Tujadili: Kuna ukweli wo wote sisi ni vilaza EA yote? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili: Kuna ukweli wo wote sisi ni vilaza EA yote?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Wa Mjengoni, Jul 1, 2010.

 1. Wa Mjengoni

  Wa Mjengoni JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2010
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 482
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Wakuu hii nimeipata kwenye comments za Caroline, ktk gazeti la Mwananchi la leo 1julai 10,topic husika ''Ajira sasa wazi EAC'' nanukuu:
  "Watanzania wote shikeni kalamu muandike maneno haya."MFUPA ULIOMSHINDA FISI MB WA HAWEZI KUULA"
  Mwalimu Julius Nyerere aliziunganisha nchi za Afrika Mashariki miaka ile.Watanzania tukaishia kuinufaisha Kenya hadi leo wanazo ndege na wanaendesha shirika lao kwa nguvu za Watanzania.Hilo ndilo wanalolitafuta tena baada ya kuona tumelalia masikio.
  Nilipata kuyasema hata hata baada ya kukiona kipindi kinachoendeshwa na shirika la simu la ZEIN kinachoitwa ZEIN AFRIKA. Sijapata kuona hata siku moja chuo chochote cha Tanzania kikivuka hata hatua pa tatu ya mchujo kama walipata hiyo bahati ya kufika hatua ta pili.Elimu yetu Tanzania mpaka baada ya miaka kumi ijayo ndio tunaweza kuingia kwenye ushindani wa ajira na ujenzi wa viwanda.Mimi naionea huruma Tanzania na hasa familia yangu kuwa kile alichokikataa Mwalimu Hayati Julius Kambarage Nyereretunakiru dia tena na hata kabla ya kujiandaa.Mwisho napenda kila Mtanzania ajue kuwa "ASIYESIKIA LA MKUU HUVUNJIKA GUU"
  Hayo maneno mekundu tuyajadili kwa kutoa vielelezo, yameniuma sana.
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 180
  Tatizo kubwa la wanafunzi wa Kitanzania ni lugha siyo uwezo mdogo kiakili. Kutoijua lugha ya Kiingereza kunawapunguzia kujiamini (confidence). Na vile vile mchakato wa kufikiri (thought process) wao unakuwa ngumu/mrefu. Kwa Mtanzania ni lazima afikiri kwa Kiswahili kwanza halafu ajaribu kutafsiri katika Kiingereza. Hivyo hawezi kuwa na kasi ya kufikiri kama mtu ambaye amezoea kufikiri katika lugha ya mawasiliano inayotumiwa katika ZEIN AFRIKA CHALLENGE, yaani Kiingereza. Lakini tatizo lingine ni kwamba hata Kiswahili chenyewe hawakijui kwa ufasaha. Siku hizi huwezi kusikiliza vijana wakizungumza ukabaini yupi ni msomi na yupi ni mhuni tu wa mitaani. Zungumza yao na lafudhi ni ile ile. Wengi hawawezi kutamka kwa usahihi maneno yenye DH na TH. Utasikia msomi wa chuo kikuu anasema SAMANI wakati anamaanisha THAMANI. Mimi napendekeza tuombe waalimu wa Kiingreza kutoka Uingereza waje wafundishe katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu kwa muda wa miaka 10 hivi. Wahitimu wao ndio watasambaa katika shule na vyuo mbali mbali na kuboresha ufundishaji wa lugha ya Kiingreza. Waalimu wengi waliopo sasa hivi nao wana tatizo kubwa na Kiingereza. Baada ya hapo shule ziweke mazingira ya kuwalazimisha watoto kuongea Kiingereza. Kwa sababu sasa hivi hawana fursa au utashi wa kukiongea. Huwezi kuimudu lugha kama huizungumzi.
   
 3. Who Cares?

  Who Cares? JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2010
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 3,465
  Likes Received: 1,950
  Trophy Points: 280
  HAKUNA UKWELI WOWOTE KUWA SIE NI VILAZA KULIKO EA WOTE....mashindano kama zain challenge sio kipimo cha akili IQ ya mtu...kama vipi ipigwe sampling ya watanzania at random sampling then na wenzetu wapimwe ndio tupate jibu kuwa nchi gani inaongoza kwa vilaza...

  nachoamini mie ni kuwa WATANZANIA WANAONGOZA KWA AKILI KULIKO WOOTE EA NDIO MAANA TUMEKUWA NA BUSARA ZA KUWASIKIZA WENZETU NA KUWA VUMILIA KWA KERO NA UPUUZI WAO...tungekuwa ni wajinga tungeshawapiga na kuwatimu wapuuzi wengi tuu ambao wanaongea upumbavu juu ya nchi na wananchi wetu eti sie ni wavivu, sio agressive, hatuna akili coz we dont do english plus many more upuuzi...

  ILA kwakuwa tunaakili tunawaacha wapige mayowe ukweli watauona wenyewe...wanagombea 1 square kilomita ya ardhi hapo ziwa victoria .. huu kimsingi ndio ujinga na ukilaza..maana ukiongea kiingereza na kushinda mashindano ya zain unashindwaje kusolve issue ndogo kama ya kisiwa cha migingo....anyway ni maoni yangu tuu
   
Loading...