TUJADILI: Hukumu kwa waliochoma Kituo cha Polisi Bunju A

Robot la Matope

JF-Expert Member
Apr 10, 2015
6,964
13,571
Huyu ni Khalfan Mshengeli akilia kwa uchungu mahakamani Kisutu leo baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha. Khalfan amezaliwa mwaka 2001. Mwaka 2015 alikua na umri wa miaka 14, akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Bunju A. Mwanafunzi mwenzao aligongwa na gari na kufariki. Khalfan na wenzie walitoka na kufunga barabara ya Bagamoyo. Leo amepatikana na hatia ya kushiriki kuchoma moto kituo cha polisi Bunju, na amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Ikumbukwe tangu mwaka 2015 yupo rumande. Ikiwa hukumu hii itabaki kama ilivyo basi Khalfan atakuwa ameishi uraiani miaka 14 tu, na atamalizia maisha yake yote gerezani.!

-----------

MTAZAMO asasena,

Wakuu,

Hii ni nchi yetu sote. Hebu tujadiliane ukweli na tatizo halisi juu ya sheria zetu. Inasemekana kati ya waliohukumiwa kifungo cha maisha ni mtoto aliyezaliwa mwaka 2001 ambaye alishiriki kufunga barabara baada ya mtoto mwenzake kugongwa na gari.

Inawezekana sheria zetu zina matatizo kuliko tunavyofikiria na tusisubiri siku yakukute wewe au mwanafamilia yako. Hivi kama mtoto kama huyu anaweza kuingia kwenye hatia kama hii ambayo kwa akili ya kawaida unaweza kujua alifikaje hapo nani yupo salama?

Kiukweli kuna sheria inawezekana zinahitaji kuangaliwa upya lakini wenye dhamana wakiwemo TLS wakizama kwenye political mileage kuliko shida zetu halisia ( najua wengi hampendi ukweli kama huu).

Namuomba Rais Magufuli ambaye binafsi nilimpigia kura sambamba na mbunge Halima Mdee waangalie hili kwa jicho la kulikomesha na si sifa za kisiasa za muda.

Kijana aliyefungwa maisha amenisikitisha mno lakini pia tusisahau rushwa na uzembe kwenye serikali zilizopita ambazo zilichangia wananchi kutafuta njia mbadala kutatua matatizo yao.

Mh Rais wetu Magufuli naomba uangalie hili ingawa halikuanza kwenye awamu yako lakini wasaidie hawa wahanga hasa huyo mtoto.

Huyu mtoto hastahili kuozea jela watanzania wenzangu! Anahitaji msaada.

FB_IMG_1550853865541.jpeg
 
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewahukumu kifungo cha maisha jela washtakiwa 8 baada ya kuwapata na hatia ya kuchoma moto kituo cha Polisi Bunju, Julai 10 mwaka 2015.

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Thomas Simba amesema kitendo walichofanya washitakiwa ni cha kinyama na hivyo amewahukumu kifungo cha maisha ili iwe fundisho kwa wengine.

#MyTake:
Sitaki kuingilia maamuzi ya mahakama lakini ningetaka kujua 'rationale' iliyotumika kuwahukumu watu hawa kifungo cha maisha gerezani.

July 10 mwaka 2015, mwanafunzi wa shule ya Msingi Bunju A aligongwa akivuka barabara na kufa papo hapo. Wenzie wakatoka madarasani na kwenda kujipanga eneo la ajali wakiomboleza. Barabara ya Bagamoyo ikafungwa kwa muda.

Polisi wakaja ili kuwatawanya watoto hao, lakini wananchi wakaingilia kati. Hoja ya wananchi ni kwamba eneo hilo wamegongwa watoto wengi na hakuna hatua zilizochukuliwa, kwahiyo watoto hao wana haki ya kufunga barabara.

Polisi hawakukubali. Wakatumia nguvu kuwatawanya watoto hao. Wananchi wakaingilia kati. Vurugu zikawa kubwa. Polisi wakafyatua risasi, na mabomu ya machozi. Lakini wakazidiwa nguvu na kundi kubwa la wananchi ambao walivamia kituo cha polisi na kukichoma moto kwa hasira.

Wakakamatwa watuhumiwa 35. Baada ya upelelezi 17 wakaacnchiwa huru. 18 wakaonekana wana kesi ya kujibu. Leo 8 wamehukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia.

Hoja yangu ni kwamba je adhabu waliyopewa inaendana na kosa walilofanya? Kwanini mahakama isingewapa adhabu ambayo ni humilivu? Atleast mwaka mmoja jela na faini ya kujenga kituo kingine badala ya kuwafunga maisha.

Tena kuwapiga fine ingekuwa 'win win situation' maana serikali ingepata pesa za kujenga kituo kingine cha kisasa zaidi, na pia washtakiwa wangerudi uraiani kuendelea na shughuli zao za kiuchumi ambazo serikali ingepata mapato kupitia kodi. Lakini kuwafunga maisha ni 'lose lose situation' maana pande zote zinapoteza. Serikali inapoteza gharama za wao kuishi gerezani kwa maisha yao yote. Pia familia zao zinageuka kuwa tegemezi bila sababu.

Ikumbukwe hawakufanya kosa hilo 'voluntarily' bali walikua kwenye 'tension' ya ajali iliyotokea. Nadhani walistahili sympathy ya 'temporary insanity' na kupewa adhabu humilivu, not a life sentence. Ni kweli wamefanya kosa lakini katika mazingira ambayo kulikuwa na 'provocation'. Hawakutoka tu nyumbani kwao na kujisikia kwenda kuchoma moto kituo cha polisi, bali kuna mazingira yaliwalazimisha kufanya hivyo.

Nimeambiwa wengi wa waliofungwa ni ndugu wa mtoto aliyegongwa. Just imagine. Yani mwanao anagongwa, anakufa. Unaenda eneo la tukio, polisi wanatumia risasi kuwatawanya. Mnashindana na polisi, mnawazidi nguvu na kuchoma kituo cha polisi. Leo unafungwa maisha. Yani umepoteza mtoto na wewe unaenda kumalizia maisha yako gerezani? Watoto wako wengine wanaishia kusema mdogo wetu aligongwa na gari, na baba alipoenda kumtizama akapata kesi akafungwa maisha. Hiki kidonda hakitakaa kipone milele.!

Huyu Hakimu alitakiwa kujiweka kwenye viatu vya watuhumiwa. Ajaribu kufikiria mwanae ndio kagongwa na gari na kufa. Halafu akaenda eneo la tukio anakutana na polisi wanapiga mabomu ya machozi, angefanya nini? A parent/relative can do anything linapokuja suala la mwanae/ndugu yake.

Hawa watu walikua wana haki ya kuomboleza, japo walifanya kosa lakini hawakustahili adhabu kali hivi. Cha msingi ni kujua kwamba hawakua katika hali ya kawaida wakati tukio hilo likitokea. So wangeweza kupewa adhabu ambayo ni humilivu, sio kufungwa maisha.!

Malisa GJ
 
Kama ni kweli aisee ...nimekosa la kusema
Huyu ni Khalfan Mshengeli akilia kwa uchungu mahakamani Kisutu leo baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha. Khalfan amezaliwa mwaka 2001. Mwaka 2015 alikua na umri wa miaka 14, akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Bunju A. Mwanafunzi mwenzao aligongwa na gari na kufariki. Khalfan na wenzie walitoka na kufunga barabara ya Bagamoyo. Leo amepatikana na hatia ya kushiriki kuchoma moto kituo cha polisi Bunju, na amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Ikumbukwe tangu mwaka 2015 yupo rumande. Ikiwa hukumu hii itabaki kama ilivyo basi Khalfan atakuwa ameishi uraiani miaka 14 tu, na atamalizia maisha yake yote gerezani.!View attachment 1029388

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watatoka wakienda CA! Najaribu kuona ushahidi ulkuwaje mpaka ukamuona Khalfani kuwa amechoma kituo katika umati mkubwa wa watu!
 
Hakimu ni kundi moja na Wilbard mashauri!
 
Kama kijana mdogo wa umri huo anaweza kupanga na kushiriki Uchomaji wa kituo cha polisi. Huyo ni hatari kwa jamii na Taifa kwa ujumla na sio MTU wa kawaida. Huyo anauwezo wa kuvamia kituo cha polisi, kupora siraha na kufanya uharifu.Hiyo hukumu ni haki kabisaa. Kama tukio lingefanyikia eneo LA ajali ya gari, tungeamini ni hasira na huzuni ya mwenzake kugongwa lakini kwenda hadi kituoni ni uhalifu uliokithiri
Huyu ni Khalfan Mshengeli akilia kwa uchungu mahakamani Kisutu leo baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha. Khalfan amezaliwa mwaka 2001. Mwaka 2015 alikua na umri wa miaka 14, akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Bunju A. Mwanafunzi mwenzao aligongwa na gari na kufariki. Khalfan na wenzie walitoka na kufunga barabara ya Bagamoyo. Leo amepatikana na hatia ya kushiriki kuchoma moto kituo cha polisi Bunju, na amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Ikumbukwe tangu mwaka 2015 yupo rumande. Ikiwa hukumu hii itabaki kama ilivyo basi Khalfan atakuwa ameishi uraiani miaka 14 tu, na atamalizia maisha yake yote gerezani.!View attachment 1029388
 
Serikali inafunga mpaka watoto ....

Ata kama alichoma kituo au hakuchoma hakuna sheria inayoruhusu kwamba mtoto akichoma kituo cha polisi afungwe maisha...

Huu ni ushahidi kwamba kuna kuingiliwa kwa uhuru wa mahakama na kuna udicteta nchini....

Sent using Jamii Forums mobile app
Wilbady mashauri kuwa jaji, tutegemee kesi Ya uchochezi mtu kuhukumiwa kunyongwa mpk kufa, manina tumekwisha walah, bora nabii Issa arudi
 
Acknowledgement
G. Malisa
Huyu ni Khalfan Mshengeli akilia kwa uchungu mahakamani Kisutu leo baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha. Khalfan amezaliwa mwaka 2001. Mwaka 2015 alikua na umri wa miaka 14, akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Bunju A. Mwanafunzi mwenzao aligongwa na gari na kufariki. Khalfan na wenzie walitoka na kufunga barabara ya Bagamoyo. Leo amepatikana na hatia ya kushiriki kuchoma moto kituo cha polisi Bunju, na amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Ikumbukwe tangu mwaka 2015 yupo rumande. Ikiwa hukumu hii itabaki kama ilivyo basi Khalfan atakuwa ameishi uraiani miaka 14 tu, na atamalizia maisha yake yote gerezani.!View attachment 1029388

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe wakati hilo tukio linatoea ulilishuhudia?
Ulikuwepo?
Na unaweza kuniambia ni nani alimgonga mwanafunzi mwenzao na alimgongaje hadi wananchi wakapandwa hasira na kushambulia kituo?
Nieleze ama kama hujui kaa kimya
Kama kijana mdogo wa umri huo anaweza kupanga na kushiriki Uchomaji wa kituo cha polisi. Huyo ni hatari kwa jamii na Taifa kwa ujumla na sio MTU wa kawaida. Huyo anauwezo wa kuvamia kituo cha polisi, kupora siraha na kufanya uhalisi.Hiyo hukumu ni haki kabisaa. Kama tukio lingefanyikia eneo LA ajali ya gari, tungeamini ni hasira na huzuni ya mwenzake kugongwa lakini kwenda hadi kituoni ni uhalifu uliokithiri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom