Tujadili njia za asili za kufukuza au kuzuia nyoka shambani au nyumbani kwako

Nilipata kusikia kuna mti unaitwa mnyokanyoka, ukiupanda nyoka hawasogei.
Binafsi sijawahi kuujaribu wala kuuona kwa yakini.

Ipo kuna sehemu inaitwa Igando au Iyayi Sijui ni wilaya gani ile ila ukiwa waelekea Mbeya kutokea Makambako ni kama Km 40 hivi au ukiwa watokea Igawa kuelekea Makambako ni kama Km 20 nadhani.
 
Wakuu habari,

Naomba tupeane uzoefu wa njia za asili za kuzuia nyoka wasiingie shambani kwako au nyumbani kwako, nafahamu kuna baadhi ya wanyama wanakula nyoka lakini hawawezi kuzuia nyoka kuingia shambani au nyumbani, nafahamu pia kuna dawa za kitaalamu ambazo ukinyunyiza nyumbani au shambani kwako zinapunguza kwa kiasi kikubwa nyoka kwenye shamba lako lakini dawa hizo zina madhara na ni gharama kubwa sana, ninaposema njia za asili ninamaanisha kupanda mimea fulani, kwa mfano ukipanda pilipili kuzunguuka shamba tembo hawasogei kwenye shamba lako, asanteni
Mafutataa na moshi wa plastic materials
 
Kuna dawa ya mti shamba mim naifaham, ukikichukua kijiti chake ukakichomeka ardhini kikiwa juu chini au chini juu apo ata nyoka mkubwa awe umbali wa mita 200 hawez kusogelea eneo hilo. Nyoka atakikimbia icho kijiti kuanzia umbal wa mita 200 labda. Kwahiyo bas kama ukikichomeka nyumbani/shambani kwako utakua umemfukuza nyoka umbali wa mita 200
 
Ipo kuna sehemu inaitwa Igando au Iyayi Sijui ni wilaya gani ile ila ukiwa waelekea Mbeya kutokea Makambako ni kama Km 40 hivi au ukiwa watokea Igawa kuelekea Makambako ni kama Km 20 nadhani.
Mkuu umewahi kuona inavyofanya kazi kwa sababu nataka kuifuata nikachukue kwa wingi kwa ajili ya shamba langu
 
Kuna dawa ya mti shamba mim naifaham, ukikichukua kijiti chake ukakichomeka ardhini kikiwa juu chini au chini juu apo ata nyoka mkubwa awe umbali wa mita 200 hawez kusogelea eneo hilo. Nyoka atakikimbia icho kijiti kuanzia umbal wa mita 200 labda. Kwahiyo bas kama ukikichomeka nyumbani/shambani kwako utakua umemfukuza nyoka umbali wa mita 200
Hiyo njia itahitaji approval ya Mshana Jr 😃😂😃😂
 
Labda nitoe mfano mwingine, ukitaka kuzuia kanga au kwale shambani mwako, chukua gongo kali au konyagi changanya na pumba weka kwenye shambani mwako halafu subiri, wakila tu yaani unawakamata kama kumbikumbi na kuwaweka kwenye magunia na kwenda kuwabanika kwa ajili ya kitoweo na kugawa kwa ndugu, jamaa na marafiki

NB; wakuu hii sio mada tafadhali tujadili mada hiyo hapo juu
Elimu ya kwanza nikiwa ndo naamka
 
Back
Top Bottom