Tujadili kuhusu pato la taifa yaani Gross Domestic Product (GDP) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili kuhusu pato la taifa yaani Gross Domestic Product (GDP)

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Raia Fulani, Jun 26, 2010.

 1. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  tunaambiwa kuwa GDP ni ile thamani ya pato la mwisho litokanalo na bidhaa au huduma fulani katika mwaka. pia ili kupata pato sahihi katika huduma na bidhaa zilizozalishwa, inachukuliwa thamani ya mwisho ya bidhaa husika ili kuepusha kuipa bidhaa thamani mara mbili au zaidi. mfano mmojawapo ni kitambaa cha nguo. huwezi kukipigia hiki kitambaa mahesabu katika pato la taifa kwani bado kipo katika mchakato wa kutengeneza bidhaa ya mwisho ambayo inaweza kuwa ni shati au gauni au suruali. pia ili kupata thamani ya hiyo bidhaa, ni mpaka mteja ainunue kwa matumizi binafsi. so kama mteja wa mwisho kanunua suruali kwa sh. 7000/- basi hicho kiasi ndio kinaingia kwenye pato la taifa. hapa tunazungumzia ile bidhaa iliyotengenezwa ndani ya nchi husika, na wala si mtumba au iliyotengenezwa nje ya nchi. bidhaa au huduma ambazo ni imported au exported zina mahesabu yake katika kukokotoa GDP. hayo macheche ni ya kuanzia tu. najua kuna wachumi wa kweli humu ambao haya mambo zaidi ya kuyasoma tu wanayafanyia kazi pia. katika hilo basi tubadilishane mawazo ili kuweza kujua mchakato halisi wa kujua pato sahihi la nchi yetu. hii pia itawasaidia wale wengine katika sekta tofauti kujua wanachangiaje katika pato la taifa lao (Tanzania).
   
 2. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #2
  Jun 27, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Kiukweli hii sio afya ya akili kabisa. What's wrong when it comes to serious issues of our nation? May be politics and socializing are too general to discuss. Tupende kujua pia na hali yetu ya uchumi tusingoje kuambiwa tu
   
 3. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #3
  Jun 27, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Duh kwa Tanzania kwa kweli ni makadirio tu maana hakuna uwekaji takwimu. Tena ukizingatia miundombinu yetu sina hakika kama kweli maelezo ya serikali juu ya pato la mwananchi ni sahihi. Tukiacha hizo blah blah, ukweli ni kwamba pato halisi la Mtanzania linazungumzika vizuri (yaani kama limeongezeka au kupungua) kwa kutumia strong/hard currency. Maana over recent kumekuwa na vijitabia vya kulitaja in Tsh wakijua fika kwa kuwa pesa yetu imezidi kuporomoka kwa hiyo sio measure halisi ya mafanikio kiuhalisia. Ukiachiia mbali hilo pato lenyewe liko very skewed and not normally distributed with probably 5%-10% of the people representing more than 80% of Tanzanians in consumptions.
   
 4. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Ni kweli kuwa ni asilimia ndogo ya watz ndio wanaowakilisha asilimia kubwa ya watz kwenye suala zima la consumption na uzalishaji. Kiuhalisia ukichukua pato linalozalishwa na wachache (ambao wanakuwa apportioned kwa wengi) ukaweka matumizi ya serikali (ambayo inaagiza kama %90 za bidhaa toka nje) ukachanganya na uwekezaji, ukaweka na net export, utagundua kuwa GDP inakimbilia negative. Kwa nini wasikisie hilo pato ili kuwapumbaza wananchi?
   
 5. O

  Ogah JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Nchi yetu imefilisika tangu zamani zile za Mwinyi.........ni usanii tu unaendelea
   
 6. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mkuu usheheneze na vijitakwimu kidogo kuweka mambo sawa
   
 7. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nchi yetu haijawahi kuwa tajiri kwahiyo haijawahi kufilisika.
   
 8. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #8
  Jun 28, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mkuu unazungumzia utajiri wa aina gani?
   
 9. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #9
  Jun 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Utajiri kwa namna unavyofahamika kuwa utajiri. Tuache dhana ya kwamba tunarasilimali lundo kama jamii ya wafugaji wanaozunguka na mifugo yao maelfu huku wakijiona matajiri. Utajiri ninaozungumza hapa ni hali bora ya afya, elimu, miundo mbinu kuanzia barabara nk. Pato la mwananchi kama mada inavyojieleza, kilimo cha kisasa, maji safi na salama, empolyment, social benefits etc.
   
 10. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,193
  Trophy Points: 280
  Umesema

  Ondoa "fulani" weka "zote". GDP ni total ya uzalishaji, si "uzalishaji wa bidhaa na huduma fulani".

  Rekebisha hilo kwanza tunaweza kuendelea kwingine huko, kwa mfano, kwa nini GDP ni kipimo kibaya cha uzalishaji, kipimo kipi kinaweza kuwa kizuri kuliko GDP na mengine mengi.
   
 11. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Kabla ya kujadili kwa kina ambacho mwanzishaji wa mada ameomba, naona ni vyema wote tukapasha kidogo ili tujue ni nini hasa wanatakwimu wa NBS wanamaanisha kuhusiana na hii misamiati ya uchumi. Naambatanisha, ila tu msiwe wavivu kusoma
   

  Attached Files:

 12. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Yah its true GDP ni contraversial. Wapo wengine wanaamini kwenye adjustments za GNI.
   
 13. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  Nadhani watu wa NBS nao wanatumia international standards kama watu wa uhasibu wanavyotumia viwango vya kimataifa vya IAS -International Accounting Standards. Ni kweli pia hapa tunazungumzia uzalishaji wa bidhaa zote na huduma pia. Kiujumla GDP ni zao la matumizi binafsi, uwekezaji, matumizi ya serikali na jumla ya export ukitoa import zote (net export). Matumizi ya serikali % kubwa ni imports. Matumizi binafsi % kubwa ni imports (pamoja na second hand products ambazo hazihesabiwi katika GDP). Upande wa uwekezaji tunategemea zaidi FDIs - foreign direct investment. EXIM ndo tuko hoi kabisa. Kitendo cha kusema kuwa pato la taifa limeongezeka, hii inaleta mashaka katika kutumia GDP Kama kipimo
   
 14. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani kabla ya pato la taifa tuazie kwenye basic level ili na tusiojua mambo ya uchumi tufaidike. Kwa mwananchi wa kawaida wa tanzania ni bora kujua pato la familia. tena wakiwepo watu wa takwimu watambie watani pato la familia ya mkoa wa arusha, mwanza na dar then waote na wastani wa pato la familia mikoa ya kigoma, mtwara lindi.

  na ukija wengi wetu tuafanya kazi kwenye service delivery( JWTZ, Wabunge, Wahasibu,Madaktari,Wanasheria,wataalamu wa IT) industry na sio kwenye real production( Wakulima na wafanyakazi wachache viwandani). sasa changamoto kwenu wataalamu how or wht do u basic huma servive delivery account in GDP.

  Sasa kuna takwimu zinaonyesha ratio ya mbunge per idadi ya watu nchi zilizoendela ni kuwa kuliko sisi. Lakini hapo hapo ratio ya madaktari per idadi ya wagonjwa kwa nchi yetu ni kubwa sana kulinganisha na nchi zilozoendelea. K wa hiyo utaona kuna tatizo la priority
   
 15. PatPending

  PatPending JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2010
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 490
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Naomba kufahamu maana halisi ya hii niliyoweka katika nyeusi. Ni kipi hasa kinakuwa hasi? Asilimia ya ukuaji wa pato ya taifa toka mwaka hadi mwaka?, Pato la taifa katika bei mbalimbali au?

  Naomba ufafanuzi maana hicho ulichoandika hakileti maana jinsi kilivyo

  Naomba pia utufafanulie hicho katika nyeusi. Tofauti ya GNI au GNP na GDI au GDP ni eneo la uzalishaji tu. Na pia hizo ni adjustments za namna gani unazozizungumzia?

  Hii si kweli, vitabu vya bajeti si mnaviona jamani? Matumizi makubwa yanakwenda kwenda kwenye matumizi ya kawaida (recurrent expenditure) ambayo inajumuisha mishahara (personnel emolument) na matumizi ya kawaida (other charges). Manunuzi ya vifaa vya uzalishaji ambavyo vyingi ndio vinavyotoka nje ya nchi yanakuwa chini ya bajeti ya maendeleo.

  Mkuu watu wanalipia kodi bidhaa zao wanazoagiza kutoka nje na hizi kodi ndio zinazohesabika katika ukokotoaji wa pato la taifa. Kuna njia kuu mbili za kukotkooa pato la taifa, ile ya uzalishaji (production based) na ile ya matumizi (expenditure based) na kodi hizi zote zinaingia katika ukokotoaji wa pato la taifa kwa kutumia matumizi. Econ 101, Expenditure based GDP = C + I + G + netX, pale ambapo G ni matumizi ya sirikali ukiondoa makusanyo yao ya kodi.
   
 16. Raia Fulani

  Raia Fulani JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2010
  Joined: Mar 12, 2009
  Messages: 10,219
  Likes Received: 84
  Trophy Points: 145
  mkuu Pat nilikuwa sijapitia hii pdf uliyobandika hapa kutokana na mibano fulani fulani. naona hii kitu itatoa majibu ya maswali yote ambayo nilikuwa nayo na pia wengine. suala la msingi ni kudownload hii report na kuisoma kwa umakini na hapo tutaepuka sintofahamu nyingi vichwani mwetu. naomba kuisoma kwanza ili kupata mwanga zaidi
   
Loading...