Robot la Matope
JF-Expert Member
- Apr 10, 2015
- 7,001
- 13,615
Huyu ni Khalfan Mshengeli akilia kwa uchungu mahakamani Kisutu leo baada ya kuhukumiwa kifungo cha maisha. Khalfan amezaliwa mwaka 2001. Mwaka 2015 alikua na umri wa miaka 14, akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi Bunju A. Mwanafunzi mwenzao aligongwa na gari na kufariki. Khalfan na wenzie walitoka na kufunga barabara ya Bagamoyo. Leo amepatikana na hatia ya kushiriki kuchoma moto kituo cha polisi Bunju, na amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani. Ikumbukwe tangu mwaka 2015 yupo rumande. Ikiwa hukumu hii itabaki kama ilivyo basi Khalfan atakuwa ameishi uraiani miaka 14 tu, na atamalizia maisha yake yote gerezani.!
-----------
MTAZAMO asasena,
Wakuu,
Hii ni nchi yetu sote. Hebu tujadiliane ukweli na tatizo halisi juu ya sheria zetu. Inasemekana kati ya waliohukumiwa kifungo cha maisha ni mtoto aliyezaliwa mwaka 2001 ambaye alishiriki kufunga barabara baada ya mtoto mwenzake kugongwa na gari.
Inawezekana sheria zetu zina matatizo kuliko tunavyofikiria na tusisubiri siku yakukute wewe au mwanafamilia yako. Hivi kama mtoto kama huyu anaweza kuingia kwenye hatia kama hii ambayo kwa akili ya kawaida unaweza kujua alifikaje hapo nani yupo salama?
Kiukweli kuna sheria inawezekana zinahitaji kuangaliwa upya lakini wenye dhamana wakiwemo TLS wakizama kwenye political mileage kuliko shida zetu halisia ( najua wengi hampendi ukweli kama huu).
Namuomba Rais Magufuli ambaye binafsi nilimpigia kura sambamba na mbunge Halima Mdee waangalie hili kwa jicho la kulikomesha na si sifa za kisiasa za muda.
Kijana aliyefungwa maisha amenisikitisha mno lakini pia tusisahau rushwa na uzembe kwenye serikali zilizopita ambazo zilichangia wananchi kutafuta njia mbadala kutatua matatizo yao.
Mh Rais wetu Magufuli naomba uangalie hili ingawa halikuanza kwenye awamu yako lakini wasaidie hawa wahanga hasa huyo mtoto.
Huyu mtoto hastahili kuozea jela watanzania wenzangu! Anahitaji msaada.