Tujadili tamko hili la Waziri wa Mifugo kuhusu usajili wa wafuga kuku

funzadume

JF-Expert Member
Jan 28, 2010
13,559
21,040
Je, utaratibu ukoje?

Je, wafugaji wa wanyama wengine vipi?

Kusajili ni vizuri ila uwekwe utaratibu kwa mifugo yote wafugaji wasajiliwe kuwe na database na sio wafuga kuku wa nyama na mayai. Kuna mifugo mingi nchini
Screenshot_20201231-105349~2.jpg
 
Ifike mahali viongozi wawe wabunifu na kuja na namna ya kufanya kitu kwa kushirikisha na kuelimisha wananchi na sio kuja na tamko la vitisho ili uonekane upo. Huo sio utendaji bora wa kazi. Tunahitaji kiongozi mbunifu na mwenye kuelimisha na sio kukurupuka na kutishia watu wakati hata huo utaratibu wa kusajili wafugaji haujulikani. Amekaa na sera zake huko za mwaka 47 ambazo hata hazijawa communicated kwa wananchi anaanza kutishia

Kwa nini kusiweke utaratibu mzuri wa kusajili mifugo ya aina yoyote ile hapa nchini na wananchi waelimishwe?

Ufugaji ni kitu kikubwa sana na kila jamii inafuga (household activities) kuna watu wanafuga kuku wa nyama au wa kienyeji 20 tu nyuma ya nyumba je naye anasajiliwa? Uchumi wetu unategemea Kilimo (ufugaji ukiwemo ndani yake) so ufugaji unagusa kila kaya. Wamejipanga vipi kimkakati kwenye hili la kuandikisha na kutoa vitambulisho? Wasije kuishia kutoa namba tu kama NIDA
 
Hatimae namimi nacomment Mitano tena

Hivi kwa hawa kuku wangu saba; Sijui natakiwa na mimi nikajisajilii..

Na hiki kitambulisho cha kufuga kuku, sijui kitauzwa sh ngapii... Serikali ni yawanyonge (wanyonge wafuga kuku), hiki kitakua bure hikii..

Ivi inamaana nikiuza mayai bila hicho kitambulisho watu hawatanunua eeh.. masikini mimi.

Ila serikali imeanza kunihurumia, yani inataka inipe kitambulisho ili inikusanye, inipe elimu ya ufugaji, ili nisipate hasara. Serikali imeanza kunipenda sana, haitaki nipate hasara.

Huu uzi una kila sifa yakucomment Mitano Tena
 
Wanasajili wapi??
Gharama za kusajili zikoje?
Kama nafuga kuku wawili je?
Kuku wa biashara?Au hata WA matumizi ya nyumbani?..
Deadline lin?
Na kwa nini kuku tu na sio mifugo mingine? Vipi ng'ombe, bata, mbuzi, kitimoto, inabidi ifanyike kwa mifugo yote na pia kwa kuwa ni suala linalogusa jamii yote basi watoe elimu na utaratibu
 
Na kwa nini kuku tu na sio mifugo mingine? Vipi ng'ombe, bata, mbuzi, kitimoto, inabidi ifanyike kwa mifugo yote na pia kwa kuwa ni suala linalogusa jamii yote basi watoe elimu na utaratibu

Huko Dodoma huwezi watafuta wahusika watupe majibu?
 
Na kwa nini kuku tu na sio mifugo mingine? Vipi ng'ombe, bata, mbuzi, kitimoto, inabidi ifanyike kwa mifugo yote na pia kwa kuwa ni suala linalogusa jamii yote basi watoe elimu na utaratibu
Hii imekaa ndivyo sivyo. Leo nasajili kuku 20 then inaingia kwenye database then mpaka February nimeshakula kuku 10. Je nitawapa taarifa kabla sijachinja kuku wangu? Kama jibu ni hapana je wata update vipi database. Kwa ufupi database ya kuku utakuwa highly unreliable maana stock ya kuku ni very volatile sijui wata monitor vipi.
 
Wafugaji kuku wa
BIASHARA na sio wa nyumbani
Someni basi hio Taarifa hapo
Tumesoma vizuri na kuelewa ila kwa nini asitoe utaratibu na anakuja kutishia? na je kibiashara ni idadi gani? mie mama yangu alinisomesha kwa kufuga kuku wa kienyeji na alikuwa anawauza (walifikia mpk 150) je mfugaji wa aina hiyo anapaswa kusajiliwa?

Kusajiliwa ni suala zuri sana ila je wananchi wanajua kuwa inapaswa kusajiliwa? Kwa nini Waziri usitoe utaratibu instead unakuja kutishia kuchukua hatua huo sio utaratibu mzuri. Unapopewa dhamana na ya Wizara fulani inabidi uongoze kama kiongozi na sio mtishiaji.

Watu walioko chini yako kama hao wafugaji ndio wadau wako wakuu inabidi uwaelimishe na kuwapeleka hatua mbele na sio kuwachukulia kama maadui na kuwatisha kuwachukulia hatua kwa kitu ambacho wala haujakiwasilisha kwa wadau wako.

Mbona Mh. Lukuvi alituelekeza kuhusu kulipa kodi ya ardhi na majengo tukamuelewa utaratibu ukawekwa mpk tukawa tunashinda kwenye foleni kulipia kodi hizo

Waige mifano hiyo sio kuwafanya wadau wako kama maadui, hiyo Wizara imeanza kiajabu sana.
 
Je utaratibu ukoje?
Je wafugaji wa wanyama wengine vipi?

Kusajili ni vizuri ila uwekwe utaratibu kwa mifugo yote wafugaji wasajiliwe kuwe na database na sio wafuga kuku wa nyama na mayai. Kuna mifugo mingi nchiniView attachment 1663632
Nadhani ni jambo la busara mana watz tunakula kuku sana, kwahiyo ni vizuri wafugaji waratibiwe ili wananchi waweza kula chakula salama. Ni vizuri kwa serekali kuwa wazi na kuelimisha jamii na kuleta process rahisi kwa jambo hilo.

Na sio kuku tu mifugo mengine pia inapaswa kujumuishwa. Cha muhimu walete haya mabadiliko kidogokidogo na ata wakileta issue ya kodi isiwe kubwa kiasi cha kumuumiza mwananchi
 
Mimi Nadhani kikubwa hapo kinachotafutwa sio database wala taarifa za kuku nchini

Ni Serikali inaangalia ni kwa Namna gani itapata chochote kitu. Unajua VAT inakatwa kwa Registered companies yoyote inayo zalisha bidhaa Au kutoa huduma frani Mf bidhaa za Bakhresa Au huduma za Vodacom

Hivyo basi kuwasajiri wafanyabiashara wa kuku wa nyama na mayai ni kuifanya Serikali kupata mapato (VAT 18%) kwenye kila kuku Au Yai moja

Mfano Sasa hivi kuku wa broiler ni 6000 mpaka 6500, endapo hili zoezi lao la usajiri litaenda sawa hawa kuku tutegemee kuuzwa 7500 na zaidi, the same kwnye mayai

Binafsi sioni shida katika hilo kabisa
Yani Serikali ipate KODI za kutosha Mimi nichukie Wallah ntakua mwenda wa zimu

Japo hili swala wamelileta kishkaji, Haliko wazi sana than it should be Au pengine no tatizo la muandishi wa hio habari gazetini
 
Tumesoma vizuri na kuelewa ila kwa nini asitoe utaratibu na anakuja kutishia? na je kibiashara ni idadi gani? mie mama yangu alinisomesha kwa kufuga kuku wa kienyeji na alikuwa anawauza (walifikia mpk 150) je mfugaji wa aina hiyo anapaswa kusajiliwa?...

Kweli kabisa wala sikupingi uko sahihi kaka

Tunahitaji Taarifa zaidi Ngoja niwapigie simu watoe ufafanuzi tena hahah
 
Back
Top Bottom