Tujadili mbinu za kuutangaza mlima Kilimanjaro Duniani

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
1593051577941.jpeg

Mlima Kilimanjaro ni moja ya vivutio vikubwa vya watalii ambao wengi wanaamini kuwa uko Kenya.

Tunaweza kuutangaza mlima kwa njia mbalimbali ikiwemo;

Kuchapisha majalada yanayoelezea historia yake, kulipuka kwa volcano, faida za udongo wa volcano kwa wananchi wanaouzunguka mlima.

Khanga na vitenge vinavyoinyesha mlima uko Tanzania na kushona nguo za vitenge hivyo kuwalenga watalii.

Vitambaa vya mapazia ikiwezekana mapazia ya hoteli.

Kalamu, notebooks, key holders, t-shirts nk.
 
Wasanii wetu pia wakatolee video zao kwa mlima hapo, zinapotazamwa huko duniani watazame na mlima wetu, wao wanapishana kuimba nyimbo za kumsifu mtukufu ili wapate dili la kampeni.
 
Jambo jema sana kuitangaza mlima Kilimanjaro.Kenya wanautangaza sana kama mlima wao,kuna Tshirt nililetewa zawadi toka kenya ikiwa na picha ya mlima kilimanjaro na kwa chini ikiwa imeandikwa kenya.
Sisi wenye mlima tunakwama wapi?
 
Wasanii wetu pia wakatolee video zao kwa mlima hapo, zinapotazamwa huko duniani watazame na mlima wetu, wao wanapishana kuimba nyimbo za kumsifu mtukufu ili wapate dili la kampeni.
Hapo pa kufanya video inabidi anayeenda awe ngangari, kumbuka kampeni ya Kigwangala ni wachache walifika tena kwa tabu ungewaona ungewaonea huruma.
 
Ni wazo zuri. Mwaka jana au juzi waziri mwenye zamana yake alipanda huo mlima na wasanii kadhaa, sijui ilikuwa na faida gani, sikuona hata wakipanda mti au maua.

Naweza sema huo mlima kama siyo the late R.Mengi aliyejitahidi kupanda miti yeye akitaka benefits kwa kupata maji yake ya chemchemi japo akivaa mwavuli wa kuulinda mlima pengine theluji yote ingekuwa imeondoka.

Unataka tufanye kitu ambacho kinaweza kuwa kigumu kutokana na direct benefits kwa mhusika.

Okay ngoja tuone,
 
Charity start at home.

Watanzania wote sio wachaga tu, wajenge utamaduni wa kutembelea na kufanya utalii wa ndani kila mwaka Kilimanjaro.
 
Back
Top Bottom