Tujadili masuala ya msingi tuache kujadili watu na walichosema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili masuala ya msingi tuache kujadili watu na walichosema

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tata, May 30, 2012.

 1. T

  Tata JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,741
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Ndugu so called "great thinkers"

  Nimekuwa nikifuatilia mijadala ya Jukwaa hili la siasa na nimegundua kuwa "threads" zinazozungumzia maneno wanayosema watu na matukio yanayotokea zinachangamkiwa sasa kwa watu wengi kujitokeza kuzijadili. Mara nyingi unakuta ni maneno tu yamewekwa bila hata uthibitisho.

  Inapotokea "thread" inayojadili masuala ya kimsingi ya nchi au michakato ya kisiasa hupati watu wengi wakichangia na mara nyingine "threads" za aina hii huwekwa pembezoni kabisa.

  Swali: Je inawezekana watu wengi humu ni "simple minded" wanaojifanya kuwa ni Great thinkers?
   
 2. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  I wish to board this kind of bus... lakini wapi halipo mkuu.
   
 3. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  sijaelewa ni mambo gani unayotaka tujadili na ni kauli zipi hutaki tuzijadili?
   
 4. O

  Omulangi JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 1,026
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Walimu wangu wote mbona walisema mtu yeyote msomi lazima atoe reference ya kila anachosema kimetokea wapi? Huwezi kusema maneno yako mwenyewe halafu ukasema umefanya analysis. Lazima uchambue misimamo mbal mbali na sababu zake na kisha ulete majumuisho. that is scholarly work.
   
 5. Wingu

  Wingu JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,326
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Unaweza ukawepo ukweli fulani kwa kile unachokisema lakini huwezi kuzungumzia mathalani siasa bila kuwa gusa moja kwa moja wanasiasa wenyewe.Hapo utakuwa umefanya kosa kubwa sana.Maendeleo ya Chadema kama chama cha siasa lazima uwaweke pamoja na viongozi wake ambao ndo hao binadamu tunaowazungumzia hapa
   
 6. N

  Njoka Ereguu JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 822
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 35
  Mkuu umenena, inapotokea topic kuhusu watu au events like fulani kafanya hivi kwa kweli tumekuwa wepesi sana kuchangia. Kinyume chake mvuto ni mdogo sana katika kuchangia mada za jumla zinazohitaji maoni na mawazo ya nini kifanyike ili tuvuke hapa tulipo. Unakuta tulio wengi tunapitia lakini wanaotoa maoni yako ni wachache mno ikilinganishwa na vile tunapochangia katika topic kama fulani kasimamishwa kazi, fulani amekatwa n.k
   
 7. N

  Nambombe Senior Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe unataka watu wangapi wachangie kila mjadala wa siasa na wachangie vipi,nadhani wewe ndio unashindwa
  kuchangia ipasavyo hiyo mijadala
   
Loading...