Tujadili kuhusu maisha baada ya Chuo

Kwanza tukubaliane kabisa lifestyle ya chuo bi yatifauti sana na maisha halisi ya mtaani, Maisha ya chuo yana maigizo mengi sana. Watu wanaishi kwa fashion na kukatchup na latest technologies ilihali uwezo ni mdogo, wanabeti sana na hawana kipato, kama huu mchezo wa kubeti umefanya madogo wengi wasimalize chuo, na amini usiamini wanachuo na majobles ndio wanaojaza mabet shop ya mjini hapa, Anyways twende kwene mada.

Ajira ni tatizo la dunia. Wanafunzi wengi huwa wana expectations kubwa sana kwa njia rahis na hapo ndio huwa tatizo linapoanzia wakishindwa kufikia malengo kwa time limit walijiwekea, wanapata msongo wa mawazo sababu vyuo vyetu vingi sio job oriented wao ukishapata gpa ya 4.8 we ndio wewe na ushamaliza kila kitu.

Kitu cha ajabu kabisa hapa bongo ni rahis kwa mtu aliesoma VETA umeme(sijui inaitwaje hii kozi) kupata kazi kuliko mwenye bachelor ya ELECTRICAL ENGINEERING pale UD. Ni rahis mtu alosoma PC maintanance VETA kupata kazi kuliko Mtu alosoma bachelor of computer science UD au vyuo vingine ? If you ask me why ? sijui hata sababu, wenye bachelor majobless wenye certificate wanafanya kazi aisee kazi ipo.

Sasa basi ndugu zetu sababu mwisho wa picha ni hela ONDOA ILE PRIDE YA MIMI NI BACHELOR HOLDER FANYA KAZI YEYOTE ITAKAYOKUPA KIPATO MAISHA KWA GROUND NI MAGUMU SANA. Jiandaeni kisaikolojia kwa disappointment za kutosha ila hakuna kukata tamaa as long as upo hai unatakiwa uendelee kupambana. Elimu haijawah kumtupa mtu siku moja itakutendea haki ya kitu ulichokuwa unakitaka wakati huo ushaadapt mazingira unalijua game vizuri unaweza pambana vizuri sasa.

Kwa mnaosoma technical studies jitahidini kuwa kujua ivyo vitu mmesoma, me ntatolea mfano wa IT/CS wakuu kamaten hivi kisawa sawa yan usijue kijuu juu jua kweli kweli. Kamata kimoja unachoona unaweza kijue kweli kweli

1.LINUX
2.PROGRAMMING LANGUAGES
Java( inakuwaga mandatory)
Python
Java script
C++
C#
PHP
3. NETWORKING
4. WEB DESIGNING, ujue html, css, php

Huu ni mfano tu basi kwanini ujue haya sababu interview nyingi sikuiz wanataka wampe mtu anaeweza kazi akiingia kazini kazi ianze effectively na sababu nyingine ni mbinu tu yakuwapunguza watu ni wengi isije ikawa wanaojua wanaachwa wanaenda wasiojua...

NB: vitu vingi vyakufanya practical tutorial zipo you tube na ni free.

Kitu kingine cha msingi KAZI YA MTU HAIKUFANYI TAJIRI, ukiweza kujiajiri ndio rahis kuwa TAJIRI, so kama unaweza kuinvest na ukawa creative THERE YOU ARE.... Ishini humo wadogo zetu mtaaani sio main cafetaria wala hall seven sijui hall one wala kwame nkuruma wala utawala wanaume mtaumia sana msipokaa sawa wanawake mtatumika sana mpaka unakuja kukaa sawa ushatumika sana na mabrotheman wa benk
Hizo programming language unawezaje kutengeneza hela mtaani?


Am curious to know.
 
Kiukweli hili jambo ni gumu sana, pia ni rahisi kulielezea kwa mdomo, kiufupi ni muda vijana tujifunze kuendena na mazingira na kukubari ukweli kuwa ajira ni mtiti kwani hii itapunguza expectations ambazo mara nyingi ndio zinatesa.

Tuache kujifariji uongo sijui kilamtu na bahati yake, sawa kuna bahati lakini ukweli nao huwa unasimama vile vile ajira ni tatizo ni tatizo basi.

Ni muda wa vijana kujifunza mbinu mpya na skills ambazo hazifundishwi mashuleni ila zinamake pesa mtaani, Mfano hivi sasa mtandaoni kuna fursa kibao sana, kama

1. Designing & graphics, sasa kama una pc afu unachekia movies tu basi endelea, vizuri.

2. Copywriting, ujuzi wa kuuza kupitia maandishi, ingia youtube search hilo neno utaelewa nini kinafanyika, kama ukiwa na ujuzi huu basi utauza kitu chochote mtandaoni kwa urahisi hivyo hata kama huna mtaji wa fedha unaweza kuuza bidhaa ya mtu mwingine na ukapata kamisheni

2. Affiliate Marketing, uuzaji wa ushirika ( udalali mtandaoni) huna haja ya kuwa na bidhaa hapa wewe ni kuuza bidhaa za watu wengine kisha unapata kiasi chako. Pia Google utaelewa vizuri inavyofanya kazi,

3. Elimu ya matangazo ya Sponsored[Facebook & Instagram] hii naweza sema kila siku inashika kasi wafanyabiashara wengi sikuhizi wanataka watu wakuwawekea matangazo. [ nimesoma Journalism lakini hii ndio kazi yangu kwa sasa sikosi hela ya kula]

4. Video editing, hii sina haja ya kuelezea sana

Kiufupi skills zipo nyingi ila hizo ni chache kwa haraka haraka nimezitaja, mwingine pia anaweza kuongezea.


Uzuri ni kwamba hivyo vyote unaweza kujifunza bure mtandaoni na kama ni garama ni ndogo sana.

Shida vijana wengi bongo tunaingia Youtube kuangalia udaku. Wakati youtube ni darasa zuri sana. Ila maisha pia ni kuchagua
 
Back
Top Bottom