Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Nilisoma sheria ajira zikawa ngumu ilinibidi nijichanganye na postgraduate ya ualimu, then niliajiriwa as mwalimu 2015 , cha kwanza nilipanga karibu na kituo cha kazi tena single room nikajiapiza sitaoa na kipato hicho, no TV, gas ndogo , nilikuwa napika , then nikawa nimeunda kikundi cha kuchangiana kila mwezi laki mbili, nilikuwa wa mwisho nilipata million moja, then nikakopa million moja na nusu bank, nikanunua kiwanja na kuanza ujenzi wa chumba sebule hapo nilijenga mwaka , nilihamia humo kama ndege , then mwaka wa tatu nilianza kununua ngombe dume nawatumia watu home wanafuga, mwaka wa tano nilikuwa na madume kama watano nilipowauza nilifungua duka na kisha nikakopa milioni 1010000 then nilianza kununua mitamba na kuwapa watu kule home, Leo hii umri wangu 35 Naoa mwaka huu, Nina mashamba kwetu makubwa as mkulima mkubwa, nimejenga nyumba standard tu mjini, namiliki canter na Nina mifugo mjini ,Nina duka kubwa tu ,nasomesha watoto wangu 1 na wajomba 2 ila salary yangu ni 249000,_so pambana tu mzee utafika huo mtaji ni mkubwa
Kuna vitu hujaweka wazi hapa kama hii habari yako ni ya kweli
1. Hela ya kununua canter
2. Hela ya kujenga nyumba standard
Zimetoka wapi maana kwa maelezo yako una ng'ombe 6 na duka moja. Kuna kitu unatuficha hapa.
 
Sisi wa Dodoma tusubiri uzi wetu.

Ila Dodoma wanaume wasio na kipato cha kueleweka sijui wanaishije maana mji mgumu huu.
Sisi wanawake ni mtelezo tu.

Mungu awasimamie wanaume zetu mlioko Dodoma. Tuko pamoja, hatuwaachi.
Asee.....pruuuuu mpaka maka
 
Ikifika zamu ya kutujadili sisi migambo tunaofanya kazi Posta(jijini) na kuishi Mbagala(Mkoani) nitatia neno. Na mshahara wetu ni laki mbili na nusu hadi laki 3.

Sent from my Infinix X623 using JamiiForums mobile app
Mgambo ni Semi skilled job kwa hiyo huo mshahara unawatosha Sana.Hebu chunguza huyo wa 540,000/=,anakaa darasani kwa muda gani?,halafu jilinganishe na wewe sasa.
 
Kuna vitu hujaweka wazi hapa kama hii habari yako ni ya kweli
1. Hela ya kununua canter
2. Hela ya kujenga nyumba standard
Zimetoka wapi maana kwa maelezo yako una ng'ombe 6 na duka moja. Kuna kitu unatuficha hapa.
Kuna mwamba hapo@Pohamba kacoment Good morning nadhani umepata picha mkuu.
 
Back
Top Bottom