mbongo_halisi
JF-Expert Member
- Apr 16, 2010
- 6,607
- 4,902
Nimeona thread nyingi zikimponda huyu na kumsifia yule kuhusu uchaguzi wa uraisi 2020..
nikapata wazo , kwanini tusijadili bila ushabiki wa vyama vyetu , kwa maslahi ya taifa letu kwanza kwani tukikosea kuchagua tunaumia wote ,
Ni Nani anayefaa kutuongoza Tena kwa miaka mongine mitano mbele uchaguzi wa 2020 na kwanini ? Nitatoa majina yanayojitokeza kugombea uraisi kwa vyama kadhaa Ila na wewe urataja wa kwako kama humu hawamo
CCM
1. John magufuli
2. Bernad membe
CHADEMA
1. Tundu Lissu
ACT
1. Zitto
2. Maalim Seif
CUF
1. Lipumba
Mitazamo wangu:
Mimi nàona JPM bado tunamhitaji Sana kwa miaka mingine mingi ijayo, kwakuwa pamoja na kwamba irani ya chama inasisitiza viwanda lakin kajitahidi kuboresha barabara, umeme , Huduma za kijamii, kuwajali wafanyabiashara , ufisadi umeisha, amefufua ndege , anatengeneza reli ya kisasa, maisha mazuri yanakuja tuwe wavumilivu , nk
Je , wewe una mtazamo gani ??
Kwa wanasiasa wa hapa Tanzania for the next 30 years anayefaa kuongoza nchi yetu ni Magufuli tu, hao wengine ni waganga njaa. Angalia maendeleo anayoleta Magufuli toka aingie madarakani na ujinga walioufanya marais vinyago waliopita katika utawala wao wa miaka 30. With Magufuli, tutafika mbali sana ila hao vinyago uliowataja hapo juu watarudisha kule kule kwa marais wasanii waliopita.