mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,663
- 18,036
Ni vigumu kuamini kuwa Mheshimiwa Ndugai hajui utaratibu wa kikatiba wa kujiuzulu nafasi ya uspika. Kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri wa muungano wa Tanzania spika au naibu spika anaweza kujiuzulu nafasi yake kwa kuandika barua kwa BUNGE na kuisaini. Spika atahesabika kuwa amejiuzulu baada ya barua yake kupokelewa na Bunge.
Afisa wa bunge anayeshughulika na mambo ya utawala ni Katibu wa bunge. Lakini Ndugai ameandika barua ya kujiuzulu kwa Katibu wa CCM, mtu ambaye katiba haijamtaja katika mchakato wa spika kujiuzulu.
Kwa mantiki hiyo, kikatiba Ndugai bado hajajiuzulu, maana hajaandika barua ya kujiuzulu kwa mamlaka inayohusika!! Je hii imetokea kwa makusudi au kwa bahati mbaya? Sidhani kama angeamua kuchukua uamuzi mkubwa kiasi hicho bila ya kujiridhisha matakwa ya kikatiba kuhusu hatua hiyo au bila ya ushauri wa kisheria.
Ninaamini Ndugai amefanya hivyo kwa makusudì, huku akijua kuwa maadui zake amewapa mwanasesere badala ya mtoto!! Watakapogundua kuwa wamepewa mwanasesere atakuwa amejipanga kwa mapambano sawasawa!!
Kinachonishangaza zaidi ni katibu wa CCM kukubali kupokea barua hiyo ambayo kikatiba haikupaswa kuelekezwa kwake!! Nilidhani asingekubali kuipokea bali angemwelekeza mahali pa kuipeleka!! Hivi CCM makao makuu hawana mwanasheria wa chama?
Usikute huyo Katibu mkuu wa CCM naye akawa ni sehemu ya mchezo ili kuzuga huku akijua mchezo unakoelekea!! Mama shituka!! mhoji katibu wako kwa nini asingemwelekeza Ndugai utaratibu wa kikatiba wa kujiuzulu?
Mchezo umepangwa kuchezewa mahakamani na wachezaji wanajulikana!! mchezaji wa kiungo upande wa Ndugai ni MBATIA!! Ndugai atakuwa kimyaaa!!!! As if hajui kitakachoendelea!!