Tujadili takwimu hizi na hatma ya Tanzania

tafiti then jadili

Senior Member
Aug 24, 2006
123
21
Kwa mujibu wa mheshimiwa Idi Simba anasema wamegundua yafuatayo:

-Kuna watanzania zaidi ya milioni 35
-Ni milion 17.5 ambao wana uwezo wa kufanya kazi ambao wapo baina ya miaka 17-60.
-Kati ya hao ni milioni 2 tu ndio wapo katika sekta rasmi wanaotambulika katika utaratibu mzima wa kodi.

-Jumla ya benki zote nchini zilizopo, kuna akaunti laki tatu tu meaning kuna jumla ya watu 1.7milioni ambao wapo katika sekta iliyo rasmi ambao hawana hata akaunti na jumla ya watanzania milioni 34.7 ambao hawana kabisaa account benki.

-Hii inamaana watanzania walio wengi wanashindwa kufaidika na huduma za ziada za benki kama vile mikopo midogo[overdraft facilities] au long term loans.

TAKWIMU NYINGINE ZINASEMA:

-Watanzania 1m huingia katika job market kila mwaka.

-Chama tawala katika ilani yake ni kujenga ajira milioni moja kwa miaka mitano meaning kutakuwa na ajira laki mbili kwa kila ajira milioni moja kwa mwaka kwa hiyo kutakuwa na watu milioni nne hawana ajira katika kipindi cha miaka mitano ijayo mbali ya wale waliokwisha kuwa hawana ajira huko nyuma.;


WAJUMBE TUJADILI...
 
Takwimu hizi za kusikitisha nliwahi kuziona katika invitation message iliyotumwa kuwaalika watanzania kujiunga na Tanzania Economic Forum inayoongozwa na Idi Simba. Ilisema kwamba data hizo wamezichukua kutoka kwa kamati ya fedha na uchumi ya bunge.

Labda hiyo ripoti ya bunge itakuwa imetaja masuala ya criteria, methodolgy na margin of errors katika kupata takwimu hizo.

Binafsi nadhani kwao ni rahisi kuangalia tu wangapi wanalipa income tax na wangapi ni wafanyabiashara wanaofahamika na mamlaka husika na hivyo kuwajumuisha kuwa ndio walio katika sekta rasmi. Au wakulima hawatambuliwi kuwa ni sekta rasmi?

Duh, ina maana ukiondoa hawa milioni mbili ... watanzania waliobaki wote wanaishi kwa ujanja ujanja tu.

Kujua idadi ya benki akaunti nadhani si big deal kwa serikali au kamati ya bunge ,.. ni kuwasiliana tu na benki zetu na kujua kila benki ina wateja wangapi.

Aisee, ina maana mpaka leo nchi yetu inalipa mishahara kwa cash? Mauzo na manunuo pia ni cash tu.

Tuna safari ndefu... labda ndio maana tukahitaji hiyo inayoitwa nguvu, ari na kasi mpya!
 
Kwa jina kamili ni Dr. Haans Kitine!,

sasa kuhusu hizo takwimu na hasa mzee uliyetuwekea who si to blame? Serikali zote tatu zilizopita au wananchi? So siajelewa hata nia na madhumuni ya walioitoa ilikuwa kuwalaumu wananchi au kuilaumu serikali? Wananchi kuishi kwa ujanja ujanja ni kosa la nani? Sio political system yetu ndio imewaruhusu kuishi kwa ujanja ujanja?

Halafu ningewaomba mtuwekee na competitor, yaani na takwimu za nchi nyingine ili tuelewe kwa undani how far we are, tafuteni za Kenya na Uganda ili tuone na tullinganishe kama wenye matatizo kama hayo ni sisi tu?

By the way, Mzee aliyeoa dada wa Mwalimu Nyerere huwa anaitwa Dr. Lawrence Gama!

Hakuna Kulala, Oooooh! I love this forum!
 
Mzee ES,

Heshima yako Mkuu, Kitine na Gama wameingiaje kwenye hii mada? i'm confused!!
 
Duh!! hapa niseme nini ? Maana lazima kujiuliza kwa nini takwimu kama hizo zinapatikana muda baada ya Tanzania kuwa hurua miaka 40 sasa ? Jamani ina maana hatukuwa na serikali makini tangia uhuru ama ni kitu gani ? Je kama JK aliichukua na kuanza kuiweka walio mfuatia na wasomi walio bobea wamefanya nini ? Je Idd Simba baada ya takwimu hizi yeye ana mawazo gani kuwaleta watanzania wengi hata katika nafasi ya banking pekee ? Jamani mweeeeeeeeeee
 
Mzee Mugishagwe

Yeye Idi Simba kuzitoa takwimu hizi ni kuchochea mbinu mbadala zipatikane ili kuweza kuondokana na matatizo ya sasa. Anasema serikali peke yake haiwezi kufanya yote ndio maana wakaanzisha TANZANIA ECONOMIC FORUM ili watu wachangie namna wanavyoweza kushiriki.

In fact wameunda taasisi kuangalia namna watanzania wao wenyewe wanavyoweza kushiriki katika zoezi zima la uwekezaji na kuondokana na kadhia hii.

Naam lengo la takwimu hizi pia ni kuonyesha namna safari ilivyo ndefu nami kuzitoa hapa nimeona na sisi tunaweza kuwa na machache ya kuchangia kuhusu tunavyoweza kubadilisha hali kama hiyo.

BBC wametoa takwimu zao wanasema asilimia 76 ya watanzania wanaishi vijijini katika umasikini wa kutupwa hivyo waungwana tuna safari ndefu.

Lengo kuu hapa nadhani ni bora liwe katika kudevice mbinu za kuondokana na hali kama hii wala sio kumtafuta mchawi ingawa najua wazi kuwa ili kwenda mbele wakati mwingine ni vizuri ukaangalia ulikotoka hivyo nategemea wapo watakaonyooshewa vidole kwa majina na pia wapo watakaohitaji kukosolewa na kulaumiwa lakini kwa ujumla ningeshauri tuelekeze nini kifanyike tusonge mbele.

Mimi nadhani kinachotakiwa kama mmoja alichangia katika thread mojawapo ni kuimarisha kilimo in fact kufanya mapinduzi na kuweka msukumo mpya kabisa. Mheshimiwa Kikwete amekuwa akilaumu wasomi wa kilimo kuwa wanakaa mijini badala ya mashambani...lakini ni vigumu kwa wataalam hawa kukaa mashambani ilhali mambo huko ya kimiundombinu haijawekwa sawa, hawana pa kukaa nk ili tuendelee inabidi idara za serikali ziweke msukumo wa namna hii.

Inawezekana kabla ya mapinduzi ya viwanda barani ulaya karne iliyopita kulikuwa na mapinduzi ya kilimo kwanza-agrarian revolution, vile vile inabidi tukaribishe uwekezaji wa kweli katika eneo hili, nashindwa kuelewa kama viongozi wetu wanafahamu tofauti baina ya uwekezaji na ugenisishaji manake badala ya kubinafsisha kwa wageni mashamba makubwa makubwa nk tungeweza ku-outsource utalaam yaani kuwaita hawa wataaalam wa mvua bandia-artificial rain kuja tanzania, wathai na michele yao waje watufunze...tutoe umuhimu mkubwa katika tafiti za kuboresha.

Nishati imekuwa ni issue tanzania iwe ni maji au mvua...nchi nyingine zinatushangaa wakati wa mvua hutokea mpaka mafuriko bara bara zinakuwa hazipitiki,watu hawaishi kwa raha kukiwa na ukame watu hawakai kwa raha, kwa nini kusiwe na mbinu za kuweza kuhifadhi mvua ile wakati wa masika ili tutumie maji hayo mtera ikikauka?!ni kichekesho kwa wasiojua lakini nchini nyingine zina rain preservation programmes.

Halafu mtera imekuwa ni kisingizio cha kila siku, yani TANESCO hawajakuwa wabunifu kabisa, mgao kila mwaka tangu nipo shule mpaka sasa nakaribia kupeleka wanangu mwenyewe shule!

Yote haya hapo juu yana direct relevance na ukweli wa takwimu za Iddi Simba,lakini na wananchi nasi tunahitaji kubadilika tuwe innovative na tuisukume serikali iende na slogan yake ikishindikana basi sio vibaya kujaribu alternative policies inabidi kuwepo na real change, pace ya changes kwa kweli ipo slow sana hususan katika kilimo.

Bwana Yusuf Kashangwa wa tanzania trade centre london ambacho ni kituo kinachohusika na kuimarisha biashara baina ya tanzania na mataifa mengine sasa aliwahi kusema kuwa alipokea order ya sisal fibre-mkonge tani laki moja kutoka nchi moja ya kiarabu akacheki na nyumbani akaambiwa kwa mwaka nchi nzima inazalisha tani 14,000 tu! ina maana mteja wa tani hizo laki moja ingebidi asubiri takriban zaidi ya miaka mitano! sasa tunahitaji kubadilika kwa kweli...manake hadithi hii ya sisal fibre ni kweli pia katika mazao mengine

Kilimo ni uti wa mgongo wa taifa lakini imekuwa nyimbo tu hakuna linalofanyika..sasa tumeanza kuanza blue prints mpya ya serikali hii ya sasa kuimarisha kilimo tusubiri tuone ingawa nasikitika kwa wajumbe sijawahi kusoma hiyo blue print licha ya kuiomba serikalini hivyo kama kuna ajuae yaliyomo uwanja uwazi amwage hapa tujifunze...
 
Kwa sasa serikali imepiga hatua zaidi inaajiri watu 3000 au pungufu kwa mwaka​
Na hakuna hata nyongeza.
 
Back
Top Bottom