1000 digits
JF-Expert Member
- Oct 16, 2012
- 6,255
- 7,930
Analipwa kwa kodi za watanzania kama wafanyakazi wengine.Nijuavyo rais wa sasa lazima atapita ili amalize kipindi cha miaka kumi kama wenzie, hili swali lilipaswa kuulizwa uchaguzi wa mwaka 2025 ndio watu wajipange kumuweka mpendwa wao.
Mfanyakazi akiharibu anastaafishwa kwa manufaa ya umma.
Kumvumilia mfanyakazi anayevuruga kwa kumuonea huruma mpaka astaafu ni kuzidi kuvuruga kazi.
Miaka mitano akimaliza pia anastaafu na anapata marupurupu yake na atakua na bafasi ya kujaribu tena 2025/2030 n.k.
Tusiibinafsishe nchi kwa MTU mmoja na familia yake.
Hayo mambo ya kuwaaminisha wanasiasa kuwa watakaa muda mrefu madarakani ndio maana Viaongozi wa Afrika wanakua mafisadi wanaojilimbikizia Mali na marafiki zao mana wanajua hawatoki mpaka wastaafu au watumie ubabe kuzeekea madarakani.
Nchi zote za kiimla zina Watawala Mabilionea na matrilionea kupitia Mali na pesa za umma. Hawajali mana wakishakalia kiti wanajua hawaguswi mpaka wastaafu au wazeekee madarakani.
Tunawakabidhi kila kitu.
Ardhi yote ni Mali yao.
Fedha zote ni Mali yao.
Vyeo vyote ni Mali yao.
Sifa zote ni za kwao.
Heshima yote ni ya kwo.
Sheria zote zipo chini yao.
Roho na nafsi za watu wote ni zao.
Waafrika wengi wamelogwa.