Uchaguzi 2020 Tujadili kwa manufaa ya Taifa: Uchaguzi 2020 twende na Nani na kwanini?

Huyuhuyu kiwete au?
Hujafa hujaumbika usitafute sifa kwa kukufuru kama mwanri,ajali zipo kila Siku nawe waweza jipatia yako anytime...Karma!!!
Kuna vigezo Vinci vya kiongozi bora,atatue shida za watu,awape matumaini na awaongoze kupigania maendeleo,awe mwerevu na mvumilivu,aendeleze na kuinua viongozi bora bila upendeleo,amche Mungu na azingatie mawazo ya wengi/ashaurike,asikimbie ikulu ya dar kisa mauzauza na kujenga nyengine Dom kwa gharama kubwa za kodi yetu...
#Membe ni Jembe...
 
Nijuavyo rais wa sasa lazima atapita ili amalize kipindi cha miaka kumi kama wenzie, hili swali lilipaswa kuulizwa uchaguzi wa mwaka 2025 ndio watu wajipange kumuweka mpendwa wao.
 
Nimeona thread nyingi zikimponda huyu na kumsifia yule kuhusu uchaguzi wa uraisi 2020..

nikapata wazo , kwanini tusijadili bila ushabiki wa vyama vyetu , kwa maslahi ya taifa letu kwanza kwani tukikosea kuchagua tunaumia wote ,

Ni Nani anayefaa kutuongoza Tena kwa miaka mongine mitano mbele uchaguzi wa 2020 na kwanini ? Nitatoa majina yanayojitokeza kugombea uraisi kwa vyama kadhaa Ila na wewe urataja wa kwako kama humu hawamo

CCM
1. John magufuli
2. Bernad membe

CHADEMA

1. Tundu Lissu

ACT
1. Zitto
2. Maalim Seif

CUF
1. Lipumba

Mitazamo wangu:

Mimi nàona JPM bado tunamhitaji Sana kwa miaka mingine mingi ijayo, kwakuwa pamoja na kwamba irani ya chama inasisitiza viwanda lakin kajitahidi kuboresha barabara, umeme , Huduma za kijamii, kuwajali wafanyabiashara , ufisadi umeisha, amefufua ndege , anatengeneza reli ya kisasa, maisha mazuri yanakuja tuwe wavumilivu , nk

Je , wewe una mtazamo gani ??
Twende na Jaji Mstaafu Augustino Ramadhan wa ccm 2020......
 
Nijuavyo rais wa sasa lazima atapita ili amalize kipindi cha miaka kumi kama wenzie, hili swali lilipaswa kuulizwa uchaguzi wa mwaka 2025 ndio watu wajipange kumuweka mpendwa wao.
Jipe moyo utashinda nilikuwa kanisani leo waumini wanaimba. .. Albashir aliwaza kama wewe
 
Huyuhuyu kiwete au?
HII KAULI IMENICHOMA MOYONI KABISA YAANI LISSU KAPIGWA RISASI NA NYIE WENYEWE LEO UNAMWITA KIWETE? HII KAULI NITAIFANYIA KAZI KWA KUSHAWISHI WATU AT LEAST 2000 WAMCHAGUE LISSU KAMA ATATANGAZA NIA, HUU NI UNYAMA WA HALI YA JUU KUMWITA KIWETE MTU MLIEPANGA NJAMA YA KUMPIGA RISASI,
ULIYETOA KAULI HII DHALILI MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU YENYE FURAHA TELE
 
Mkuu, huyo jamaa ni mwehu, mwenye akili timamu hawezi kushangilia jaribio la kumuua mtu asiye na hatia, hajaiba wala kumdhulumu yeyote.

Vv
 
Hujafa hujaumbika usitafute sifa kwa kukufuru kama mwanri,ajali zipo kila Siku nawe waweza jipatia yako anytime...Karma!!!
Kuna vigezo Vinci vya kiongozi bora,atatue shida za watu,awape matumaini na awaongoze kupigania maendeleo,awe mwerevu na mvumilivu,aendeleze na kuinua viongozi bora bila upendeleo,amche Mungu na azingatie mawazo ya wengi/ashaurike,asikimbie ikulu ya dar kisa mauzauza na kujenga nyengine Dom kwa gharama kubwa za kodi yetu...
#Membe ni Jembe...
Angalia ndugu yangu huijui kesho yako itakuwaje. Ulemavu unaweza kuupata muda wowote kwani hata huyo unayemwita kiwete hakuomba awe hivyo alivyo.

Tumuogope Mungu maana hatima ya maisha yetu hatuijui.
Hata Dr Didas Massaburi aliwahi kumtukana Lowassa kuhusu afya yake, leo hii kati ya Lowassa na Masaaburi nani kamtangulia mwezake?
HII KAULI IMENICHOMA MOYONI KABISA YAANI LISSU KAPIGWA RISASI NA NYIE WENYEWE LEO UNAMWITA KIWETE? HII KAULI NITAIFANYIA KAZI KWA KUSHAWISHI WATU AT LEAST 2000 WAMCHAGUE LISSU KAMA ATATANGAZA NIA, HUU NI UNYAMA WA HALI YA JUU KUMWITA KIWETE MTU MLIEPANGA NJAMA YA KUMPIGA RISASI,
ULIYETOA KAULI HII DHALILI MUNGU AKUPE MAISHA MAREFU YENYE FURAHA TELE
Amina. Mungu awabariki. Huyu jamaa kanisikitisha sana!
 
Twende na yeyote lakini asiwe:

1. Mjuaji kila kitu anajua yeye.
2. Rais na Waziri wa Wizara zote yeye mwenyewe.
3. Mbabe. Adumishe demokrasia akijua nchi ya vyama vingi hii.
4. Muuaji wa raia wanaotofautiana mawazo.
5. Mtu asiyeheshimu katiba ya nchi.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom