Tujadili Mfumo wa Elimu utakaotufaa Tanzania. Maoni yataunganishwa na kufikishwa Bungeni na Serikalini

Mimi kwa mawazo yangu,
Kwanza masomo yapunguzwe. Tukianza na elimu ya msingi, wasome masomo matano tu. kwa mchanganuo ufuatao:-
1. LUGHA [Kiswahili na kiingereza]
2.MAARIFA YA JAMII [Urai, Historia, na elimu ya mazingira na kujitambua]
3.STADI ZA KAZI [Kilimo, uvuvi, ufugaji na ufundi]
4.Sayansi [Jiografia,baiolojia,kemia na fizikia + kompyuta kozi(introduction)]
5. HESABU/HISABATI na BIASHARA
Kwa sekondari nako masomo yapunguzwe.
Wakimaliza shule ya msingi, wanapopangiwa kwenda sekondari basi wa speshelaizi na kombinesheni zao kabisa, yaani ukitoka shule ya msingi unapangiwa kwenda arts, science au business.
Masomo yawe kwa mchanganuo ufuatao:-
1.ARTS [LANGUAGE( kiswahili na kiingereza/kifaransa/kiarabu), + CIVICS and HISTORY + BASIC MATHEMATICS]
2. SCIENCE[PCM,PCB,PGM, CBG n.k + PURE MATHEMATICS]
3. BUSINESS[ECONOMIC, COMMERCE and ACCOUNTANCE + BASIC MATHEMATICS]
4. COMPUTER COURSE iwe kwa wote arts, science na business
-Kingine miaka ya kusoma nayo pia upunguzwe.
Kwa shule za msingi wanafunzi waanze shule wakiwa na miaka 7 baada ya kumaliza elimu ya awali ambayo kwasasa nayo pia iwe ya lazima.
-Shule ya msingi wasome miaka mitano ya darasani na mwaka mmoja wa stadi za kazi wakisubiri kuingia sekondari.
-Kwa sekondari wa wasome miaka minne ya darasani na mwaka mmoja wa stadi za kazi wakisubiri kuingia chuo.
-Baada ya hapo, chuo wasome miaka miwili/mitatu darasani mwaka mmoja kazi kwa vitendo.
Hayo ndo mawazo yangu.
Mkuu haya yote yanawezekana tatizo ni utekelezaji yaani kuanzia ngazi ya chini Hadi ya juu

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Ww jiulize tu toka 2005 serikali yetu bdo inaangaika na ujenzi wa madarasa tulianza kwa kujenga wenyew japo tunatoa kodi mpaka sasa tunajenga kwa ela za covid bdo atujaanza kuwekeza kwenye vyuo vya ualimu wala kwenye kuajili
Pia Maabara zilijengwa kwa michango ya wananchi wanyonge

matokeo yake hizo Laboratory zimekaa kama magofu hazina walimu wenye uelewa wa Sayansi Wala vifaa
Yaani hii sisi watu weusi tungeacha kwanza Mzungu atutawale.

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu,Mfumo wetu wa elimu uwe hivi

Pre Primary 3 years(Hapa mkazo uwe kwenye Development ya Motor Skills,Personality,Behaviour,Communications etc)
Primary 4 years(Hapa Iwe ni development ya Writing,Arithmetics,Verbal(Language Skills)
Post Primary 2 years(Hapa iwe ni Mkazo ni kwenye Vocational Skills,Physical Education(Sports,Arts,Culture)
Secondary 2 years(Hapa Iwe ni Academic Skill kulingana na Fani au uwezo wa Mtoto,Arts studies,STEM,Business,)
Pre College 2 years(Hapa Mkazi uwe kwenye Pre SPecialist Courses
College 3 Years(Hapa iwe ni Full Specialization.)


KAtika Stages zote tunaweza amua maeneo ya kuwekea mkazo
Mimi nasema hivi!!

Kabla serikali haijaanza malekebisho kwenye mfumo wa Elimu, kwanza ianze kuandaa walimu wenye uzalendo na weledi ktk kufundisha nasiyo walimu wenye njaa na uchu wakwenda ATM ili hali wavivu wakufundisha na wenye visilani over.

Sent from my Nokia 1 using JamiiForums mobile app
 
Ntajikita zaidi kwenye mada zinazofundishwa kwenye masomo mbali mbaki:

Baadhi ya mada zimepitwa na wakati kwa mfano kwenye somo la historia sekondari kuna umuhimu gani wa kupoteza muda kusoma evolution of man,eti tumetokana na masokwe,kweli dunia ya sayansi na teknolojia bado tupo kwenye usokwe!

Kwenye masomo ya lugha,kisw na engl tujikite zaidi kwenye stadi nne za lugha ie speaking,listening,writing and reading

Na kwenye mtihani iwepo practical ya hizo stadi nne yani kama ni speaking mtoto ajue kuna maksi za kuongea ili tupime uwezo wake wa lugha.

Ni ajabu kukuta msomi wa chuo kikuu hajui kabisa kujieleza kwa lugha aliosoma kwa miaka zaidi ya kumi.tuwe serios basi

Kwenye stad ya writig tukazanie creative writing hiyo ipo form four,kwmba mtoto waweze kuandika liwaya,tamthilia,mashairi nk.angalieni kwenye issue ya vitabu vya kingeleza ie nnovels,play etc

Waandishi wengi sio watanzania chukua unanswered cries,three suitors,this time tomorrow etc sio wantanzania.

Je, utamaduni wetu utatambulishwa na nini kama sio kwenye fasihi yetu?
 
BTEC business technology education council.
BTECs are specialist work-work related qualifications.

Ni mfumo thabiti unaofaa katika kuleta mapinduzi ya mfumo wetu wa elimu
 
Naomba elimu ya kuingia bungeni iwe bachelor na Tena iwe ya mwisho upper second over,hatutaki vilaza wawe viongozi wetu.

Yaani unaongozwa na mtu hajasoma kisa anapiga mdomo.

Pia Kama mbunge lazima awe na pesa isiyopungua billion tano benki ndani ya 10yrs consecutively haijawahi kushuka yaani iyo ndio balansi zero kwake.

Pia uraisi uwe first class gpa na awe na salio lisilopungua a half trilioni
Mana suala la kuwapa madaraka masikini inafanya wakasaini miktaba kwa kuhongea vipesa kidogo huku wakiuza Taifa.

Yaani kiongozi anaingia uongozini hajawahi ishika 10M mkononi siku akipewa Mia mbili anakuja kutetea kuwa vinyesi na mikojo ndio chanzo Cha kifo.

Kwani ivyo havikuwepo miaka ya nyuma huko na ndio kulikuwepo na ng'ombe kama ng'ombe hata hao wadinka wa sudani wakasome ama wa amhara na wa omoro wa Ethiopian
 
Darasa I-III
Uraia, Kiswahili na Hisabati

IV-VII
Hisabati, Kiswahili, Historia na Ufundi stadi (LEVEL 1)

Form I-IV (LEVEL 2-3)

Hisabati, Kiswahili, Historia na Ufundi stadi
Form V-VI

Hisabati, Kiswahili, Historia na Ufundi stadi (LEVEL 4-6)
 
Nadhani hatuhitaji kujadili mfumo wa miaka, tunatoka kwenye7.6.3 twende 8.4.8 au... tunahitaji kujadili kipi n kipi kitolewe au kiongezwe kwenye mtaala wetu ili kuifanya elimu yetu iwe n tija zaidi.
 
Naomba elimu ya kuingia bungeni iwe bachelor na Tena iwe ya mwisho upper second over,hatutaki vilaza wawe viongozi wetu.

Yaani unaongozwa na mtu hajasoma kisa anapiga mdomo.

Pia Kama mbunge lazima awe na pesa isiyopungua billion tano benki ndani ya 10yrs consecutively haijawahi kushuka yaani iyo ndio balansi zero kwake.

Pia uraisi uwe first class gpa na awe na salio lisilopungua a half trilioni
Mana suala la kuwapa madaraka masikini inafanya wakasaini miktaba kwa kuhongea vipesa kidogo huku wakiuza Taifa.

Yaani kiongozi anaingia uongozini hajawahi ishika 10M mkononi siku akipewa Mia mbili anakuja kutetea kuwa vinyesi na mikojo ndio chanzo Cha kifo.

Kwani ivyo havikuwepo miaka ya nyuma huko na ndio kulikuwepo na ng'ombe kama ng'ombe hata hao wadinka wa sudani wakasome ama wa amhara na wa omoro wa Ethiopian
Elimu ipi unayoongelea kwa hao wabunge???

Hii hii tunayoongea humu humu inayohitaji reforms??

Upper second ya kukariri??

Au ipi unayongelea?
 
Daaah. Nilitegemea hii mada iwe na wachangiaji zaidi ya 500 within 3hrs
Shida ni hayo kupelekewa bungeni ambako kiukweli watz wengi Kwa sasa hatuna Imani nako!

Tunaona ni kijiwe Tu cha wapigaji! Wala Kodi za bure!

So point zangu nitazitunza!

Mawazo na maoni yakifanyiwa kazi, atashukuriwa Rais Kwanza, wala hawatakumbuka Bambushka nilisema wazo wanalolitumia!
 
Back
Top Bottom