Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Tutaoaje kwa take home hizi hatutaki kulaza njaa watoto wa watu. Ngoja tununue hadi hali itakapokaa sawa
Kama ni hivyo watu wasingeoana huku kitaaa.

Pesa hiyo haitoshi ila unatakiwa uishi kulingana na kipato chako.
 
Tatizo linaanzia hapa kwa sisi vijana tunaoajiriwa. Tunataka tupate ajira Leo mwakani tuanze kujenga. Na hapo lazima mshahara uwe mdogo tu. Kujenga ni process inatohitaji muda mrefu kidogo ikitegemeana na mshahara na majukumu mengine ya lazima.
Wengi wenye uhakika wa kulipa kodi hawana haraka ya kujenga mapema sababu wana uhakika
 
Kuna vitu hujaweka wazi hapa kama hii habari yako ni ya kweli
1. Hela ya kununua canter
2. Hela ya kujenga nyumba standard
Zimetoka wapi maana kwa maelezo yako una ng'ombe 6 na duka moja. Kuna kitu unatuficha hapa.
Tena cha kuongeza tu hapo anasema miaka mitano yoka 2015 ambayo ni 2020 alikuwa na madume ya ng'ombe ma 5 ameyatuma kijijini, sasa anasema leo ana canter na nyumba standard yaani ndani ya mwaka mmoja sio ?
 
Nilisoma sheria ajira zikawa ngumu ilinibidi nijichanganye na postgraduate ya ualimu, then niliajiriwa as mwalimu 2015 , cha kwanza nilipanga karibu na kituo cha kazi tena single room nikajiapiza sitaoa na kipato hicho, no TV, gas ndogo , nilikuwa napika , then nikawa nimeunda kikundi cha kuchangiana kila mwezi laki mbili, nilikuwa wa mwisho nilipata million moja, then nikakopa million moja na nusu bank, nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa chumba sebule hapo nilijenga mwaka , nilihamia humo kama ndege , then mwaka wa tatu nilianza kununua ngombe dume nawatumia watu home wanafuga, mwaka wa tano nilikuwa na madume kama watano nilipowauza nilifungua duka na kisha nikakopa milioni 1010000 then nilianza kununua mitamba na kuwapa watu kule home, Leo hii umri wangu 35 Naoa mwaka huu, Nina mashamba kwetu makubwa as mkulima mkubwa, nimejenga nyumba standard tu mjini, namiliki canter na Nina mifugo mjini ,Nina duka kubwa tu ,nasomesha watoto wangu 1 na wajomba 2 ila salary yangu ni 249000,_so pambana tu mzee utafika huo mtaji ni mkubwa
Uliajiriwa mwaka 2015
~Mwaka wa tatu (means 2018) ulinunua ng'ombe
~Mwaka wa tano (means 2020) ulikua na ng'ombe 5 ukauza wote ukafungua duka
~Sasa hivi (means hii miezi miwili ya 2021) unamiliki duka kubwa,mashamba makubwa, nyumba standard na una canter. Kumbuka mshahara ni ule ule 249k
Mkuu unafaa kuwa motivational speaker

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Uliajiriwa mwaka 2015
~Mwaka wa tatu (means 2018) ulinunua ng'ombe
~Mwaka wa tano (means 2020) ulikua na ng'ombe 5 ukauza wote ukafungua duka
~Sasa hivi (means hii miezi miwili ya 2021) unamiliki duka kubwa,mashamba makubwa, nyumba standard na una canter. Kumbuka mshahara ni ule ule 249k
Mkuu unafaa kuwa motivational speaker

Sent from my SM-A217F using JamiiForums mobile app
 
Tena cha kuongeza tu hapo anasema miaka mitano yoka 2015 ambayo ni 2020 alikuwa na madume ya ng'ombe ma 5 ameyatuma kijijini, sasa anasema leo ana canter na nyumba standard yaani ndani ya mwaka mmoja sio ?
Huyu muongo tu, anafikiri kila mtu ni mjinga humu bei ya canter na nyumba standard ni zaidi ya milioni 100. Hao ng'ombe alikuwa analimisha au anauza maziwa?
 
MIMI nilikuwa ninapata laki 4 na nyumba nikawa nimepanga ya laki na nusu na sijawahi kuyumba, nilipanga jirani na kazini kuliko kupanga mbali kwa elfu 60 halafu nauli ukijumlisha kwa mwzi ni yaleyale bora upange jirani
 
Ulikuwa wilaya gani?
 
TGS D ni kiwango cha mshahara kwa mtumishi mwenye shahada ya kwanza anaefanya kazi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa (halmashauri). Baada ya makato ya PAYE, NHIF na TUCTA kiasi kinachobaki ni around Tshs. 540,000/-. Hapo sijaweka makato ya HESLB.

Sasa hapa tuijadili hii 540,000 inayobaki. Je, inaweza kuendesha familia kwa watumishi walio mjini DSM, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya?

Kwa jinsi gani kiasi hiki kinaweza tosha:
1. Kulipa kodi ya nyumba
2. Chakula cha familia mwezi mzima
3. Nauli ya mtumishi kwenda na kurudi kazini hasa DSM
4. Mavazi ya familia
5. Chakula cha mtumishi akiwa kazini
6. Elimu ni bure ila kuna nauli na hela ya kula mtoto kila siku
7. Bili ya maji, umeme na king'amuzi

Leteni uzoefu hapa mnawezaje kumudu haya yote?

Karibu kwa mchango wako
Hivi kumbe wafanyakazi wa Tanzania mnaishi maisha magumu kiasi hiki !
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom