Tujadili miaka mitano ya tumbuatumbua na matumizi mabaya ya mali za umma

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
May 18, 2019
762
6,980
Tunaingia miaka mingine mitano ya awamu ya tano na tumeanzia pale tulipoishia. Tumbua tumbua inaendelea......kwanini wateule niwagumu kumwelewa anayewateua?

Kama ubadhirifu huu unaotajwa kila siku ni kweli Basi Tanzania tunaongozwa kwa kuwa na mfumo mbaya wa uteuzi wa viongozi. Tunateua watu wasio na sifa na uwezo wakusimamia taasisi tunazowapa. Tunateua watu wasiojua awamu ya tano inataka nn. Tunateua watu kwa usiri bila kutaka public opinion.

A simple vetting inaanzia kwa watu waliofanya kazi na mtu anayetegemewa kuteuliwa, wakubwa zake kikazi na waliopo chinu yake wanaweza kukueleza anafaa au la.

Tunapata hasara kubwa sana kupitia uchunguzi, ili Ni eneo ambalo wapo watu naamini kila safari au kazi ya uchunguzi majina yao yapo. Si kwamba wanajua sana ila wameshajitengenezea sehemu ya ulaji. Wao wanaishi kwa kufuatilia maisha ya wenzao, Wana safari nyingi mikoani kujustfy uhalifu na wizi wa Mali za umma.

Hiyo ni njia moja yakupotezea serikali mapato. Njia nyingine ni kuwa na watumishi waandamizi nchini wasiofanya kazi zao lakini WANALIPWA mishahara ya vyeo vyao baada ya kutumbuliwa na kubainika Awana makosa.

Njia nyingine ya upotevu wa mapato ni uhamisho unaoambatana na kuingia ofisini kwa safu mpya ya uongozi. Kila kiongozi kwenye utumishi wa Umma anachagua afanye na nani kazi hivyo kusababisha uhamisho usio na tija.

Njia ya mwisho nikuondoa imani ya taasisi nakuwafanya watu kuamua kutokushirikiana na taasisi za umma kwenye kazi. Mtu anaamua kumkwepa TRA kwa sababu anaamini ujio wao kwenye eneo lao la kazi Ni kudai rushwa, same to police na mamlaka nyingine.

Suluhisho ni kubadili mfumo wa vetting, tusiangalie usafi wa majalada kwani wakati mwingine watu wachafu utumia fedha zao kujisafisha. Tusijikite kwenye elimu pekee kwani wasomi wengi siyo watendaji.

Tuunde kitengo chakufuatilia utendaji kazi wa watu wanaofaa kupendekezwa kushika ofisi. Wapo junior officers wamefanya mabadiliko makubwa ya taasisi hasa private sector kuliko senior officials. Wapo watoto kwenye taasisi wanafanya kazi hadi taasisi inatamani kuwavusha vyeo, si watu wote wamezaliwa kusota, wengine upeo wao unawafanya wakue kiubongo nakutumia akili zao kufanya mabadiliko. Tufuatilie Idara moja moja, tutagundua wapo watu wana uwezo mkubwa na wanafaa kupewa ofisi.

Mhe. akiteua basi aliyeteuliwa taasisi anayofanyia kazi wakiri kwamba anafaa. Watu wanateuliwa taasisi nzima inaguna, Hawa ndio wanaodhalilisha posts kubwa serikalini. Tumbua tumbua inakera

Tafteni watu wenye uwezo wakutoa huduma mtapunguza tumbuatumbua.
 
Nakubaliana na mtoa hoja.. ningekua na mamlaka, uzi huu ungepita moja kwa moja kwa DG-TISS kwenye kitengo chake cha GSO, Ofisi ya Rais Utumishi wa Umma pamoja na kwa Katibu Mkuu kiongozi Eng Kijazi.

Nakubaliana na mtoa mada kuwa muundo wa vyeo vya utumishi wa umma hauna reward mechanism kwa wanaofanya kazi vizuri. Junior officers wengi sana wamekua na "full scale impact" hadi Wakuu wa Utawala wanatamani kuwavusha madaraja. Lakini kigugumizi kinarudi kwenye neno lao pendwa wanaita "vyeo vya muundo" ambacho kinataka mtu kupanda daraja kwa kuhudumu kati ya miaka 5-10!

Hata kama sio kupanda madaraja, vyeo vya maofisa serikalini haviangaliwi hasa hasa kwenye teuzi. Watu wanateuliwa wasioijua ofisi, wanatumia muda mwingi sana kujifunza kazi. Unakuta DG wa taasisi fulani anategemea kwa kiasi kikubwa ushauri wa kifaalamu kutoka kwa junior officer.. kimantiki junior officer angepaswa hata kuwa ofisa mwandamizi, pasingekua na "rigidity" katika upandaji wa madaraja.

Kwa muktadha huu, tumbua tumbua ya Magufuli na serikali yake haitaleta suluhisho lolote zaidi ya kuiongezea sana serikali mzigo na gharama.. zipo ofisi ni highly technical, hivyo teuzi zinapaswa kuzingatia technical capability plus institutional memories..

Itoshe tu kusema kuna madhaifu katika ofisi ya Rais, kitengo cha Utumishi wa Umma.

Nawasilisha.
 
Hapa tatizo ni jiwe mwenyewe.
Elimu yake ya kuungaunga. Uelewa wa mambo ni kiduchu sana , hivyo anaendeshwa na mihemko.

Anateua watu kwa misingi ya ukanda, ulamba viatu na ukabila. Sasa unategemea ufanisi ktk serikali hii???
 
Back
Top Bottom