mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,037
Hii ni kero namba moja ya muungano ya muda wote!! Kwa bahati mbaya haijaorozeshwa wala hakuna mpango wa kuiorodhesha miongoni mwa kero za muungano.
Juzi juzi tumefanya sherehe ya kumbukizi la miaka 60 ya uhuru wa "Tanzania", au wakiona aibu wanasema kumbukizi la uhuru wa "Tanzania bara"!! Lakini ukiwauliza Tanzania au Tanzania bara ilikuwa inatawaliwa na mkoloni gani?
hawana jibu!!!! watakuambia huo ni uchochezi.
Tumeamua kuificha historia yetu kwa kuifunika kwa kioo!!! Tumeifunika lakini inaonekana wazi.
Binafsi naukubali muungano, lakini hii kero ishughulikiwe.
Najivunia Utanganyika wangu kama wanavyojivunia Uzanzibari wao kabla ya wote kujivunia Utanzania wetu!!