Tujadili; je ni haki watanzania kununua huduma ya maji wakati tunalipa kodi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tujadili; je ni haki watanzania kununua huduma ya maji wakati tunalipa kodi?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by blueray, Sep 25, 2012.

 1. b

  blueray JF-Expert Member

  #1
  Sep 25, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi, naomba tujadili mada hii kwani hili swala la kununua maji yanayoletwa kwetu na mamlaka za taifa za maji Kama vile DAWASCO Mimi haliniingii akilini. Sasa hivi maji imekuwa ni biashara kubwa ya serikali kuwalangua wananchi wake. Sasa hivi gharama za maji vile vile za umeme ni kubwa sana na Kila siku zinapanda! Maji haya, na hata umeme, yanazalishwa kutokana na rasilimali zetu ambazo tunajivunia na kuwajibika kuzilinda kama watanzania. Hata mishahara wanayolipwa wafanyakazi wa mamlaka za maji za miji na TANESCO inatokana na kodi zetu. Hata vipuli na mafuta ambayo wakati mwingine yanahitajika kuendesha mitambo ya kusukuma maji au kuzalisha umeme ni kodi zetu zinazotumika kununulia. Kwa nini sasa haya maji na umeme serikali inatulangua? Sasa hivi si kuchangia tena ni kulanguliwa hadi wengine tusio na kipato kizuri tunashindwa kumudi. Wanajamvi tutafakari, je hii ni sawa?
   
 2. Mzalendo Mkuu

  Mzalendo Mkuu JF-Expert Member

  #2
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 737
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Tatizo hapa ni kupata maji na si kulipia. Kulipia maji ni wajibu kwa watu wote. Kumbuka kuwa maji ni huduma kama ilivyo kwa umeme na afya ambazo pia zinalipiwa.
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Sep 25, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Ni kutokana na kuwa na serikali (MAITI)
   
 4. georgeallen

  georgeallen JF-Expert Member

  #4
  Sep 25, 2012
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 3,758
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Maji na umeme ni huduma. Tatizo hapa ni serikali kutumia hizi huduma kibiashara na kama chanzo cha mapato!!. Watumiaji wengine hawapati maji lakini bado wanaletewa bili kila mwezi. Hizi ni kero tunazotakiwa kuzi- address 2015
   
 5. S

  Savannah JF-Expert Member

  #5
  Sep 26, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 238
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  [TABLE]
  [TR]
  [TD]Kinacho takiwa ni sekali kuhakikisha kuwa inawapatia maji safi na salama wananchi wake. Hii lazima iwe haki ya kikatiba. Huduma hii inalipiwa ili kukabili gharama ya uendeshaji (operation and maintenance). Kodi ina mambo mengi ya kufanya na kwa suala la maji itatumika kama "capital cost " katika kuanzisha na/au kupanua miundombinu (mabawa, mitamo ya kusafisha maji na usafirishaji wa maji).
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 6. m

  mzeelapa JF-Expert Member

  #6
  Sep 26, 2012
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 1,034
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Kodi zetu zinatumika kwa mambo mengi. Ziko huduma ambazo tunazipata bure, nyingine kwa bei ya chini kulinganisha na gharama halisi. Huduma za maji kuna maeneo mengine wanapata bure na maeneo mengine tunalipia, sehemu nyingine wanachangia kutegemeana na sababu mbalimbali. Hivyo unachotakiwa kulalamikia ni ikiwa unacholipia hakilingani na huduma unayopata. Kutoa kodi sio msingi wa kupata huduma bure.
   
 7. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #7
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo na kama Atc ingekuwepo ungetaka kupanda bure kisa ni ndege ya shirika la serikali na imenunuliwa kwa Kodi ya wananchi...
  Nenda kapate lunch maybe hujala mchana
   
 8. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #8
  Sep 26, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,767
  Likes Received: 2,494
  Trophy Points: 280
  kama kweli we nimlipa kodi rusha tax identification number yako!
  alafu usipende vitu vya bure! uanatumia tu nani akulipie
   
 9. b

  blueray JF-Expert Member

  #9
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu C.T.U
  Sina maana kama shirika limeanzishwa kwa misingi ya kufanya biashara kama ATC, TRL nk, basi tusilipie kwa sababu haya mashirika yameanzishwa kwa kodi zetu. Kuna tofauti kubwa kati ya ATC na Mamlaka za maji kama DAWASCO. Wakati ATC imeanzishwa kwa misingi ya kufanya biashara ili baadaye ijiendeshe yenyewe, Mamlaka za maji zimeanzishwa kwa misingi ya kutoa huduma kwa wananchi. Hata sheria zilizoanzisha hizi taasisi ni tofauti!
  Au kwa vile umekwishaaminishwa kwamba tanzania huduma ni za kununua huwezi kuwa na mtazamo tofauti?
   
 10. C.T.U

  C.T.U JF-Expert Member

  #10
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 4,708
  Likes Received: 1,210
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo unataka utumie bure tu mkuu maintanance cost watatolea wapi kodi yako wametumia kwenye kuanzisha na installation je wakubali kodi iongezwe kwa asilimia 7 na hizo huduma upate free ??
   
 11. b

  blueray JF-Expert Member

  #11
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  mkuu tunalipa kodi kila siku, tena kodi kubwa sana kuliko nchi nyingi pamoja Na vipato vidogo kwa wananchi. mfano kila mtanzania analipa VAT asilimia 18, kodi ya mapato kwa wenye mapato nk. kodi Tz ni nyingi sana. vile vile mkuu tumeikabidhi serikali isimamie rasilimali zetu kama madini ili iweze kutoa huduma hizi muhimu kwa wananchi ili iweze kujiendesha Na kulipa mishahara ya wafanyakazi wake nk. serikali isipotoa huduma muhimu kwa wananchi wake wewe utajivunia nini Kama mtanzania? kwa sababu hata siku moja serikali haitagawa vipande vya dhahabu kwa wananchi isipokuwa huduma
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Sep 26, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  tanzania ndiyo nchi pekee umeme ukikatika na kurudi wananchi wanashangilia.........huoooooooooooooooooo.

  tanzania ni nchi pekee ukimshangilia kiongozi unaona hadi magego ila ukimzomea kwa pumba zake unaenda jela kwa oder tu.
   
 13. Kijakazi

  Kijakazi JF-Expert Member

  #13
  Sep 26, 2012
  Joined: Jun 26, 2007
  Messages: 3,546
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 135
  Hao ndio watu ambao CHADEMA itakumbana nao siku moja wakija kuongoza nchi baada tu ya mwaka wote wataanza kulalamika na kutaka CHADEMA iwape kila huduma bure subirini tu huko mbele kutamu sana!
   
 14. Jodoki Kalimilo

  Jodoki Kalimilo JF-Expert Member

  #14
  Sep 26, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 8,628
  Likes Received: 2,049
  Trophy Points: 280
  Labda ungetuambia hicho unacholalamika ni kiasi gani kwanza na una familia ya watu wangapi ili tuangalie cost ya kila mmoja badala ya kulalamika, wakati mwingine bill za maji zinakuja kuja kubwa kutokana na sie wenyewe kutotumia maji vizuri mfano koki hazitengenezwi za maji zinavuja au mtu anaosha vyombo alafu anasuuza kwenye sink huku likimwaga maji kibao hata ndoo moja wakati unasuuza sahani 6. Ni kweli maji ni huduma lakini bei isiwe chini kiasi cha kushindwa kupata ela ya uendeshaji. Soma sera ya maji ya mwaka 2002 inahimiza wananchi kuchangia huduma za maji hata kama kwa sie tuliopo huku kijijini Imalamakoye ambako maji ni ya visima na chemchem tunatakiwa tuchangie ili tupate ela ya operation na maintanance. Wanaolipa kodi nchi hii ni 20% hivyo hatujafikia hatua ya kulalamika kwamba kodi zinatosha kwa kila huduma kutolewa bure au kwa kiwango cha chini

  FANYA UCHUNGUZI KWANZA UJUE MATUMIZI YA MAJI KWAKO YAKOJE MAANA UNAWEZA UKAWA KAZINI WATU WANAUZA MAJI NYUMBANI BILL INAKUJA KUBWA UNAWALAUMU DAWASCO
   
 15. Autorun

  Autorun JF-Expert Member

  #15
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 21, 2008
  Messages: 556
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  ni moja ya ilani ya chama tawala
   
 16. b

  blueray JF-Expert Member

  #16
  Sep 26, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kwa wakazi wengi wa dar wanapata bili zao bila kuzingatia matumizi au mita zinasomaje, sehemu nyingi Wanalipia kuanzia sh. 35,000, 50,000 au zaidi kulingana na maeneo. By the way hayo maji yenyewe yanapatikana kwa kuvizia!
  Lakini nimeshakuelewa, kumbe ni sera ya serikali kuuza maji tena ambayo muumba ametujaalia, badala ya kuyatoa Kama huduma! Au sh 35000 au 50000 kwa mwezi ndio kuchangia ghalama? Unajua kima cha chini cha mshahara wa watanzania? Au hata kima cha Kati, na maana ya kutumia hicho kiasi kwa ajili ya maji tu? Kwa hiyo hawa jamaa viongozi wa serikali waendelee kutumia kodi zetu kwenda nje ya nchi kutalii na familia zao na kuendelea kugawanya rasilimali zetu na Sisi tusiwadai hata huduma muhimu?
   
 17. peri

  peri JF-Expert Member

  #17
  Sep 26, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,588
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  umenena vyema
  mkuu, hili ni jibu tosha.
   
 18. Abunwasi

  Abunwasi JF-Expert Member

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Jun 25, 2009
  Messages: 3,166
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Kwanza ni wangapi wanapata huduma hii?? how much does it cost to provide such service? how many of us do pay taxes?
  where in the world is such service not paid for -urban areas [may be china and the former eastern block]
   
 19. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,725
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  "NO FREE LUNCH UNDER THE SUN".
  Wewe unalalamikia kulipia kodi ilihali kuna watu wanalipia upepo (maji hayatoki ila bili inakuja). Kuna watu wanaharibu miundo mbinu ya DAWASCO ili wauze maji kwa faida.
   
 20. Iron Lady

  Iron Lady JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 4, 2008
  Messages: 4,077
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  analipa sana indirect tax huyo ambayo mapato yake yanasaidia kupeleka pesa katika mizara na taasisi husika, nisichokubaliana naye ni kuwa tusilipe gharama za maji, kuchangia kunasaidia gharama za matengenezo na hata usambazwaji.
  isipokuwa serikali imekuwa na katabia kachafu ka kutumia kodi za wananchi kwa mambo yasiyo na msingi na ubadhilifu na kufanya watu wachukie uchangiaji gharama wa vitu mbalimbali pamoja na kuzilipa hizo kodi zenyewe. ingalikuwa kodi tunazolipa zinafanya kazi za maendeleo kisawasawa tungekuwa mbali. angalia miaka 50 ya uhuru,maazimisho ya siku ya mapinduzi, safari za mh. rais, na viongozi wengine wa serikali, sherehe za kiserikali ukiachilia mbali uchaguzi mkuu na chaguzi ndogondogo,utaona kodi kubwa ya watu inatumika kwa upuuuzi upuuzi na kufanya gharama ya huduma n yingi kuwa kubwa baada ya kuwa ndogo.
   
Loading...