Tujadili njia za kumsaidia mtoto kuongeza IQ yake katika ukuaji

said1994

Member
Dec 3, 2016
99
35
Habari za asubuhi wanajamvi,

Nimeleta uzi hapa naamini nitapata msaada wa kimawazo. Kwa kawaida katika makuzi ya watoto malezi yanatofautiana na hivyo kuleta tabia tofautitofauti baina ya familia moja na nyingine au jamii moja na nyingine.

Hoja yangu ni kuhusu kuongeza IQ, Creativity and Innovation kwa watoto. Je, kuna njia gani/ hatua gani anazotakiwa kuzichukuwa mzazi au mlezi ili aweze kufanya apate mtoto wenye IQ kubwa, creativity, Innovations kwa kiwango cha juu maana nimejaribu kupitia kitabu kilichoandikwa na Edward De Bono kinaitwa Think Before It's Too Late.

Anazungumzia kuwa Creativity, Innovations and Designing Thinking zinaweza tengenezwa na kumfanya mtu awe bora kwenye Field yake ningependa wataalamu wa malezi/ Child psychology wanipe Hints au njia anazoweza tumia mzazi/mlezi kuongeza IQ ya mtoto, mathalani mtoto awe chini ya miaka 10 awe anauwezo wa kufikiri, kujenga hoja sawa na mtu mwenye 20s.

Ahsante.
 
Afya ya mama kabla na wakati wa ujauzito plays a big role. Wakati wa ujauzito hasa wakati wa kuundwa kwa ubongo, mazingira yawe ya kiafya. Baada ya hapo lishe ya mama iendelee kuzingatia afya. Sio wakati wa ujauzito mama K anakula udongo, chips na pepsi na unadhani mtoto akizaliwa ndio uanze kutengenezea ubongo bora!!! No. Kanazaliwa kakiwa mentally fit ila unafanya kuimarisha tu kilichopo.
 
Zingatia chakula bora protein kwa wingi na vitamin vyengine.. ila iwe kwa kiasi kiujumla ni balance diet. Mazoezi ya mwili na akili.. Kuna michezo itakayomtafakarisha pia magemu mpe Yale ya kutumia akili Kama sokoban n.k Kuna vitu muweke navyo mbali kwanza hasa kama hakuna ulazima wa yeye kutumia teknolojia za simu n.k usimpe kwa asilimia Mia! Mpk uhakiki amevielewa nini ni nini..!! Pia kama itawezekana Kama unauwezo mpatie nafasi ya kujifunza kupiga kinanda ama gitaa ila Kama atapenda.

Ukiwa Kama mzazi unajukumu la kumfundisha mwanao muda ni nini na anatakiwa autumie vipi.. hili muelekeze kwa vitendo na si maneno tu,mnunulie vitabu asome,unajua vya kumchagulia.

Nje na hayo unajukumu hili pia ni lazima umuelewe mwanao! Kwa maana ya personality yake kisaikolojia jifunze makundi manne ya kisaikolojia itakusaidia kujua mwanao anasifa zipi na umpeleke vipi.. hichi ni kiini Cha nini umfanyie mwanao.. saikolojia imebaba umaana wa maisha yake! Utafahamu udhaifu na utimilifu wake na kipi umpatie nguvu kukijua na kipi ukiache.. jifunze saikolojia ya makundi ya watu hata wewe itakusaidia.. yangu ni hayo.
 
Ahsante sana
 
Lakini pamoja na mambo hayo yote, nyie Wazazi lazima muwe Role Model wa Watoto! Brain ya mtoto inajifunza kutokana na mazingira mtoto aliyomo!

Mzazi ukiwa hufuatilii malezi ya mtoto esitegemee hata hio IQ kuwa kubwa. IQ ni selection ya mambo mengi kwa mtazamo wangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom