Tujadili Kuhusu Sheria ya Matumizi ya Fedha Kwa Ajili ya Uchaguzi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili Kuhusu Sheria ya Matumizi ya Fedha Kwa Ajili ya Uchaguzi!

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Buchanan, Jan 19, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jan 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  MUSWADA HUU WA SHERIA YA MATUMIZI YA FEDHA KWA AJILI YA UCHAGUZI UMEPINGWA NA NCCR-MAGEUZI KAMA ILIVYOELEZWA HAPA CHINI:
  ***************************************************************
  CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimepinga muswaada wa marekebisho ya sheria za uchaguzi na ule wa Sheria ya Fedha za Uchaguzi kutokana na mapungufu yaliyomo waliyosema yanavikandamiza vyama vya upinzani.

  Hayo yalisemwa jana Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa NCCR, Bw. Samuel Ruhuza kuwa endapo Bunge litapitisha muswaada huo chama chake kimejipanga kwenda mahakamani kuipinga na kuichongea serikali kwa wananchi kuhusiana na uozo wake.

  "Suala la kubadili na kutunga sheria zinazohusiana na uchaguzi ni suala nyeti sana kwa maendeleo ya nchi, nchi yetu imefika mahali ambapo mabadiliko ni lazima yafanyike ili tuweze kusonga mbele, lakini mabadiliko katika zama zetu yataletwa kwa njia ya sanduku la kura," alisema Bw. Ruhuza

  Bw. Ruhuza alisema kama miswaada hiyo ikipitishwa na kuwa sheria, haitaleta maendeleo bali itachangia kudidimiza demokrasia nchini na kuendelea kukipendelea chama tawala.

  Alisema marekebisho ya miswaada hiyo yaliyofanywa yana lengo la kuwahadaa Watanzania na jamii ya wahisani na pia ni mpango wa Rais wa Awamu ya Nne, Rais Jakaya Kikwete kujitafutia umaarufu kisiasa.

  "Pamoja na upungufu mkubwa uliopo katika miswada hii ni wazi kuwa serikali itatumia wingi wa wabunge wake bungeni ili kuipitisha, kama chama tawala kilitumia wingi wake kuruhusu takrima itumike katika uchaguzi hili litawezekana pia," alisema

  Alisema sheria hiyo pia inawabana wapinzani katika matumizi ya uchaguzi ambapo alidai kuwa ruzuku zinazotolewa na vyama vya siasa ni zaidi bilioni mbili, ambazo hutokana na kodi za wananchi.

  Kwa upande wa muswada wa Sheria ya Matumizi ya Uchaguzi alisema mapungufu yaliyopo katika kifungu cha 4(1)ambacho kinampa msajili mamlaka ya kusimamia na kuhakiki matumizi ya uchaguzi kwa vyama vya siasa.

  "Hiyo ni sheria ya kubana wapinzani katika uchaguzi, utajiri wako ndio utakaokupa ubunge na udiwani, kama wewe lofa ni bora uondoke,"

  Alisema katika kifungu cha 12(1) na (3) cha muswaada huu kinazuia mtu, asasi, shirika au kampuni kuingiza nchini fedha kutoka nje ndani ya siku 90 kabla ya Uchaguzi Mkuu au ndani ya siku 30 kabla ya uchaguzi mdogo.

  "Inasema fedha za kutoka nje zifike situ tisini kabla hata hujamjua mgombea wako, hiyo sio haki na ndio maana wao wameanza kuagiza magari mapema kwa kuwa walitambua wanachotaka kuanzisha," alisema.

  NCCR imependekeza kufuta vifungu vyote vinavyokandamiza vyama vya upinzani na kuipa Tume ya Uchaguzi mamlaka ya kuteua maafisa na wafanyakazi wake kama inavyoona inafaa, na siyo kuwateua maafisa wa serikali kama ilivyo sasa.

  SOURCE: http://www.majira.co.tz/index.php?option=com_content&view=article&id=2346:nccr-yalia-na-sheria-ya-fedha-za-uchaguzi&catid=34:kitaifa-tanzania&Itemid=57

  Je, madai ya NCCR-Mageuzi ni ya msingi, esp wanapozungumzia kuhusu kukandamizwa kwa vyama vya siasa vya upinzani (mambo ya siku 90 au 30)? Tujadili!
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jan 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Learned bros and sisters mnaniangusha, nategemea mngeshaanza kumwaga sera zenu muda mrefu!
   
 3. K

  Kibori Member

  #3
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Asante kwa kufuatilia mambo muhimu kama haya But please if possible provide us with the Bill for more details. It is a risk and unproductive to react to other's ideals tena ambazo zimetoka kwenye magazeti tu without the bill/law itself . Ndio maana ya Jukwaa la Sheria
   
 4. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #4
  Jan 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sijaipata. Ni kweli ingekuwa ni vizuri zaidi kujadili jambo la kisheria ikiwepo Sheria yenyewe. Lakini wahusika wa magazeti wame-cite vifungu husika vya Muswada. Unless kama hatuna imani na magazeti kiasi hicho basi tujadili yale waliyoyataja, kama working tool yetu wakati tunatafuta Muswada wenyewe. Juzi juzi kwenye jukwaa hili hili tumejadili mabadiliko ya the Law School Act, 2007 bila kuwa na Sheria ya mabadiliko hayo, lakini baadaye ikapatikana, tukaendelea na mjadala.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jan 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Mmmh, haka kaeneo naona hakajadiliki maana mpaka sasa hakuna mchango wowote toka kwa wadau wa JF. Labda kweli tusubiri Muswada wa Sheria uwekwe wazi kisha tuujadili kama alivyogusia mdau mmoja hapo juu!
   
 6. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145

  Mzee, katika hatua ya kupitisha Miswaada ya Sheria, kuna hitaji kuwa na "extensive public consultations" ikiwemo "PUBLIC HEARING" ambapo mara nyingi unakuta wanaoitwa kwenye hiyo mikutano ya wadau ni baadhi ya watu ambapo hawawezi kuleta vipingamizi vikubwa (Kwa baaddhi ya Wabunge, wengi wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuzibwa midomo na "bahasha za kaki")na imekuwa kama "deal" kwenye mikutano ya wadau watu kuulizia kwanza "bahasha" badala ya "makabrasha".

  Tatizo kubwa hapa ni kujadili kile ambayo twaweza kuona ni sawa kumbe sivyo au twaweza kuona sivyo, kumbe kipo sawa.

  Tunachopata nacho tabu ni kuwa siku za nyuma miswaada ya sheria iliweza kupatikana katika tovuti ya Bunge lakini sasa haiwekwi. Na la pili, tulitegemea Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwe na tovuti ya kuweka pamoja na masula mengine, Miswaada na Sheria kwa ajili ya kuwawezesha wadau kuzijua sheria na pengine kutoa maoni lakini hayo ni kitendawili kwa wanasheria wakuu wa awamu zote.

  Tatu, chama kama TLS pia kilipaswa kiwe "up todate" kuhabarisha jamii masuala yote muhimu ya kisheria zikiwemo kesi, mishwada ya sheria na majadiliano yanayoendelea nchini na ndunianai ilkibidi kuhusu sheria> Lakini, sina haja ya kusema kuhusu utendaji wa chama hicho tokea kianzishwe. ...


  Nne, Kitivo cha Sheria cha Chuo cha Umma kama UDSM siku za nyuma kilikuwa "active" sana kuweka mijadala ya kisherai wazi na kutoa elimu ya sheria kwa jamii mbali na misaada ya kisheria (Legal Aids) kwa kwa mfumo wa "pro bono".

  Sasa wahadhiri wa Kitivo hicho, ukiacha wachache tu walio "committed" kwenye kazi zao, wengi wao wamekuwa ni "academic mechants" or "Laptop Dr/Professors" so to say" na "google searchers" (not abusing them!), Wamekuwa wakihangaika huku na kule kwenye makongamano ya kitaifa, ki kanda na kimatafa kusakanya kazi za nje na ambazo zina maslahi binafsi zaidi kuliko umma wanao utumikia (siwalaumu kwa kufanya hivyo kutokana na mfumo wenyewe lakini hapo ndo tulipo na tunakoelekea ni kubaya zaidi).

  Kwa hawa Wahadhiri vijana wanaopata kazi hiyo sasa ni balaa zaidi kwani wao ni "dot.com" staili kama Muziki wa Kizazi kipya ( una hangaikia kuuza "single" ili upate hela chap chap umalize shida za leo pasipo kufikiria kesho itakuaje kwenye fani) na unakuwa taaluma haina radha, Wahadhiri wamekuwa ni wa "copy, paste and save changes" kwenye kazi za wenzao, lakini ikaja kwa mwanafunzi wanataka ukasomeee uje na "ideas" zako mwenyewe vinginevyo huwezi kumaliza chuo.

  Tano, hawa wanaojiita "TUME YA KUREKEBISHA SHERIA" tulidhani ingesimama baada ya kutapa kiongozi mwenye upeo, profesa na msomi wa sheria aliyekubuu kwenye "utafiti" na sasa ni Jaji wa Mahakama Kuu. Lakini hakuna hatua kubwa zilizopigwa katika kuweka mfumo mzuri wa kur atibu marekkebisho na utungwaji wa sheria zetu. Na sijui hata kama hii taasisi ina tovuti iliyo hai. Wao wamejikita zaidi kwenye nyanja ya elimu kwa umma kwenye "radio one"....wakihabarisha wananchi sheria ambazo pengine zimepitwa na wakati na hazikufanyiwa utafiti.na pengine unakuta mchambuzi anatoa mpaka mifano ya "kesi za mahakamani" ambazo zimeripotiwa kwenye vitabu vya sheria toka Mahakama za nje ya nchi na ambazo pengine sio sahihi au zinagongana na uhalisia..Sijui ni watanzania wangapi wanafuatilia vipindi vya sheria "Radio one"??.

  Sina uhakika kama hata "assessment" inafanyika kujua ni kiasi gani watanzania wameelimika na vipindi vya sheria vinavyotolewa na hii Tume, japo kwa kufanya hivyo pia ni kazi ya ulaji mwingine pia lakini ingesaidia kuliko kuongea kila wiki Redioni na kuhisia kuwa watu wanakusikiliza na kukuelewa kumbe inawezekana hakuna anayekusikiliza kabisa au wale wanaokusikiliza hawakuelewi chochote.....

  Bado safari ni ndefu sana!...
   
 7. B

  Bravo777 Member

  #7
  Jan 19, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muswada ulichapishwa in full katika magazeti machache sana nchini wiki ya Krismas (nadhani Daily News na Habari Leo peke yake - sijauona kwingine). Ulikuwa wakati wa pilikapilika za Xmas/New Year, bila shaka watu wengi wala hawakuushtukia. Nahisi serikali ilifanya hivyo makusudi katika jitihada zake za ku-push through hii sheria mpya bila feedback ya kutosha kutoka umma (public). Na tusipokuwa makini, jitihada hizo zitafanikiwa.
   
 8. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #8
  Jan 19, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kama uliupitia naomba utupatie abc zake ndugu, ukiacha zile za hapo juu!
   
 9. B

  Bravo777 Member

  #9
  Jan 20, 2010
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ilichapishwa kama tangazo ya kulipiwa katika hayo magazeti, hivyo si rahisi ku-download. Ila ninachoelewa mimi ni kwamba imo ndani ya latest government gazette (ya tarehe 11 December 2009) kama Bill Supplement No. 17. Pengine mnaweza kufuatilia hapo.
   
Loading...