Tujadili mshahara wa TGS D kwa watumishi wanaoishi kwenye majiji

Elewa mshahara ni kwa ajili ya dhamana ya kukopea, maisha usukumwa kwa urefu wa kamba.
 
TGS D ni kiwango cha mshahara kwa mtumishi mwenye shahada ya kwanza anaefanya kazi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa (halmashauri). Baada ya makato ya PAYE, NHIF na TUCTA kiasi kinachobaki ni around Tshs. 540,000/-. Hapo sijaweka makato ya HESLB.

Sasa hapa tuijadili hii 540,000 inayobaki. Je, inaweza kuendesha familia kwa watumishi walio mjini DSM, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya?

Kwa jinsi gani kiasi hiki kinaweza tosha:
1. Kulipa kodi ya nyumba
2. Chakula cha familia mwezi mzima
3. Nauli ya mtumishi kwenda na kurudi kazini hasa DSM
4. Mavazi ya familia
5. Chakula cha mtumishi akiwa kazini
6. Elimu ni bure ila kuna nauli na hela ya kula mtoto kila siku
7. Bili ya maji, umeme na king'amuzi

Leteni uzoefu hapa mnawezaje kumudu haya yote?

Karibu kwa mchango wako
Ama kweli binadamu hatosheki..waliwahi kusema wahenga wa Kiswahili..ukute kabla ya kupata hiyo kazi umelialia sana kwa kukosa kazi.
 
  • take home ya 540,000 ni Pesa ndogo Sana
  • yaani bodaboda kumbe Wana Hela kuliko maafisa wa halmashauri, Kwa maana Kuna bodaboda kibao nawajua wanalaza 30,000/-+ Kwa mwezi kupata 900,000/- Sio issue, kunaa makondakta wanalaza 30,000/-+ Kwa siku
  • Fanya mpango utafute ajira nyingine yenye Pesa au Fanya ujasiriamali.
 
Omba uamisho uende kijijin au wilayani huko mikoani piga kazi mpaka ukifika tgs h au above hamia dar.
Njia ya pili ishi chini ya kipato yaani chini ya tgs d wekeza miradi midogomi dogo na hifadhi Kadri uwezavyo.
 
TGS D ni kiwango cha mshahara kwa mtumishi mwenye shahada ya kwanza anaefanya kazi Serikali Kuu na Serikali za Mitaa (halmashauri). Baada ya makato ya PAYE, NHIF na TUCTA kiasi kinachobaki ni around Tshs. 540,000/-. Hapo sijaweka makato ya HESLB.

Sasa hapa tuijadili hii 540,000 inayobaki. Je, inaweza kuendesha familia kwa watumishi walio mjini DSM, Arusha, Mwanza, Tanga na Mbeya?

Kwa jinsi gani kiasi hiki kinaweza tosha:
1. Kulipa kodi ya nyumba
2. Chakula cha familia mwezi mzima
3. Nauli ya mtumishi kwenda na kurudi kazini hasa DSM
4. Mavazi ya familia
5. Chakula cha mtumishi akiwa kazini
6. Elimu ni bure ila kuna nauli na hela ya kula mtoto kila siku
7. Bili ya maji, umeme na king'amuzi

Leteni uzoefu hapa mnawezaje kumudu haya yote?

Karibu kwa mchango wako
Hii nchi INA kazi ya ziada!!! Yan MTU unakaa unajadiki kitu kisicho na faida kwako hata 0/1% !??? Duuu
 
  • take home ya 540,000 ni Pesa ndogo Sana
  • yaani bodaboda kumbe Wana Hela kuliko maafisa wa halmashauri, Kwa maana Kuna bodaboda kibao nawajua wanalaza 30,000/-+ Kwa mwezi kupata 900,000/- Sio issue, kunaa makondakta wanalaza 30,000/-+ Kwa siku
  • Fanya mpango utafute ajira nyingine yenye Pesa au Fanya ujasiriamali.
Boda boda wa wapi mkuu wanalaza 30k+ kwa siku nitume watu waje wapige kazi huko mkuu.?
 
  • take home ya 540,000 ni Pesa ndogo Sana
  • yaani bodaboda kumbe Wana Hela kuliko maafisa wa halmashauri, Kwa maana Kuna bodaboda kibao nawajua wanalaza 30,000/-+ Kwa mwezi kupata 900,000/- Sio issue, kunaa makondakta wanalaza 30,000/-+ Kwa siku
  • Fanya mpango utafute ajira nyingine yenye Pesa au Fanya ujasiriamali.
Mdanganye mwenzio bodaboda gani analaza 30000

Sent from my TECNO K9 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom