Tujadili Mradi wa magadi wa ziwa Natron

Idimi

JF-Expert Member
Mar 18, 2007
14,888
10,371
Ujenzi wa kiwanda cha magadi Ziwa Natron ni wa kuutilia shaka
2007-10-11 10:18:38
Na Johnson Mbwambo wa JET

Mwingereza mmoja mwenye asili ya Ireland, John Nolan, alipata kunukuliwa na gazeti moja kubwa la nje akisema kwamba; Tanzania ndiyo nchi pekee duniani ambayo Mzungu anaweza kuingia akiwa mikono mitupu na kuondoka akiwa bilionea!.

Mzungu huyo ndiye yule aliyeendesha mapambano makubwa dhidi ya Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET) ambacho kilikuwa kikipinga mpango wake wa kufungua mashamba ya kamba (prowns) katika Delta ya Rufiji, mpango ambao kama ungetekelezwa ungewaacha mamia ya wavuvi masikini katika Delta hiyo kuwa masikini zaidi.

Pamoja na serikali ya awamu ya tatu ya Benjamin Mkapa kuupitisha mradi huo Ireland, JET na wanaharakati nchini, wakiungwa mkono na jumuiya za kimataifa, walisimama kidete kuupinga mradi huo na hatimaye serikali ikasalimu amri.

Ni vigumu kutoikumbuka kauli hiyo ya John Nolan unapotafakari kasi ya sasa ya kukaribisha uwekezaji wa kigeni katika maeneo mbalimbali nchini bila kujali athari za muda mrefu za mazingira ya maeneo hayo.

Moja ya mambo yanayosaidia sana kuitangaza Tanzania nchi za nje na kuiingizia mamilioni ya pesa za kigeni, kwa miaka mingi tu, ni vivutio vyake vya kitalii.

Mungu ameijalia nchi hii kwa kuipa mbuga, maziwa, misitu na hata milima yenye viumbe hai ambavyo havipatikani sehemu nyingine duniani.

Na ni mbuga hizo na viumbe hai hivyo ambavyo vimekuwa, kila mwaka, vikiwavuta kuja nchini watalii na watafiti kutoka sehemu mbalimbali duniani, na kwa njia hiyo kuliingizia taifa mamilioni ya pesa za kigeni.

Kwa mujibu wa takwimu za Wizara ya Maliasili na Utalii, zilizotolewa bungeni, hivi karibuni, kwa mwaka 2006 tu Tanzania ilipata watalii 644,124 walioiingizia nchi jumla ya dola za Kimarekani milioni 862.

Kinachowaleta watalii hao hapa nchini ni wanyamapori na viumbehai wengine wasioonekana kwingineko duniani; lakini sasa Tanzania imenasa katika mtego wa uwekezaji wa kigeni katika mbuga na maeneo mengine yenye maliasili hizo kiasi kwamba miaka si mingi wanyama na viumbe hai hivyo vitakimbia na kuufanya uwepo wao hapa nchini kubakia kuwa ni historia.

Lengo la Serikali, kwa mujibu wa bajeti ya wizara hiyo ya mwaka 2007/2008, ni kuongeza idadi ya watalii kufikia milioni 1.2 ifikapo mwaka 2012.

Mkakati mkuu wa Serikali katika kulifikia lengo hilo ni kuongeza idadi ya hoteli za nyota tano katika mbuga za wanyama.

``Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kuwakaribisha wawekezaji wenye uwezo wa kujenga hoteli za nyota tano katika mbuga zetu na katika maeneo yanayozunguka mbuga zetu,`` ndivyo Waziri wa Wizara hiyo,Prof. Jumanne Maghembe alivyoliambia Bunge wakati akiwasilisha bajeti yake, Julai mwaka huu.

Lakini sote tunajua kwamba huwezi ukajenga hoteli kubwa za kitalii za nyota tano katika mbuga za wanyama, ukajenga na barabara kubwa na hata viwanja vya ndege vikubwa ndani ya mbuga hizo, na kisha ukatarajia wanyamapori waendelee kuwepo hapo.

Lakini hivyo ndivyo serikali ya Tanzania inavyofanya. Mwekezaji na tajiri wa Uarabuni ameruhusiwa kujenga hoteli kubwa ndani ya mbuga, na sasa kuna mpango wa kujenga barabara kubwa ndani ya mbuga ya Serengeti na pia kualika wawekezaji wengine wa nje kujenga hoteli nyingine zaidi za nyota tano ndani ya mbuga hizo.

Huhitaji kuwa mtaalamu wa mazingira kujua kwamba vyote hivyo vitafanya shughuli za binadamu ndani ya mbuga hizo kuongezeka, na hivyo kuwafanya wanyama kuhamia kwingineko (Kenya?!).

Je, bila kuwepo kwa wanyama hao, mtalii gani atatembelea hoteli hizo za nyota tano ndani ya mbuga? Nani kaiambia Serikali ya Tanzania kwamba watalii wanafuata hoteli za nyota tano ndani ya mbuga za wanyama?

Si kweli kwamba kwao wana hoteli nzuri zaidi kuliko zilizopo hapa nchini? Si kweli kwamba wanachokifuata nchini ni wanyamapori katika mazingira yao ya asili na si hoteli za kifahari?

Ni jambo linaloeleweka wazi kwamba kadiri shughuli za binadamu zinavyoongezeka katika maeneo ya pori, ndivyo pia wanyamapori na viumbe hai vingine vinavyozidi kuyakimbia maeneo hayo kuwakwepa binadamu.

``Mradi wowote ule ambao huhusisha kusafisha eneo kubwa la ardhi na kuondoa forest cover, si wa kuuendekeza; vinginevyo, tutamaliza uoto wa asili na kuwafanya wanyamapori wetu na viumbe hai vingine kuondoka,`` anasema Rais wa Chama cha Wataalamu wa Misitu Tanzania (TFA), Dk. Felician Kilahama.

``Mbuga ya Serengeti imeingizwa katika orodha ya maeneo ambayo ni Urithi wa Dunia (World Heritage Site), na pia ni moja ya maajabu saba ya dunia.

Ni wazi itapoteza sifa hizo kama shughuli za binadamu zitaruhusiwa kuongezeka ndani ya eneo la mbuga hiyo na kusababisha wanyama kutoweka,`` alisema Dk. Kilahama alipotembelea ofisi za JET, mjini Dar es Salaam, hivi karibuni.

Lakini si Serengeti tu. Kama zitajengwa barabara kubwa za lami ndani ya maeneo ya mbuga na kisha kuwakaribisha wawekezaji wa kigeni kujenga hoteli za nyota tano ndani ya mbuga hizo, shughuli za binadamu ndani ya mbuga hizo zitaongezeka na wanyamapori watatoweka moja kwa moja.

Na kama wanyamapori watakimbilia kwingineko kukwepa shughuli za binadamu, ni mtalii gani atatembelea mbuga hizo zisizo na wanyama? Je hoteli hizo za nyota tano ndani ya mbuga hazitaishia kuwa ``white elephants``?

Mfano mwingine wa jinsi Serikali inavyoendekeza uwekezaji wa kigeni unaofukuza wanyama au viumbe hai vinavyovutia watalii nchini, ni huu unaohusu ujenzi wa kiwanda cha magadi katika Ziwa Natron lililopo mkoani Manyara karibu na mpaka wa Kenya.

Licha ya kwamba Ziwa Natron ni eneo la hifadhi ya Ramsar (Ramsar Site) kwa mujibu wa Mkataba wa Kimataifa wa Ramsar ambao Tanzania imeuridhia, Serikali imeingia makubaliano ya awali (MOU) na kampuni ya Tata Chemicals Limited ya India kujenga kiwanda cha magadi katika eneo la ziwa hilo.

Wadau mbalimbali wa mazingira, ndani na nje ya nchi, ikiwemo JET, inaupinga mradi huo si tu kwa sababu ni eneo la hifadhi la Ramsar, lakini pia kwa sababu ujenzi wa kiwanda hicho utawafukuza ndege aina ya Lesser Flamingo kuondoka katika eneo hilo. Asilimia 75 ya ndege hao waliosalia duniani wanapatikana Tanzania katika Ziwa Natron.

``Ujenzi wa kiwanda cha magadi karibu na Ziwa Natron utatibua mazingira ya ndege aina ya Lesser Flamingo na kuwasababisha waondoke.

Ziwa Natron ndilo eneo pekee lililosalia katika Afrika Mashariki ambako ndege hao hutaga mayai,`` anasema Naibu Mkurugenzi wa East African Wildlife Society (EAWLS), Hadley Becha.

``Lesser Flamingo wanatoweka kwa kasi duniani. Wamo katika orodha ya IUCN ya ndege wanaotoweka kwa kasi duniani. Ni ndege wanaohitaji mazingira tulivu mno kuweza kutaga mayai yao na kutotoa.

Tanzania imebahatika kwamba bado inao ndege hao; lakini ni dhahiri ujenzi wa kiwanda hicho utafanya waondoke,? anasema Becha.

Kwa mujibu wa andiko la mradi huo, kiwanda hicho kinatarajiwa kuzalisha tani 500,000 za magadi kwa mwaka.

Aidha wakati wa ujenzi kitakuwa na wafanyakazi 1,225 na kikianza uzalishaji kitakuwa na watumishi 152. Kitatumia megawati 11.5 za umeme na lita 106,000 za maji kwa saa na kutoa maji machafu lita 10,000 kwa saa.

``Kiwanda kitakuwa na wafanyakazi wengi na hivyo shughuli za binadamu zitaongezeka katika eneo la ziwa.

Kutakuwa na kelele za malori yakiingia na kuondoka yakiwa na shehena za malighafi au magadi.

Haya yote yatawafanya ndege hao kuondoka kabisa na kuhamia nchi nyingine,`` anasema Andrew Wairu wa African Conservation Centre (ACC), moja ya asasi za mazingira zinazoupinga mradi huo.

Si siri kwamba moja ya sababu za watalii kuja Afrika Mashariki, hususan, Tanzania ni kuwaona Lesser Flamingo. ``Hiyo maana yake ni kwamba ndege hao wakishatoweka, watalii nao watapungua kuja``, alisema Wairu.

Hilo ndilo pia limewafanya wanamazingira wa Kenya kujitosa katika kampeni ya kupinga kuanzishwa kwa kiwanda hicho cha magadi, kwani ndege hao wa Lake Natron ndiyo pia huvuka mpaka na kuingia Kenya ambako watalii pia huweza kuwaona.

Ingawa wakati wa kikao cha bajeti Waziri anayeshughulikia Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Deodatus Kamala, aliwaambia wanamazingira hao wa Kenya kwa kusema kwamba Lake Natron ni mali ya Tanzania; hivyo lazima kiwanda hicho kitajengwa, lakini Waziri alisahau kwamba ziwa hilo ni trans-boundary; yaani uwepo wake unahusu au unagusa nchi zaidi ya moja.

Ni dhahiri Dk. Kamala alisahau kwamba ingawa Ziwa Natron lipo Tanzania, lakini mto unaoingiza maji katika ziwa hilo unaanzia Kenya. Je Kenya nao ikiuzuia mto wake kutakuwa tena na Ziwa Natron?

Hivi sasa kampuni ya Tata Chemicals Limited tayari imeshatoa zabuni kwa kampuni ya Nor Consult Tz kufanya tathmini ya athari za muda mrefu za mazingira (Environmental Impact Assessment - EIA) ya mradi huo, lakini haitarajiwi ripoti yake kuwa kinyume na matarajio ya `mtoa kazi`; yaani Tata Chemicals Limited.

Katika hali hiyo, matumaini ya mwisho ya wanamazingira wa Tanzania na Kenya yamo katika EIA itakayofanywa na Baraza`la Taifa la Mazingira (NEMC).

Matarajio ni kwamba NEMC litafanya uchunguzi wake likizingatia hofu zilizotolewa na wadau wa Ziwa Natron katika kikao kilichohusu mradi huo, kilichofanyika Julai 12 mwaka huu, mjini Dar es Salaam.

Lakini hata kabla NEMC haijafanya utafiti wake na kutoa ripoti yake ya EIA, kilifanyika kikao kingine, Agosti 13 mwaka huu, mjini Mumbai, India kati ya viongozi wa Tata Chemicals Limited na Shirika la Kimataifa la Mazingira - IUCN (Asia) na kutolewa ripoti ya `kujikosha`.

Ripoti yao inasema kwamba kampuni hiyo itazingatia maoni ya wadau wa Ziwa Natron yaliyotolewa katika kikao cha Julai 12, lakini wanamazingira hawana uhakika na utekelezaji wake.

Yawezekana Serikali ya Tanzania katika kuukubali mradi huo ilisukumwa na hamu yake ya kuongeza ajira. Lakini nini faida ya kutengeneza ajira za muda mfupi kwa kuua maliasili ambayo ingedumu vizazi na vizazi?

Tata Chemicals Limited ilikuwa na viwanda viwili vya magadi nchini Kenya, lakini kimoja tayari kimeshafungwa baada ya maji kukauka (viwanda vya namna hiyo hutumia sana maji).

Kwa maana hiyo, ajira walizoahidiwa nazo zinakuwa za muda mfupi.

Wanamazingira wanaamini kwamba kama Tanzania ikiendekeza uwekezaji huu wa kigeni unaoua maliasili, kwa sababu tu ya `faida ndogo za muda mfupi`, hakuna tena kitakachobakia kitakachowavuta watalii kutoka sehemu mbalimbali duniani kuja nchini. Huwezi kula keki yako na ukaendelea kuwa nayo!

Hii ndiyo changamoto kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe, Waziri katika ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Profesa Mark Mwandosya na waziri wa Viwanda na Biashara, Basil Mramba.

SOURCE: Nipashe

Maoni Yangu
Kwa ninavyojua, eneo la Ziwa Natron linalindwa na mkataba wa Ramsar,ambao lengo lake ni kulinda maeneo oevu yote duniani, hivyo kuweka mradi eneo hili ni kukiuka mkataba huo.
Maelezo zaidi yanapatikana katika tovuti yao "www.ramsar.org"
 
IDIMI,

1. Nchi zote duniani zinaendelea kwa kutumia raslimali zao- sasa issue iwe tupunguzeje athari za mazingira? Manake ni shughuli chache sana anazifanya binadamu bila kuharibu mazingira?

2. Maoni- tumechelewa kuanza kuchimba- lobbists ndo wanarudisha nyuma maendeleo saa ingine! Muhimu tuangalia taifa tutapata faida kiasi gani ktk huu uwezaji- isiwe kama Bugwazi!

3. Watalii hao hao ndo wanasema tusijenge barabara kupitia Serengereti ili wao waweze kuja kuwaangalia wanyama!

Contribution of Tanzania ktk Mabadiliko ya Hali ya Hewa duniani bado ni 0.01%!
 
Sawasawa Mkuu,
Ila tuangalie, hayo madini tuliyochimba mpaka sasa yametufaidishaje? Haya magadi yatabadili nini ambacho tumeshindwa kupata toka katika migodi mingine? Madini mengine yametufikisha wapi mpaka sasa? Je mkataba huu na hawa jamaa hautakuwa kama ule wa Buzwagi? Shida iko hapo, nadhani tungepembua kwanza mikataba ya nyuma kabla ya kuukubali huu wa magadi kwanza.
 
Nimekuwa nikifuatilia sana mjadala wa ujenzi wa mradi huu na kuhudhuria kongamano lililoandaliwa na Mamlaka ya Mazingira yaliyofanyika pale Karimjee. Ukweli ni kwamba mradi huu ni rasilimali kubwa sana kwa nchi yetu kwani magadi yale yatakuwa chachu ya kuanzisha viwanda vingine kadhaa. Ikiwa Kenya wanacho kiwanda kama hicho tunachotaka kujenga iweje leo Tanzania tukitaka kujenga iwe issue kubwa na je hao ndege wamehama Kenya? Hizi ni njama za mabeberu za kudhoofisha juhudi za kujikwamua kiuchumi. Wale waliopata bahati ya kuhudhuria kwenye kongamano Karimjee tar 23.01.08 utaona kwamba wale 'wenyeji'wa eneo hilo ni dhahiri wamenunuliwa na wapinzani wa ujenzi wa kiwanda hicho. Wamelipiwa nauli na malazi ili kuja Dar kutoa maoni yao. Ielewweke kuwa wazalishaji duniani wa soda ash wana 'cartel' au umoja wao na ili bei ya soda isishuke wanapiga vita juhudi zozote za kufungua miradi mipya duniani kama wa Lake Natron. Tukijadili hili tuwe macho tusitekwe na hisia potofu. Ripoti ya mazingira na faida za kiuchumi hasa 'backward' na 'forward' linkages viangaliwe kwa umakini sana. Faida itakayopatikana kwa ujezi huo ni kubwa kuliko hiyo ya utalii inayozungumziwa. Let us be bold.
 
Are you serious?
 
IDIMI,

1. Nchi zote duniani zinaendelea kwa kutumia raslimali zao- sasa issue iwe tupunguzeje athari za mazingira? Manake ni shughuli chache sana anazifanya binadamu bila kuharibu mazingira?

2. Maoni- tumechelewa kuanza kuchimba- lobbists ndo wanarudisha nyuma maendeleo saa ingine! Muhimu tuangalia taifa tutapata faida kiasi gani ktk huu uwezaji- isiwe kama Bugwazi!

3. Watalii hao hao ndo wanasema tusijenge barabara kupitia Serengereti ili wao waweze kuja kuwaangalia wanyama!

Contribution of Tanzania ktk Mabadiliko ya Hali ya Hewa duniani bado ni 0.01%!

Ni mawazo potofu kuamini kuwa sababu kubwa ya kulinda hao Lesser Flamingoes ni kwa ajili ya watalii. Kwa spidi tunayoangamiza species zilizo asili kwetu sitashangaa kama wajukuu wetu hawataenda ulaya kujua Flamingo yukoje? Rasilimali hii ni kwa vizazi vyetu vinavyokuja.

Miaka ya nyuma muwekezaji maarufu aliyejulikana kama John Nolan alipendekeza kuanzisha prawn farming huko Rufiji. Wanasiasa kama kawaida yao wakaupigia debe sana mradi huu. Isingekuwa juhudi za hao mnaowasimanga sasa hivi Rufiji ingeisha kufa na Nolan angehamia kwingine. Hicho mnachotaka kuvuna ni finite na kitakwisha siku moja. kikiisha mtafanya nini? Mtaenda kuwaomba hao flamingo warudi?

Kaangalie madhara ya barabara huko Mikumi ndiyo utajua ni kitu gani kinachopingwa hapa. Tatizo letu ni kuwa hatuambiliki mpaka hapo tunapoharibu. Tukishaharibu ndiyo tunarudi na kuwalaamu kwa kutushauri vibaya.

Huu mradi ni bomu. Hiyo miradi ya huko Serengeti na yenyewe hivyo hivyo ni myopic. Itatutokea puani.
 
Nimekuwa nikifuatilia sana mjadala wa ujenzi wa mradi huu na kuhudhuria kongamano lililoandaliwa na Mamlaka ya Mazingira yaliyofanyika pale Karimjee. Ukweli ni kwamba mradi huu ni rasilimali kubwa sana kwa nchi yetu kwani magadi yale yatakuwa chachu ya kuanzisha viwanda vingine kadhaa. Ikiwa Kenya wanacho kiwanda kama hicho tunachotaka kujenga iweje leo Tanzania tukitaka kujenga iwe issue kubwa na je hao ndege wamehama Kenya? Hizi ni njama za mabeberu za kudhoofisha juhudi za kujikwamua kiuchumi. Wale waliopata bahati ya kuhudhuria kwenye kongamano Karimjee tar 23.01.08 utaona kwamba wale 'wenyeji'wa eneo hilo ni dhahiri wamenunuliwa na wapinzani wa ujenzi wa kiwanda hicho. Wamelipiwa nauli na malazi ili kuja Dar kutoa maoni yao. Ielewweke kuwa wazalishaji duniani wa soda ash wana 'cartel' au umoja wao na ili bei ya soda isishuke wanapiga vita juhudi zozote za kufungua miradi mipya duniani kama wa Lake Natron. Tukijadili hili tuwe macho tusitekwe na hisia potofu. Ripoti ya mazingira na faida za kiuchumi hasa 'backward' na 'forward' linkages viangaliwe kwa umakini sana. Faida itakayopatikana kwa ujezi huo ni kubwa kuliko hiyo ya utalii inayozungumziwa. Let us be bold.

Kuna swali halijajibiwa hapo juu.
Kwamba: Hayo madini ambayo tushachimba mpaka sasa (dhahabu, makaa ya mawe, almasi, Tanzanite, bati nk) yametusaidiaje kama nchi? Tumeondokana na umasikini kutokana na migodi hiyo? Je tunaamini magadi yatatuondoa kutoka katika masikiniyulio nao? Naomba majibu tafadhali, msikwepe hoja.
Soma hapa, uone kama mradi una faida ama la! "http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/1/29/makala7.php"
 
Ni mawazo potofu kuamini kuwa sababu kubwa ya kulinda hao Lesser Flamingoes ni kwa ajili ya watalii. Kwa spidi tunayoangamiza species zilizo asili kwetu sitashangaa kama wajukuu wetu hawataenda ulaya kujua Flamingo yukoje? Rasilimali hii ni kwa vizazi vyetu vinavyokuja.

Miaka ya nyuma muwekezaji maarufu aliyejulikana kama John Nolan alipendekeza kuanzisha prawn farming huko Rufiji. Wanasiasa kama kawaida yao wakaupigia debe sana mradi huu. Isingekuwa juhudi za hao mnaowasimanga sasa hivi Rufiji ingeisha kufa na Nolan angehamia kwingine. Hicho mnachotaka kuvuna ni finite na kitakwisha siku moja. kikiisha mtafanya nini? Mtaenda kuwaomba hao flamingo warudi?

Kaangalie madhara ya barabara huko Mikumi ndiyo utajua ni kitu gani kinachopingwa hapa. Tatizo letu ni kuwa hatuambiliki mpaka hapo tunapoharibu. Tukishaharibu ndiyo tunarudi na kuwalaamu kwa kutushauri vibaya.

Huu mradi ni bomu. Hiyo miradi ya huko Serengeti na yenyewe hivyo hivyo ni myopic. Itatutokea puani.

Fundi,
Nimeshindwa kupata pointi katika ujumbe wako huu! Umechanganya mambo mengi sana kiasi kwamba nashindwa kuelewa unapinga nini na kutetea nini. Be specific please!
 
Haya MzalendoHalisi, ID yako na unachosema ni totally opposite.
Anyway its all about perception.
I think the problem with us Tanzanians, is that we lack the knack of having long term plans, thats why we cant see all that we are going to destroy in short term plans.

Who needs a 5 star hotel there, the tourists come all the way here to experience rugged life, including rough off roads, tents, people the maasai and other local residents not stay in a "Sun city" lookalike hotel.

Please let us wake up and see what we are bound to destroy here. For the love of our future generation.

My heart breaks for the country that is slowly slipping away........
 
Let them tell us what we have benefited from all the mines and minerals that we have so far depleted maybe we might be convienced....
 
Fundi,
Nimeshindwa kupata pointi katika ujumbe wako huu! Umechanganya mambo mengi sana kiasi kwamba nashindwa kuelewa unapinga nini na kutetea nini. Be specific please!

In a nutshell. Naupinga huu mradi kwa nguvu zangu zote. Naamini tunachoangalia hapa ni short term gains bila kujali madhara yake ya muda mrefu. Uwezekano wa extinction wa lesser flamingoes upo sana maana hii ndiyo breeding ground yake iliyobaki. Wenzetu wana miradi ya kukusanya mbegu za wanyama wote duniani Kinachoweza kutokea ni wao kuchukua mayai ya hawa ndege na kuyakuza huko ulaya. Kwa sababu hawa ndege hawatakuwepo tena huku kwetu, vijukuu wetu itabidi waende ulaya kuwaona. Hii hali imeishaanza kutokea kwenye mimea yetu. Botanical gardens za ulaya zina aina nyingi ya miti kutoka kwetu ambayo huku kwetu imeishakuwa adimu. Mifano mingine ni vyura wa kihansi. Hatunao tena, wako ulaya. Mwingine ni vifaru. Ilibidi tuletewe vifaru kutoka Afrika Kusini kujazia kwenye mbuga ya sadani. Mimi ningependa wajukuu zangu waweze kuviona vyote hivi hapa kwao na si kusimuliwa tu kuwa tulikuwa navyo.

Mfano wa John Nolan ni kuonyesha vipi uroho mwingine ulikuwa almanusura uteketeze mikoko ya Rufiji. Ni juhudi za wanamazingira ambao kwa kutumia mifano kutoka Sri lanka na kwingine walihamasisha wananchi kupinga mradi huo kwa juhudi zote. Mashamba ya prawn yanaathiri sana mazingira kwa kukata mazalio asili na kuongeza sumu kwenye eneo. Ni kama ukulima wa kutumia mbolea chumvi. Mapato yanakuwa sana kwa muda mfupi lakini uwezo wa ardhi kujirutubuisha unapungua. Mkulima anakuwa tegemezi wa mbolea na madawa, ambapo awali hakuwa hivyo.

Kuhusu barabara Serengeti. Nimetoa mfano wa barabara iendayo Iringa kupitia Mikumi na jinsi wanyama pori wanavyouawa kila siku. Wote tunajijua tunavyoendesha.Pamoja na hayo, kila eco-system inauwezo wake. Kwa kuongeza watu katika eco-system nyeti kama ile ni kuua bata anayetaga mayai ya dhahabu. Huu mradi nao naupinga kwa nguvu zote.

Umenielewa sasa?
 
Ndugu Fundi,
Hapo tunaongea lugha moja, kumbe na wewe ni mfurukutwa wa rasilimali na mazingira kama mimi. Mie napinga sana suala la kuendekeza pesa na kusahau uhai, heshima na utu. Ni aibu sana eti kwenda kuchukua vifaru kule Kruger Afrika Kusini mwaka 2001, kisa? Eti sisi tumewinda mpaka wamekwisha! Shame on us! Sasa hawa Lesser Flamingo (korongo wadogo) wakiiisha Tanzania tuende kukopa Ujerumani katika 'zoo'?
What a shame!

[media]http://www.jamboforums.com/attachment.php?attachmentid=1060&stc=1&d=1201696636[/media]

[media]http://www.jamboforums.com/attachment.php?attachmentid=1061&stc=1&d=1201696636[/media]
 
Attachments

  • Korongo.jpg
    Korongo.jpg
    63.6 KB · Views: 94
  • Korongo1.jpg
    Korongo1.jpg
    16.8 KB · Views: 87
Ni mawazo potofu kuamini kuwa sababu kubwa ya kulinda hao Lesser Flamingoes ni kwa ajili ya watalii. Kwa spidi tunayoangamiza species zilizo asili kwetu sitashangaa kama wajukuu wetu hawataenda ulaya kujua Flamingo yukoje? Rasilimali hii ni kwa vizazi vyetu vinavyokuja.

Miaka ya nyuma muwekezaji maarufu aliyejulikana kama John Nolan alipendekeza kuanzisha prawn farming huko Rufiji. Wanasiasa kama kawaida yao wakaupigia debe sana mradi huu. Isingekuwa juhudi za hao mnaowasimanga sasa hivi Rufiji ingeisha kufa na Nolan angehamia kwingine. Hicho mnachotaka kuvuna ni finite na kitakwisha siku moja. kikiisha mtafanya nini? Mtaenda kuwaomba hao flamingo warudi?

Kaangalie madhara ya barabara huko Mikumi ndiyo utajua ni kitu gani kinachopingwa hapa. Tatizo letu ni kuwa hatuambiliki mpaka hapo tunapoharibu. Tukishaharibu ndiyo tunarudi na kuwalaamu kwa kutushauri vibaya.

Huu mradi ni bomu. Hiyo miradi ya huko Serengeti na yenyewe hivyo hivyo ni myopic. Itatutokea puani.

Fundi,

"We meet the needs of present generation without jeopardizing the needs of Future Generations'- Our Common Futute- Bruthland Commission, 1990.

Kwa kifupi..hatuwezi kukaa tu tukakalia madini, mafuta, land nk kwa kuhofia tu athari za wanyama! Tunapozalisha kwa manufaa ya sasa pia tuangalie future- haimanishi basi tulale na tuongope eti tutayaharibu mazingira! Saudia na Iran leo wasichimbe mafuta kwa kuwa yataisha?

The largest contributor to effects of CFCs ni US which contributes 25%, Tz tunacontibute .01%. Je US waache kuzalisha lei in the name of environmental protection? No- wazalishe but wawe sensitive to environmetal concerns!

Hata magadi ya Natron yachimbwe tu- ila tuwe conssious na hao Flamingo! Sasa rate ya dereforastaion Tz inasemekana for the last 50 years over 50% of natural forests zimetumika ktk human activities -je watu leo kule kijijini tuseme wasikate miti kupata kuni kupikia? Je wapikie nini? Alternative sources za energy kupikia ndo hupunguza kuni dependence!

Nachotaka kusema ni kuwa, lobbists, western advocates have brainwashed our critical thinking- wakati watu wetu wanakufa kwa njaa na umaskini- wao wanasema wanyamamuhimu zaidi- how many poor African die? Yet leo akifa Ndege mmoja kule Natron utaona ktk TV BBC na CNN!

Well nimeangalia Magadi Natrion ktk larger picture!

Wacha EIA zinafanyike na kutoa ushauri wa Magadi project- my concern ni kuwa je Tz watabenefit vipi na huu mradi? This is another question!
 
1.Kabla hatujaenda mbali na mradi huu, kunakuwa na tathmini ya athari za kimazingira inayofanywa na mamlaka husika. Kazi hii ni ya kitaalamu na hutoa majibu yanayotuwezesha kufanya miradi tukijua matokeo yake ni nini. Tathmini hii inasemaje?

2. Kenya wana mradi wa namna hii kwa upande wao, lakini ziwa Natron hilo hilo. Wamewezaje bila kuathiri mazingira?

3. Kuna msukumo mkubwa wa kuzuia mradi huu juu ya athari za mazingira toka kwenye taasisi za Kenya. Je, ni hatua za dhati kulaani ujenzi huu na si mbinu za kibiashara?
 
..issue iwe mradi huu utatunufaisha vipi na tutazuia vipi uchafuzi au uharibifu wa mazingira.

..nyingine ni siasa tu! ndio,baadhi ya wanaojiita wanamazingira ni wanasiasa "wakubwa" tusipotezane malengo,tuwe wakweli!
 
Mkuu,
Hii ripoti ipo maktaba ya taifa, ila sijaiona. Ukiachilia hilo, Tanzania ilisaini mkataba wa Ramsar wa kulinda ardhi oevu, ikiwemo eneo la Ziwa Natron ambapo ndio tuna mpango wa kuchimba magadi. Hii ripoti (EIA) imefanywa na hao wawekezaji, huenda inaegemea upande wao, sitashangaa. Kama una nafasi ipitie.
 
..issue iwe mradi huu utatunufaisha vipi na tutazuia vipi uchafuzi au uharibifu wa mazingira.

..nyingine ni siasa tu! ndio,baadhi ya wanaojiita wanamazingira ni wanasiasa "wakubwa" tusipotezane malengo,tuwe wakweli!

Ukweli gani unaoutaka? Wewe ulie mkweli, si utatajie hao wanamazingira wanasiasa wakubwa wenye hidden agenda?Ukielezwa unakimbilia kusema hizi zote ni longolongo mpaka hapo maji yatakapowafika shingoni.

Wamarekani wana mafuta kibao Alaska. Mpaka leo wanagombana kuhusu namna ya kuyavuna. Kinachogota ni swali kuwa kweli waharibu mazingira huko Alaska kwa ajili ya mafuta? George W na wenzake pamoja na wingi wao wameshindwa ku'convince' senate kwamba hii ni price ambayo taifa inastahili kulipa. Na huko hakuna watu. Ni misitu na wanyama.

Kuna wazo kuwa kwa vile sisi tunachangia kidogo katika uharibifu wa mazingira basi na sisi tuachiwe tuchafue hadi hapo tutakapofikia stage ya wenzetu. Projections zote kuhusu athari za global warming ni kuwa watakaoathirika zaidi ni wale waishio kwenye tropics. Pataongezeka ukame na El Ninos. Nchi za magharibi hazitaathirika sana na pengine zitafaidika kwa vile watakuwa na muda mrefu wa kuotesha mazao. Sasa hivi wenzetu wameishaanza kupanga mikakati ya namna ya kushughulikia wakimbizi watakaotoka katika nchi zitakazoathirika zaidi na global warming. Tanzania tupo kwenye mkondo huo.

Hawa ndege wanaozungumziwa wanataga katika sehemu moja tu Afrika Mashariki na pengine duniani na ni hapo Lake Natron. Hatuwezi kuwachukua na kuwahamishia mahali kwingine wakati tunaendelea na mradi huu. Mazingira yanayowafanya waje L. Natron yakishaharibika hawatarudi tena. Sasa mataifa ambayo yanaweza kuingia gharama ya kutengeneza mazingira kama hayo artificially ni huko kwenye nchi za magharibi. Hawa wana uwezo wa kuwachukua baadhi ya ndege na kuwakuza huko. Mnaamini kuwa baadaye watatuhurumia baada ya mhindi kuondoka na kutuachia ziwa lililoishakufa? La, wajukuu zetu italazimika kwenda huko huko kuwaona. Lakini kama kawaida yetu, kwenye ulaji tunaoona wa bure, hatusikii wala hatuambiliki. Na ni wepesi wa kuvurumusha matusi. Ni sisi tuliomtukana Clare Short alipotuonya kuwa mradi wa rada ni bomu! Leo hii tunajifanya kulia machozi ya mamba na kunyosheana vidole vya ufisadi! Tumeishaonywa. Ni uamuzi wetu kama watu wazima kusikiliza au kukataa. Mungu atunusuru na hili tena.
 
Fundi,
Kwanza nikuponzeze kwa kutoa ufafanuzi murua katika suala hili la Ziwa Natron kwa mara nyingine. Tusijebaki kusaga meno miaka michache baadaye baada ya kuingia mikataba feki na kuharibi kabisa ikolojia ya eneo la Ziwa Natron na kusema "Tungejua"! ambayo Wahehe husema "Ngalinzeela"! Unajua ili kuweza kuwaelewesha hawa jamaa wasioona umuhimu wa suala hili, inabidi tuwaeleweshe kwanza mfumo ikolojia unavyofanya kazi. Kwamba, mimea na wanyama huwa tunategemeana. Wale korongo wadogo pale Manyara wanategemea lishe yao kutokana na mwani (algae), mimea ambayo hustawi vyema zaidi katika eneo lile. Na hawa korongo, kama unavyosema, kwa hapa Afrika Mashariki wanastawi na kuzaliana kwa wingi hapo Ziwa Natron. Sasa kama ukisema ukaushe ziwa lile kwa kuchimba magadi na kuwahamisha korongo utakuwa umeharibu kabisa mfumo ikolojia wa eneo lile, utaua mwani na korongo, kwani wanategemeana. Faida ya kuacha lile eneo kama lilivyo ni kubwa kuliko kuchimba magadi na kuharibu ziwa, ikizingatiwa kwamba magadi hayo hayatamsaidia kwa lolote Mtanzania wa kawaida, kwani pesa ya madini hatujui inakoelekea.
Mwenye sikio na asikie!
 
Fundi Mchundo na Wataalmu wenzako wa mazingira mmeishia wapi kujadili mradi huu wa wahindi? Sina uhakika kama hawa jamaa wamesitisha mradi huu, any updates please!
 
April 3, 2011

A soda ash mining plant planned for Tanzania's Lake Natron, the breeding ground for all of east Africa's endangered lesser flamingoes, must go ahead, President Jakaya Kikwete said Saturday.

"There is no need for further delay of the project, which will give the country's economy a big boost," Kikwete said.

Kikwete, who was addressing officials at the trade and industry ministry, said Lake Natron's reserves of soda ash deposits were big enough to make Tanzania the world's leading producer of the product.

The plant, which will be able to process up to 500,000 tonnes of soda ash annually, has attracted criticism from environmentalists who argue the project and its associated infrastructure will destroy the flamingoes' breeding ground.

Like all flamingoes the birds lay a single egg on a mound of mud.

Kikwete argued, however, that destruction of the breeding grounds could be avoided.

"We cannot continue with poverty while we have vast resources, including our minerals that are lying untapped. We can just apply the right technology that is not harmful to flamingoes," he said.

Industry minister Cyril Chami has said that the relevant environment and social impact assessments should be completed by the end of April.

The plant, which is to be built and operated by Tata Chemicals of Mumbai, and which will feature a grid of pipes running across the lake as well as infrastructure for workers on the shore, was put on hold in 2008 on environmental concerns.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom