Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 5
Jamani naona umuhimu mkubwa sana wa kuadili pamoja ishu ya mgomo wa waalimu unaoandaliwa.
Chama cha walimu Tanzania (CWT) kimeshaanza maandalizi ya mgomo kwa kusambaza fomu kwa walimu kusudi walimu wajaze kama ishara ya kuunga mkono mgomo huo.
Wakati mkakati huo ukiwa mbioni kutekelezwa imeibuka hoja ya ni lini mgomo huo uanze.Wapo wanaopendekeza kuwa mgomo huo uanze ama siku ya mitihani ya darasa la saba au siku ya kuanza mitihani ya kumaliza kidato cha nne mwaka huu.
Hata hivyo kuna walimu huko Shinyanga wameanza kugwaya hasa wale waajiriwa wapya kwa madai kuwa bado hawaja onja utamu wa kazi.
Napenda kuweka hoja nzito zifuatazo:
Serikali inalichukuliaje suala la malimbikizo ya madeni ya waalimu?
Serilkali itaendelea kuwahadaa walimu na wafanyakazi wengine mpaka lini?
Hivi ni kweli kuwa serikali inatafuta fedha wakati kuna wengine wanazichota hukohuko serikalini na kujineemesha?
Serikali imeshajiuliza nini zitakuwa athari za mgomo wa walimu kitaifa?
Ni nini hatima ya elimu yetu na watoto wa Tanzania katika Jumuiya yaAfriaka Mashariki,SADEC,AU na dunia kijiji kwa ujumla?
Kama walimu watagoma je sisi wenye watoto mashuleni natuliopitia mikononi mwa haohao walimu tufanyeje?Tukae kimya? Tuandamane?
Mimi ni mdau wa ELIMU tena hasa.Najua madhila wayapatayo waalimu.Sijahadithiwa na mtu.Mimi ni Mtanzania, Nafahamu ahadi hewa ambazo serikali yetu imekuwa ikizitoa.Mimi nami ni MUATHIRIKA wa serikali iliyopo na zilizopita kwa kiasi.
Tusipoitazama ELIMU kwa umakini tunapoteza mwelekeo wa Taifa.Wanasiasa wetu wameingiza siasa kwenye masuala nyeti na mtambuka.Imekuwa rahisi sana kusimama Bungeni na kusema 'Serikali imeliona hilo na inalifanyia kazi pindi fedha zitakapopatikana'.Hata Rais katika hotuba ya mwisho wa mwezi alituambia kuwa'Uvumilivu ni sehemu ya kutatua tatizo'.Alimaanisha kuwa kama umekalia makaa ya moto uvumilie tu wakati utaratibu wa kuondoa huo mkaa unafanywa.Alikuwa anatuma salamu kwa walimu na vikongwe wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika Mashariki kuwa hata wakiandamana na kulia siyo rahisi mambo yao yakatatuliwa mapema, wajifunze kuvumilia shida.
Hivi huko serikalini wanajua shida kweli?.Sijawahi kusikia wafanyakazi wa ofisi ya Bunge, wabunge,wafanyakazi wa Ikulu au Mahakama wanalalamika kucheleweshewa malimbikizo yao.Huko kwa wakubwa mshahara unaongezwa na wanalipwa kwa wakati bila kulimbiiza.Waalimu wanadai malimbikizo ya miezi 6 mpaka miaka miwili.Nchi moja, Raisi mmoja, chama dola kimoja.
Sitaki kuamini kuwa watanzania tumekubali kuwa wadanganyika kwa kiasi hiki lakini nataka kuamini kuwa tunaelekea kufumbuka macho na kuuona ukweli wa uongo wa wanasiasa wetu na watendaji tuliowapa dhamana.
Sipendi niendelee kuamini kuwa tumelishwa unga wa NDERE kama Mtolewa kwenye tamthiliya ya KIVULI KINAISHI.Kama kweli tumelishwa unga wa ndere tutaendelea kuamini kuwa uvumilivu wetu wa milele ni sehemu ya kutatua matatizo.
Mwaka 2010 tutaletewa Ilani ya uchaguzi mpya na somo la uvumilivu litaendelea...
Karibuni wadau.