TUJADILI: Job Ndugai kuandika barua ya kujiuzulu kwa mtu asiyehusika ni bahati mbaya au makusudi?

Mimi namuulizia huyo ndg Job yuko wapi kwa sasa?.
Haonekani na hapatikani hata kwa namba yake ya simu ninayoifaham hapatikani, kulikoni huko?
 
Mimi namuulizia huyo ndg Job yuko wapi kwa sasa?.
Haonekani na hapatikani hata kwa namba yake ya simu ninayoifaham hapatikani, kulikoni huko?
Anajipanga upya. Mtamsikia tena 2025 (kama atakuwa hai) akija na ngonjera mpya kuwa alilazimishwa kujiuzulu. Pengine ataibukia chama kingine kama mgombea uraisi na kutumia kisingizio cha kulazimishwa kujiuzulu sababu ya kutetea maslahi ya taifa kama karata ya kuombea kura.
 
Mwacheni Mzee Ndugai apumzike

Watoto wa Marehem wanataabika sana mwingine tayari yupo kizimbani Mtwara kwa kosa la kupiga sindano za sumu wenzie
 
Government doc goes on paper.yawezekana iliandikwa na ndugai mwenyewe halafu original yenyewe ndio akaisubmit.

Ile ilkua taarifa tu kwa umma ,siyo barua ya kiserikali.nawaza tu
 
Ni vigumu kuamini kuwa Mheshimiwa Ndugai hajui utaratibu wa kikatiba wa kujiuzulu nafasi ya uspika. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania spika au naibu spika anaweza kujiuzulu nafasi yake kwa kuandika barua kwa BUNGE na kuisaini. Spika atahesabika kuwa amejiuzulu baada ya barua yake kupokelewa na Bunge.

Afisa wa bunge anayeshughulika na mambo ya utawala ni Katibu wa bunge. Lakini Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu wa CCM, mtu ambaye katiba haijamtaja katika mchakato wa spika kujiuzulu.

Kwa mantiki hiyo, kikatiba Ndugai bado hajajiuzulu, maana hajaandika barua ya kujiuzulu kwa mamlaka inayohusika!! Je hii imetokea kwa makusudi au kwa bahati mbaya? Sidhani kama angeamua kuchukua uamuzi mkubwa kiasi hicho bila ya kujiridhisha matakwa ya kikatiba kuhusu hatua hiyo au bila ya ushauri wa kisheria.

Ninaamini Ndugai amefanya hivyo kwa makusudì, huku akijua kuwa maadui zake amewapa mwanasesere badala ya mtoto!! Watakapogundua kuwa wamepewa mwanasesere atakuwa amejipanga kwa mapambano sawasawa!!

Kinachonishangaza zaidi ni katibu wa CCM kukubali kupokea barua hiyo ambayo kikatiba haikupaswa kuelekezwa kwake!! Nilidhani asingekubali kuipokea bali angemwelekeza mahali pa kuipeleka!!
Baada ya JYN kuandika barua batili kujiuzulu uspika, kwanza nilimuombea JYN msamaha
Kisha kuna kitu nilipendekeza kwenye uzi huu
Je, wajua haramu isipoharimishwa inageuka halali? Na batili isipobatilishwa inageuka halali. Je, tuhalalishe ubatili huu kwa mhimili wetu wa Bunge? nilipendekeza
3. Japo Spika Mhe. JYN tayari ameisha jiuzulu uspika, kujiuzulu huko, japo ni kujiuzulu batilifu, lakini kujiuzulu ni kujiuzulu na Spika amejiuzulu, lakini kwa kuheshimu katiba, lazima ubatili katika barua hizo uondolewe kwa kuandikwa barua rasmi kwa mujibu wa katiba.
4. Bunge lipokee kimya kimya barua mpya ya kujiuzulu kwa Spika iliyoandikwa kwa mujibu wa katiba, kisha Bunge ndio litoe copy kwa CCM.
Hitimisho.
Namalizia kwa lile swali la msingi la uzi huu
Je wajua, haramu Isipoharimishwa Inageuka halali?, na batili Isipobatilishwa inageuka halali!. Je, Tanzania, tuhalalishe ubatili huu wa kujiuzulu kinyume cha katiba kwa mkuu wa mhimili wetu wa Bunge? Kama katiba imeelekeza jinsi ya kufanyika kwa jambo fulani, kuna sababu gani ya msingi ya kutofuata katiba na badala yake tukumbatie ubatili?

Jumatatu Njema.
Pascal
Habari njema kwa watu wote, pendekezo No. 3 na No. 4 Katika bandiko hili, limetekelezwa kwa asilimia 100% kama lililopendekezwa.
Hivyo sasa ule ubatilifu katika barua ya kujiuzulu kwa JYN umeondolewa kama nilivyo shauri, kwa kuwasilishwa barua mpya halali, ambayo ni backdated.
Hivyo ile taarifa ya JYN kwa waandishi wa habari, kuwa ameandika barua kwa Katibu Mkuu CCM, sasa imebatilishwa na imefutwa kwenye website ya Bunge, barua rasmi ni kwa Katibu wa Bunge, na CCM kupewa nakala.
Hongera sana Bunge letu tukufu kuubatilisha ubatili huu. Sasa kwenye hili la Spika umebaki ubatili mmoja wa Naibu Spika, Dr. Tulia Akson kujiuzulu u Naibu Spika, kabla ya kugombea Uspika.
P
 
Ni vigumu kuamini kuwa Mheshimiwa Ndugai hajui utaratibu wa kikatiba wa kujiuzulu nafasi ya uspika. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania spika au naibu spika anaweza kujiuzulu nafasi yake kwa kuandika barua kwa BUNGE na kuisaini. Spika atahesabika kuwa amejiuzulu baada ya barua yake kupokelewa na Bunge.

Afisa wa bunge anayeshughulika na mambo ya utawala ni Katibu wa bunge. Lakini Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu wa CCM, mtu ambaye katiba haijamtaja katika mchakato wa spika kujiuzulu.

Kwa mantiki hiyo, kikatiba Ndugai bado hajajiuzulu, maana hajaandika barua ya kujiuzulu kwa mamlaka inayohusika!! Je hii imetokea kwa makusudi au kwa bahati mbaya? Sidhani kama angeamua kuchukua uamuzi mkubwa kiasi hicho bila ya kujiridhisha matakwa ya kikatiba kuhusu hatua hiyo au bila ya ushauri wa kisheria.

Ninaamini Ndugai amefanya hivyo kwa makusudì, huku akijua kuwa maadui zake amewapa mwanasesere badala ya mtoto!! Watakapogundua kuwa wamepewa mwanasesere atakuwa amejipanga kwa mapambano sawasawa!!

Kinachonishangaza zaidi ni katibu wa CCM kukubali kupokea barua hiyo ambayo kikatiba haikupaswa kuelekezwa kwake!! Nilidhani asingekubali kuipokea bali angemwelekeza mahali pa kuipeleka!! Hivi CCM makao makuu hawana mwanasheria wa chama?

Usikute huyo Katibu mkuu wa CCM naye akawa ni sehemu ya mchezo ili kuzuga huku akijua mchezo unakoelekea!! Mama shituka!! mhoji katibu wako kwa nini asingemwelekeza Ndugai utaratibu wa kikatiba wa kujiuzulu?

Mchezo umepangwa kuchezewa mahakamani na wachezaji wanajulikana!! mchezaji wa kiungo upande wa Ndugai ni MBATIA!! Ndugai atakuwa kimyaaa!!!! As if hajui kitakachoendelea!!
sio mbaya kujiuzulu kwake amepata muda wa ziada wa kuchunga ng'ombe wake saa hz mzee wa watu
Screenshot_20220429-091807_Gallery.jpg
 
Back
Top Bottom