TUJADILI: Prof: Mwandosya na sifa kemkem kwa Rais Kikwete

Nyamtala Kyono

Senior Member
Sep 23, 2010
163
34
Juzi wakati natizama taarifa ya habari ITV niligutushwa na statement ya Mwandosya kuwa, na hapa natoa nukuu isiyo rasmi:
''Semeni yoooote kuwa raisi kikwete hajafanya hiki wala kile kutimiza ahadi za wananchi, ...lakini kikwete ni mtu mzuri na mwema sana kama binadamu,kwa maana yeye ataenda hata kwenye misiba ya watu wa kawaida kabisa,ataenda mahospitali kuwajulia hali waandishi wa habari wa kawida kabisa tena siyo wahariri....'' Mwisho wa kunukuu.

Nilijiuliza maswli yafuatayo:

1. Je raisi kikwete anaweza kwenda kwenye misiba ya raia zaidi ya milioni 45 wa nchi hii?
2. Je mwananchi wa kawaida anajali sana kuhusu nani anaenda kwenye matanga ama misiba ya familia yake?
3. Je kuhudhuria misiba ni muhimu zaidi kuliko mfumuko wa bei?
4. Je kuhudhuria misiba na kutembelea wagonjwa hospitali ndicho hasa wananchi walicho mpigia kura raisi wao akafanye?

Maswali ni mengi sana, wewe pia unaweza kuongeza ya kwako ukiweza.

Kusema ukweli nikaanza ku doubt u-professor wa huyu mheshimiwa, au ndo tuseme bado haja recover vizuri?

wasalaam,

Unafiki ni mbaya sana,huyu Prof ana BIF na JK.
 
Na wala Prof. hakuonyesha kwamba Rais anadhamiria kufanya hivyo. Amezungumzia uungwana wake wa kuweza kushuka hadi kwenye grassroot wakati wengine wasingeweza kufanya hivyo. Wala hakusema kwamba sifa hizi ni substitute ya majukumu yake anayotakiwa kuyafanya kwa mujibu wa nafasi yake au ilani ya uchaguzi ya chama chake. Misintepretation isiyo na lazima hii.
 
hapo kwenye rangi anaweza sababu ni muuza sura
 
Only in tanzania mtu na mkongonja wake and the president can't relive them off their duties!!!! Jamani hivi hakuna wengine wazima ni hao hao tu???
 
Hakuna mtu mwenye mabaya 100% ikionekana mazuri fulani yapo tukubali ndio uungwana huo,hata sisi wachangiaji tuna mapungufu yetu ndo maana mradi wa kuporomosha matusi ni mkubwa hapa JF. Let be real great thinkers for accepting some truth
 
Na wala Prof. hakuonyesha kwamba Rais anadhamiria kufanya hivyo. Amezungumzia uungwana wake wa kuweza kushuka hadi kwenye grassroot wakati wengine wasingeweza kufanya hivyo. Wala hakusema kwamba sifa hizi ni substitute ya majukumu yake anayotakiwa kuyafanya kwa mujibu wa nafasi yake au ilani ya uchaguzi ya chama chake. Misintepretation isiyo na lazima hii.
Nadhani kiungwana professor alitakiwa amwalike mahali wamekaa huku wakinywa chai amshukuru kwa uungwana aliomwonyesha...watanzania hawahitaji uungwana wa style hii...asipokuja kumjulia hali hospitali mtu wangu wa karibu,nikimlaumu kwa kutokuja atakubali?
 
Juzi wakati natizama taarifa ya habari ITV niligutushwa na statement ya Mwandosya kuwa, na hapa natoa nukuu isiyo rasmi:
''Semeni yoooote kuwa raisi kikwete hajafanya hiki wala kile kutimiza ahadi za wananchi, ...lakini kikwete ni mtu mzuri na mwema sana kama binadamu,kwa maana yeye ataenda hata kwenye misiba ya watu wa kawaida kabisa,ataenda mahospitali kuwajulia hali waandishi wa habari wa kawida kabisa tena siyo wahariri....'' Mwisho wa kunukuu.

Nilijiuliza maswli yafuatayo:

1. Je raisi kikwete anaweza kwenda kwenye misiba ya raia zaidi ya milioni 45 wa nchi hii?
2. Je mwananchi wa kawaida anajali sana kuhusu nani anaenda kwenye matanga ama misiba ya familia yake?
3. Je kuhudhuria misiba ni muhimu zaidi kuliko mfumuko wa bei?
4. Je kuhudhuria misiba na kutembelea wagonjwa hospitali ndicho hasa wananchi walicho mpigia kura raisi wao akafanye?

Maswali ni mengi sana, wewe pia unaweza kuongeza ya kwako ukiweza.

Kusema ukweli nikaanza ku doubt u-professor wa huyu mheshimiwa, au ndo tuseme bado haja recover vizuri?

wasalaam,
Nyamtala Kyono

Si mkubwa, msomi, mtoto, si shehe, padre, etc. wote wanafiki wanatazama mkono uende kinywani. Mungu ndie ajuaye mwenye haki
 
Mwandosya kwa wakati huu ingefaa kuangalia afya yake kwanza na kuyaacha hayo mambo mengine yafuate baada ya hali yake kuimalika!!
 
Prof. Mwandosya anaweza kuwa sahihi kabisa kuhusu Jakaya Mrisho Kikwete, kwamba anatembelea wagonjwa, anashiriki kwenye misiba na shughuli zingine za jamii. Kwa kifupi Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu wa watu. Lakini ni vizuri turudi nyuma na kutafakari kwa makini. Watanzania walipanga foleni kupiga kura ya kumchagua rais, na NEC walimtangaza Jakaya Mrisho Kikwete kuwa ameshinda kiti hivyo, hivyo kwa sasa tunamwita Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Watanzania hawakuwa wanamchagua mtu wa kuwajulia hali wakiwa wagonjwa, au kuhudhuria mazishi au mtu wa kunywa naye chai. Rais sio charity worker. Kwenye ilani ya CCM aliyokuwa anatumia Kikwete hakuna mambo ya kutembeleana. Wimbo ulikuwa ni maisha bora kwa kila mtanzania.

Kwa kiasi naweza kuelewa ni kwanini Prof Mwandosya anasema hayo na yuko sahihi kabisa maana vinginevyo angeonekana mtu asiye na shukrani. Lakini atambue kuwa sio kila mtu anapata fursa ya kupata matibabu India. Hata hivyo sidhani kama watanzania wanam-judge Kikwete kama mtu binafsi, ila wanaangalia utekelezaji wa ahadi zake. Prof aangalie nini watanzania waliahidiwa (mbali za ilani ya ccm):
1.Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
2.Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
3.Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
4.Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
5.Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
6.Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
7.Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
8.Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
9.Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
10.Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
11.Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12.Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
13.Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
14.Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
15.Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
16.Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
17.Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18.Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
19.Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
20.Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
21.Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
22.Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
23.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
24.Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
25.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
27.Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
28.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
29.Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
30.Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
31.Kuboresha barabara za Igunga - Tabora
32.Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
33.Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
34.Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
35.Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
36.Kulinda haki za walemavu - Makete
37.Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
38.Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
39.Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40.Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
41.Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
42.Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
43.Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45.Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46.Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
47.Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
48.Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49.Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
50.Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
51.Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
52.Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
53.Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
54.Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
55.Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
56.Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
57.Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
58.Ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
59.Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
60.Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
61.Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
62.Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
63.kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
64.Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
65.Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
66.Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
67.Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
68.Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
69.Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Haahaaa! Siwasikilizi kabisa wanasiasa maana hawamaanishi yale wanayoyatoa mdomoni
 
ni lazima aseme hivyo,
inaonekana bado hajapona vizuri sasa atakimbilia wapi
iwapo mambo yatabadilika ghafla.
 
Mi nadhani ni mkakati wa kujikomba kwa JK si unajua JK ndiyo M/kiti wa Chama na atakuwa anasimamia vikao vya kumchagua mgombea wa kiti cha urais 2015?
 
mengi tu tutaongea lakini tafsiri sasa ya alichoongea au kumaanisha ndiyo muhimu. sikuona akiongea nashindwa kuchangia kwani inaweza kuwa ni tafsiri ya mtuma thread kama alivyoelewa
 
Kulingana na uzoefu wangu kwa wasomi katika level ya uprofesa, unatakiwa kuchambua neno kwa neno na mazingira yanayowazunguka ilikupata maana. La sivyo, unaweza fikiria umeelewa kumbe umelewa tu.
 
Halafu last week, kuna mtu alikuja na hoja kwamba huyu Professor ndiye anafaa kuwa next president of URT.
Mimi nikasema I quote again "Insanity is to repeat the same thing expecting different results. CCM are all alike,
let us look outside the box. No disrespect to the Professor, lakini I pray that huo ugonjwa haujatafuna
mendula oblongata yake, labda ndiyo maana anatoa matamshi kama ya akina Tabwe Hizza!
 
Back
Top Bottom