Tujadili kauli ya kinana kwamba wabunge wa ccm wanapitisha miswada mibovu

chaikavu

JF-Expert Member
Apr 18, 2015
760
473
Kinana akiwa mwanza alisema wabunge wa ccm wanapitisha miswada na sheria zisizo na tija. Hii maana yake ni kwamba wabunge wa ccm ni mbumbumbu,wajinga, na wapumbavu wasio jua wanachokifanya. Naama nyingine ni kwamba serikali iliopo madarakani pamoja na wabunge wake hawapaswi kuwepo /kuongoza hii nchi. Maana nyingine ni kwamba wabunge wa ccm wameuza nchi kwa umbumbumbu wao kwenye mambo muhimu ya nchi.

Kauli ya kinana inadhihirishwa na msuguano unaoendelea bungeni sasa hivi kuhusu miswada ya gesi na mafuta. Wabunge wa ccm wanadhihilisha upumbavu/umbumbumbu huu kwa kulazimisha kupitisha miswaada hii ambayo wabunge wa upinzani wamesema marekani ndio wanaoishinikiza serikali kupeleka miswada hii bungeni kwa dharura ili marekani ijue maslahi yake kwenye gesi na mafuta.

Jana lisu alisikika akisema 'mwambieni obama mambo yameshindikana'

hivi kumbe kinana anajua chama cha ccm kina watu ambao ni punguani wasioweza pambanua mambo ila anashindwa kuwambia liv
 
Kinana alikuwa akicheza siasa, lakini nafikiri atajuta kuyatamka hayo aliyoyasema Mwanza. Asingesema kama angejua kuwa kuna miswada tatanishi iko bungeni tena kwa hati ya dharura na itapingwa kila kona, lakini wabunge wake hawatakuwa na nguvu za kupinga bali kuiunga mkono serikali kuipitisha.
 
Kinana alikuwa akicheza siasa, lakini nafikiri atajuta kuyatamka hayo aliyoyasema Mwanza. Asingesema kama angejua kuwa kuna miswada tatanishi iko bungeni tena kwa hati ya dharura na itapingwa kila kona, lakini wabunge wake hawatakuwa na nguvu za kupinga bali kuiunga mkono serikali kuipitisha.

Hata hivyo sidhani kama shinikizo ni Marekani, kwa sababu sijaona maslahi makubwa ya sekta hiyo hapa Tanzania kuliko wachina na Ulaya.
 
Kwa miswada hii hapa ndio tuwapime wagombea uraisi wa ccm wanaojinadi kuhusu wananchi kunufaika na raslimali zetu,,sioni hata mmoja kati ya aspirants wote anaezungumza hili,kifupi wote ni mbumbu
 
Back
Top Bottom