Tujadili jinsi ya kuisaidia familia ya mwandishi marehem mwangosi!

samilakadunda

JF-Expert Member
Oct 13, 2011
1,780
354
Nakereheka sana namajadiliano ya wanasiasa, waandishi wa habari wanaharakati na serikari ya jamhuri ya muungano wa Tanzaniani,jinsi wanavyo lijadili suala hili la huyu nduguyetu,aliye itumikia serikali hii na kutoa mchango mkubwa,naami alikuwa na malengo na na mtazamo mkubwa juu ya familiaa yake na hasa watoto wake wanne aliowaacha hapa duniani wasijue nn hatma ya maisha yao kwani nguzo muhimu ya mafanikio yao imekatwa pasipo hata kuwaachia hata neno moja.naomba kama tunavyojadili juu ya kifo chake pia tujadili jinsi ya kuwasaidia hawa watoto walioachwa baharini na nahodha kutoweka pasipo waaga.kwa maelezo haya wote niliowataja hapojuu kilamoja kwa nafasi yake atafakari naaone kamayeye angekuwa ndio daudi ! Naumia sana naomba kuishia hapa.
 
Ni kweli unachosema tuache propaganda za siasa tujadili pia hatma ya familia ya marehemu. Mimi binafsi naona kila aliyeguswa na jambo hili kusaidia lkn iwepo njia ya uhakika kuwa atakayesaidiwa ni mlengwa (watoto wa marehemu).
 
Wewe kama una nia ya kweli ya kutoa msaada onana na mmoja wa wanafamilia wake au fika moja kwa moja nyumbani kwake. Bila shaka ukifika watakupokea na kupokea ulichowapelekea. Sasa hapa unataka watu wajadili nini hasa? Watu wengine bwana.
 
Wewe kama una nia ya kweli ya kutoa msaada onana na mmoja wa wanafamilia wake au fika moja kwa moja nyumbani kwake. Bila shaka ukifika watakupokea na kupokea ulichowapelekea. Sasa hapa unataka watu wajadili nini hasa? Watu wengine bwana.

Anataka watu wajadili namna ya kuwachangia,watanzania tumekuwa na ubinadamu na utamaduni wa kuchangiana
kila inapotokea tumepata matatizo.wewe ni matanzania kweli,akienda kutoa yeye tu yamkini hawezi kutoa kiasi cha
kutosha lakini akiwashirikisha wengine atakuwa amepanua wigo wa michango.Think Twice"
 
hili wazo jamiiforum wako agaist.maggid ameweka post hapa na ameongea na mjane amesema anahitaji kusaidiwa kulipia pango la ofisi na kununulia fotocopier machine,wameiondoa jukwaa la siasa,mimi nikaicopy na kuiweka tena kwa jina langu,nayo wameitoa na sasa wakati nasearch ili nione responce ya watu,nimekuta wameipeleka jukwaa la matangazo madogo.jamani tatizo ni nini?
 
[h=2]Mjengwablog Inachangisha Pole Ya Kumsaidia Mjane Wa Daud Mwangosi Kuendesha Bishara Ndogo...[/h]
Ndugu zangu,

Daud Mwangosi ambaye pia alikuwa ' Mwanakijiji' mwenzetu hapa Mjengwablog hatunaye tena.

Nimemfahamu Daud Mwangosi tangu mwaka 2004 nilipofika Iringa. Tangu wakati huo, amekuwa akiinipa ushirikiano mkubwa kwenye kazi ya kutangaza shughuli za kijamii kwenye Vyuo Vya Maendeleo ya Wananchi.

Ni kwa kupiga picha za televisheni na kurusha habari kwenda Channel Ten; Iwe ni kwenda naye Ilula au Njombe, Daud Mwangosi alikuwa tayari kila nilipomwomba aongozane nami kwa shughuli ya kijamii.



Mara nyingi nilimkuta Daud ofisini kwake ( Picha ya kwanza juu) akichapa kazi na huku mkewe akimsaidia kazi nyingine. Daud Mwangosi alikuwa mbunifu. Alikuwa ni mwenye kiu ya kujifunza mambo mapya kwenye teknolojia ya habari na mawasiliano.


Najua Daud Mwangosi alikuwa na malengo ya kuendeleza shughuli zake za ujasiriamali. Mbali ya mambo mengine, alikuwa na Photocopy machine ya kumwongezea kipato ambayo iliharibika mwaka jana. Akawa na ndoto ya kuwa na studio ndogo ya kupiga picha za vipande ( Passport Size). Yote ni katika kumwongezea kipato kutunza familia yake.


Leo Daud Mwangosi hayuko nasi. Ameacha familia, mjane na watoto wanne; Itika Mwangosi ( Mjane) Nehemia Mwangosi ( 17) Kidato cha Nne Malangali Sekondari, Hetzgovina Mwangosi (12) Bathsheba Mwangosi (9) na Moria Mwangosi ( 2)
Namini Daud Mwangosi angependa shughuli alizokuwa akizifanya ziendelee na zije kuwasaidia watoto wake pia.


Jana na leo nimewasiliana na mjane wa marehemu Mwangosi ambaye bado yuko Tukuyu. Nikamwambia kuna ' Wanakijiji ' wa Mjengwablog walioguswa na msiba wa Mwangosi na wangependa kutoa pole yao imsaidie katika kupata mwanzo kutoka hapa alipo sasa. Mjane wa Mwangosi amefarijika sana kusikia habari hizo.


Kwa vile tayari ameahidiwa msaada wa kusomeshewa watoto. Msaada anaouhitaji kwa sasa ni kupata photocopy machine ( Used) na kodi ya pango la ofisi. Jumla yake kwa yote hayo mawili haitazidi shilingi za Kitanzania milioni mbili na laki mbili. Hivyo msaada anaouomba kwa wenye mapenzi mema ni shilingi 2, 200,000 ( Shilingi milioni mbili na laki mbili). Shughuli hizo zitamsaidia kujikimu.


Kutokana na hali aliyo nayo sasa, Mwenyekiti wenu napendekeza nichukue jukumu la kuratibu michango hiyo. Shime tushirikiane kufanikisha hili ili tumsitiri mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi.
Napendekeza ifikapo mwisho wa mwezi huu ( Septemba) tuwe tumefanikisha zoezi hili kwa yeyote aliye nacho, hata kama ni shilingi elfu tano, ni msaada mkubwa.


Mjengwablog bado tuna rekodi nzuri katika kuchangishana kuwasaidia wenye kuhitaji. Itakumbukwa, huko nyuma, kwa pamoja, tulifanikisha kukusanya michango ile ya watoto wa Somalia na kuikabidhi UNICEF, Dar es Salaam. Ni zaidi ya shilingi milioni mbili.
Tulifanikisha mchango wa kusaidia ukarabati wa maktaba ya Kijamii kijijini Mahango, Madibira. Zaidi ya shilingi milioni nne.

Sasa ni zamu ya kumchangia mjane wa mwenzetu Daud Mwangosi. Kinachohitajika ni milioni mbili na laki mbili.


Naam, kutoa ni moyo, usambe ni utajiri.


Mwenyekiti wenu na familia yangu naanza kwa kuchangia shilingi laki moja.

Na kama kawaida, taarifa za waliochanga na kiasi kilichopatikana kitawekwa kwenye blogu kwa kila mmoja kuona.


Namna ya kuwasilisha michango: Tumia M-Mpesa, Tigo Pesa, Airtel Money au NMB Mobile. Kwa namba 0754 678 252, 0712 95 61 31, 0788 111 765 ( Kwa walio nje mnaweza kutuma kwa Western Union, jina la mpokeaji- Maggid Mjengwa)



Natanguliza Shukrani.


Maggid Mjengwa,
Iringa.
0788 111 765
Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo

Post yenyewe ndoo hii hapa.utaona kama haitaondolewa.jamani tatizo nini? nadhani watani BAN hawa
 
Back
Top Bottom