Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Hapo hapo ofsini kwenu Kuna mlinzi wenu analipwa take home
270,000
Amejenga, ana mke na anasomesha watoto watano.

My take:
Hakuna mshara mkubwa Wala mdogo, Ni suala la vipaumbele vya matumizi litakalowatofautisha mfanyakazi uyu na Yule kimaendeleo
Na mlizi huyo huyo anaweza hata kumnyandulia mke wake, tena kwa kumpeleka hadi guest za Buza Kwa Mpalange! Maisha hayapo fair
 
Yaan we unaanza kazi tu unaanza kuwa na majukumu makubwa ,familia watoto wanasoma etc...
Unafahamu Wafanyakazi walio ajiriwa kuanzia mwaka 2014 mpaka leo bado hawajapandishwa madaraja/ vyeo vya kimuundo! na hivyo kuishi kwa mshahara ule ule wa TGS D sawa na hawa walio ajiriwa 2021?

Kwa hiyo unategemea mfanyakazi aliyeanza kazi mwaka 2014 mpaka mwaka huu wa 2021 bado awe tu hana familia au mtoto anayesoma?

By the way, kuna wahitimu wengine wanamaliza shule/vyuo wakiwa tayari wana familia kutokana na ukweli kwamba umri una waruhusu kuwa na hizo familia!
 
Mleta mada atakuwa mtoto wa mama alizoea kupewa pocket money laki mbili kwa mwezi kula kulala bure nyumbani chumba self contained cha peke yake anatumia gari ya wazazi mzazi anajaza mafuta na kila kitu .Umeme maji nk mzazi sasa akipangiwa kazi na mshahara laki tano anataka aishi maisha yale yale apate nyumba self contained yenya kasebule ka peke yake ale buffet na pizza nk kama alivyokuwa akila kwa wazazi haipo hiyo!! Nina mtoto wa jirani alikataa kwenda mbinga kikazi ualimu shule ya msingi akawa anatukana wazazi wake kuwa wana vyeo vikubwa lakini hawampendi akasema kwa nini nisipangiwe Dar es salaam? akaulize kazi ya vyeo vyenu vikubwa ni nini kama hamnisaiidii mtoto wenu wakabaki wanatoa machozi tu sababu hata hiyo ajira kuipata ni Mungu aliyesaidia .Hawakujua hata watafanyaje baada ya kumaliza course ya ualimu

Kuanza maisha inatakiwa kushuka ndio maana kunaitwa kuanza maisha ulizoea kukaa kwa watu sasa zamu yako kuanza na wewe maisha!! Panga sehemu zinaoendana na kipato na uishi maisha ya kawaida tu digrii yako is not a big deal hata vijijini sasa hivi ziko kibao watu wanazo hawana kazi
Una undugu na Mzee Yusuph? Mbona unapenda sana Taarab! Yaani walau hiyo paragraph yako ya mwisho ndiyo kidogo umeandika point! Ila hilo liparagraph lako refu la mwanzo, limejaa vijembe tu na taarab nyingi! Aaaaaahhhh!😫😫
 
Unafahamu Wafanyakazi walio ajiriwa kuanzia mwaka 2014 mpaka leo bado hawajapandishwa madaraja/ vyeo vya kimuundo! na hivyo kuishi kwa mshahara ule ule wa TGS D sawa na hawa walio ajiriwa 2021?

Kwa hiyo unategemea mfanyakazi aliyeanza kazi mwaka 2014 mpaka mwaka huu wa 2021 baso awe tu hana familia au mtoto anayesoma?

By the way, kuna wahitimu wengine wanamaliza shule/vyuo wakiwa tayari wana familia kutokana na ukweli kwamba umri una waruhusu kuwa na hizo familia!
Ukisikia uchawi ndio huo anaoufanya jamaa.
 
Achana nae huyo bado amekariri formula : kuzaliwa, kusoma, kupata kazi, kuoa, kuzaa.
Siku hizi mambo yamebadilika
 
Mlinzi akijenga chumba kimoja huku umri wake 50's unasema maendeleo?
Kwani wee ulitakaje labda?
Ajenge bangaloo au?

Au hujawaona waliostaafu (60s) hawana hata kiwanja achilia mbali hata icho chumbani kimoja alichonacho uyo mlinzi.

Tujifunze kuappreciate ata kwa vile vidogo walivyofanikiwa wenzetu.

Kwa maana hawajavipata kirahisi wamepambana Sana mpk kufika pale kwa levo yao.
 
Huyo mlinzi aliyejenga ukifatilia utakuta alikuwa askari mstaafu ila sio hawa wa miaka 20-25.
Tatizo linaanzia hapa kwa sisi vijana tunaoajiriwa. Tunataka tupate ajira Leo mwakani tuanze kujenga. Na hapo lazima mshahara uwe mdogo tu. Kujenga ni process inatohitaji muda mrefu kidogo ikitegemeana na mshahara na majukumu mengine ya lazima.
 
Back
Top Bottom