa afande (sijui ni nani mkuu wa usalama barabarani). Hapa napo nidhamu itarejea japo pole pole lakini kizazi kijacho kitafikiri Mungu ndivyo alivyoumba huu ulimwengu!
 
Salaam wana Jamvi leo nimeona niwahusishe issue ya uendeshaji wa magari yetu jijini na Tanzania kwa ujumla. Wote tunajua Tanzania yetu ilivyo Taifa bingwa kwa Ajali za barabarani ila naamini mambo madogo madogo yanaweza kuepusha Ajali hizi. Kuna Jambo moja nimejifunza kwa uendeshaji wetu wa vyombo vya moto na hii mi naichukulia very serious.sijapata kuelewa ni kwa nini sisi watanzania tukisha kaa nyuma Ya usukani almost 90 percent tunabadirika na Kuwa na mtazamo wa Kuwa na haraka wakati in reality si kweli? Kwa nini nasema hivi? Sijaelewa kwa nini kama wote mko mwendo wowote, uwe wa chini wa Kati ama wa juu, mko mlimani, kwenye kona, ama sehemu yenye hali yoyote dereva wengi hawapendi kuona gap ama nafasi mbele Ya gari iliyomtangulia? Kwa vyovyote vile ata overtake tu .hivi ni kweli kila dereva awae yote huwa yuko na haraka? Haya ni mambo madogo mno ila jamii yetu haina uvumilivu kitu ambacho mi naona ni kama ugonjwa ama si dalili Nzuri kwa jamii yetu na katika kukabili Ajali za barabarani. Na sielewi kwa nini uharaka wetu pindi tukiwa nje Ya vyombo vya moto hauendani Ya zile haraka tukiwa nyuma Ya usukani.

Hiyo ndio Bongo, hii inachangia sana na Madereva wengi Tanzania kutokufuata Sheria za Barabarani. Na Faini zetu za Barabarani kuwa ndogo.
Pia madereva wengi kutokujua alama aka sign za barabarani.
Mimi kinachonikera zaidi utakuta mtu yupo mbele yako, anaendesha taratibu kuliko hata mwendo unaotakiwa, unapoanza tu kumpita, na yeye anaongeza mwendo kana kwamba mnashindana. wakati alikuwa anaendesha taratibu na kuweka foleni.
My Take: Madereva wote kufuata Sheria zote za Barabarani na kuwa Waungwana wakiwa barabarani. Pia Trafiki na Polisi wetu wa Barabarani kuwa wakali pindi wanapokamata madereva wanaovunja Sheria za Barabarani kwa makusudi.
 
Kwa jinsi nilivyoshuhudia uchukuaji wa LESENI hizi,tunasafari ndefu ya kumaliza ajali.

Bodaboda hawajui hata sheria zinamtaka aendesheje pikipiki akiwa barabarani.Bodaboda na waenda kwa miguu hatujui namna bora ya kutumia barabara,hasa tunapovuka kwenye high way.

Kwenye driving lesson madereva hawaambiwi umuhimu wakusimama au kupunguza mwendo pale anapokaribia Zebra Crossings.Na Zebra Crossings either zimegeuzwa kuwa eneo la kuvushia pikipiki au kituo cha daladala.
 
Mkuu sio Dar pekee Arusha dereva wa gari asilimia kubwa kama vile wanaendesha Treni hawana fair hata kidogo kupisha gari iingie bara bara kuu dereva yupo radhi agonge lakini sio kupisha gari ingine iingie katika iyo bara bara kuu watu wa fair hapa ni wageni na wachache sana wenyeji..
 
Huyo mlete Dar tumfundishe kuendesha gari 'Kiujamaa'...
 
Kuna mtu anamazoea ya kukimbia tu na gari hata kama hana haraka ni hulka yake tena ukute yuko na Subaru atakanyaga mafuta mengi mno ili asikie ule muungurumo wake...Nasema si tatizo kama mtu yupo na control ya kutosha tatizo kuna mwingine anaiga hayo manjonjo ili hali control ni zero...Hapo ndiyo balaa inapoanza na kama hizi Subaru zimewachinja wengi mno..
 
Dar ni mji wenye madereva wa hovyo sana.....ngoja niishie hapa tu maanake nikianza kuelezea uozo wa madereva wa mji huu nitajaza page 100!
 
Ila kuna kaushetani fulani hivi behind the wheel, yaani inatokea tu katika barabara iliyo wazi unataka ufike 100++, Cha msingi ni utii wa sheria na kuwa moderate wakati wote. Niwe katika congestion au niwe pekee barabarani bado nitazingatia kuwa speed si nzuri
 
hivi wakati wanaweka top speed 120 ulifikiri za kupigia picha ?

unaweza kupanda trekta kama hutaki mwendo mkali
 
Back
Top Bottom