Tujadili: Mada maalumu ya kero,maoni na ushauri kwa TRA

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
42,722
49,418
Uzi huu ni mahsusi kwa kuibua vitendo vya kionezi vya TRA,malalamiko na ushauri au maoni ili kuboresha huduma kwa mteja
Je ni kweli TRA ni wabaya kihivyo au tunawasingizia hatutaki kulipa kodi so wanapotimiza wajibu wao tunawaona wabaya?
 
Sipotezi muda wangu. TRA waache wafanye kazi zao, siasa zinaharibu hizi taasisis ingawa nazo zinauchafu mwingi
Kumekuwa na malalamiko mengi sana kuwahusu TRA ,uzi huu ni maalumu kwa kubainisha vitendo hivyo na kushauri nini kifanyike
 
TRA sio tatizo, awamu hii inaoneka hii taasisi ni kero kuu kwa sababu tu kiongozi wa nchi ndio anafanya kazi TRA, yeye ndio anatoa maagzio ya kufanya wafanyayo..TRA IMEINGILIWA.
 
TRA wenyewe wanafuata sheria zilizowekwa na serekali zinazohusu kukusanya Kodi, chamsingi ni serekali kurekebisha sheria hizo ambazo ni kandamizi , TRA hawana kosa wanatumwa tu.
Ni kweli mkuu ila za kuambiwa changanya na zako
 
TRA sio tatizo, awamu hii inaoneka hii taasisi ni kero kuu kwa sababu tu kiongozi wa nchi ndio anafanya kazi TRA, yeye ndio anatoa maagzio ya kufanya wafanyayo..TRA IMEINGILIWA.
Ni kweli ila za kuambiwa changanya na zako,,ko wanapotumwa wajiongeze
 
Hukusikia walivyokuwa wanalalamikiwa? Wao walikuwa wanasingizia maagizo toka juu,mbona wa juu kawakana? Waliagizwa kubambikia watu kodi?
Ni kweli kabisa..kuna baadhi ya jamaa wa TRA wana mambo ya kipumbavu sana,. Mfano mtu unaenda kulipa kodi ambayo umepewa estimate alafu umbembeleze ofisa kukukatia risiti? Au u wabembeleza wakupe makadirio say ya mauziano ya kiwanja as if hawana haja na kodi yako...hawa jamaa baadhi yao wanakera...ila wapo wastaarabu pia.
 
Maafisa wengi wa TRA ni wezi na wahujumu uchumi wakubwa. Kodi ya mil 10, unawapa mil. 5, wanakupa risiti ya mil 3.
 
Mfumo wa ukusanyaji kodi uliowekwa ndio mbovu maana ndio unatoa mianya ya maofisa wa TRA kutaka rushwa. Kwani kiwango cha kodi kwa kila aina ya biashara kikiwa kinajulikana na hakibadilishwi si watu wangelipa tu? Unapompa ofisa wa TRA mamlaka ya kukadiria ndipo umempa njira nyeupeeee ya kudai rushwa ili akadirie kodi ndogo
 
Uzi huu ni mahsusi kwa kuibua vitendo vya kionezi vya TRA,malalamiko na ushauri au maoni ili kuboresha huduma kwa mteja
Je ni kweli TRA ni wabaya kihivyo au tunawasingizia hatutaki kulipa kodi so wanapotimiza wajibu wao tunawaona wabaya?
Mwaka 2014 niliuziwa gari lenye usajili bandia Toyota Regius... Ni wakati nafuatilia ROAD LICENSE by then ndio nikagundua tatizo
Gari lilikuwa na deni kama 980,000 nikalipa ila wakati wa kuchukua sticker ikashindikana Kwakuwa kwenye system ilionekana ni gari ya wizi
Nilafuatilia makao makuu na kugundua kuwa haikuwa ya wizi bali haikulipiwa ushuru wa kama million NNE hivi...
Nikiwa nimetoka TRA nikitafakari nianzeje kulipa deni ambalo sikulitegemea siku ya pili gari ikakamatwa kariakoo mtaa wa rufiji na madalali wa majembe
Sikuwa na wasiwasi kwakuwa tayari kesi yangu inajulikana na TRA, jamaa wakataka niwape M3 waniachie nikagoma
Tukaenda mpaka TRA, walichoongea wao na watu wa TRA wanajua wenyewe... Lakini ule ndio ukawa mwisho wa ile gari
Nikaongozwa kuipeleka yard... Ikafungiwa hapo nikaanza kufuatilia nikawapa kila walichohitaji lakini mwisho wa siku nikatakiwa kulipa million kumi
Ninapoandika sasa hivi muda huu inaozea yard pale....
Ilifika mahali nikakubali kulipa bila fine lakini figisu zikawa nyingi sana
 
Mfumo wa ukusanyaji kodi uliowekwa ndio mbovu maana ndio unatoa mianya ya maofisa wa TRA kutaka rushwa. Kwani kiwango cha kodi kwa kila aina ya biashara kikiwa kinajulikana na hakibadilishwi si watu wangelipa tu? Unapompa ofisa wa TRA mamlaka ya kukadiria ndipo umempa njira nyeupeeee ya kudai rushwa ili akadirie kodi ndogo
Well said...
Warekebishe sheria ya makadirio ya viwango vya kodi na ikiwezekana fixed rates ziwekwe kwa uwazi ili MTU azijue ..
Pia wajifunze kumlipisha raia kodi kubwa hakutowafanya wapate makusanyo makubwa Bali wanatengeneza walipa kodi sugu, pia wanakimbiza mapato coz iko wazi watz wanaenda nchi nyingine kama Uganda kununua bidhaa iliyopota bandari ya salama Tanganyika....
Bei ya bidhaa nchi zingine rahisi kuliko Tanganyika.. Who cares??
 
Mwaka 2014 niliuziwa gari lenye usajili bandia Toyota Regius... Ni wakati nafuatilia ROAD LICENSE by then ndio nikagundua tatizo
Gari lilikuwa na deni kama 980,000 nikalipa ila wakati wa kuchukua sticker ikashindikana Kwakuwa kwenye system ilionekana ni gari ya wizi
Nilafuatilia makao makuu na kugundua kuwa haikuwa ya wizi bali haikulipiwa ushuru wa kama million NNE hivi...
Nikiwa nimetoka TRA nikitafakari nianzeje kulipa deni ambalo sikulitegemea siku ya pili gari ikakamatwa kariakoo mtaa wa rufiji na madalali wa majembe
Sikuwa na wasiwasi kwakuwa tayari kesi yangu inajulikana na TRA, jamaa wakataka niwape M3 waniachie nikagoma
Tukaenda mpaka TRA, walichoongea wao na watu wa TRA wanajua wenyewe... Lakini ule ndio ukawa mwisho wa ile gari
Nikaongozwa kuipeleka yard... Ikafungiwa hapo nikaanza kufuatilia nikawapa kila walichohitaji lakini mwisho wa siku nikatakiwa kulipa million kumi
Ninapoandika sasa hivi muda huu inaozea yard pale....
Ilifika mahali nikakubali kulipa bila fine lakini figisu zikawa nyingi sana
Duu pole sana mkuu mambo kama haya ndio yanatakuwa kuyaibua na kupigiwa kelele
Kwa sasa sidhani kama itakuwa nzima ila ndio muda muafaka wa kuwafuata wakubwa wa sasa ili mkompromise vinginevyo itabidi ufidiwe kama yule mkongo.TRA ni kero na ni majangili kweli kweli
 
Back
Top Bottom