Tujadili hoja ya Mahanga kuhusu ukubwa wa serikali ya JPM

Hewa mkaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2012
742
377
Lakini kama ameona kwamba kuleta ufanisi serikalini lazima ajaze watendaji wengi kwenye wizara, kama anavyoendelea kufanya, aseme tu hivyo, lakini akijua hatua hiyo haitapunguza gharama za kuendesha serikali ambazo wabunge, hasa wa upinzani, wamekuwa wakipigia kelele kwenye serikali ya awamu ya nne.

Hata hivyo hili la kuleta ufanisi pamoja na kuteua makatibu wakuu wengi wanaoonekana wazuri kwa utendaji, kuna wizara ambazo hakushauriwa vizuri na akateua makatibu wakuu wale wale na kuwarudisha pale pale wakati walikuwa "mizigo" na walikwamisha mno sekta husika katika awamu ya nne. Hawa ni watu ambao rais au katibu mkuu kiongozi angeenda kwenye wizara zao leo na kuitisha kura ya siri ya wakurugenzi na wafanyakazi wote, asilimia 90 ya watumishi wote wangewakataa makatibu wakuu hao. Ni heri kukosea kuteua kwa mara ya kwanza kuliko kukosea kuteua "mizigo" iliyokuwepo.

Tukirudi kwenye hoja ya msingi ya gharama za kuendesha serikali, nimesema na ninarudia kusema: bila kutakiwa kutoa takwimu hapa, gharama za waziri mmoja na ofisi yake ni ndogo sana kulinganisha na gharama za katibu mkuu mmoja na ofisi yake, kwani waziri tayari analipwa sehemu kubwa ya mshahara na marupurupu kutokana na yeye kuwa mbunge (na hapa niwajuze baadhi ya walionipinga kwamba waziri halipwi mishahara miwili - ya ubunge na ya uwaziri).

Na hapa hatujajadili mikanganyiko mingine ambayo haijawekwa wazi hadi sasa. Kwa mfano kutakuwa na afisa masuhuli mmoja wa wizara au maafisa masuhuli wawili au watatu kwenye baadhi ya wizara? Kwa kawaida wizara inakuwa na fungu (vote) moja; sasa katika hali hii kila idara ya wizara itakuwa na fungu (vote) tatu (ukiacha idara zinazojitegemea)? Je hili la afisa masuhuli mkuu wa wizara kutokuwepo haitaleta shida katika uwajibikaji? Na vipi katika kusimamiwa na bunge na kamati zake? Nani hasa mtendaji mkuu wa wizara atakayewajibika kwa bunge kwa mambo ya kisera ya wizara nzima? Wote watatu?
 
yaani mmesahau kile kipindi cha kasi mpya ari mpya kilidumu kwa muda gani.
 
Kuna hoja za msingi ambazo majibu yake yanatakiwa mapema. Watu kama Ole Sendeka walipaswa kutoa majibu katika mlengo huu wa kuwekana sawa badala ya kuona kila mwenye hoja kinyume chao ana makusudi mabaya.
 
Naomba mtoa mada ufafanue ukubwa kwenye hoja hii una maana gani?

Majukumu ya waziri ni zaidi ya mbunge, yeye anatumikia taifa zima na huwa na safari nyingi zenye posho.

Napata shida kuamini kwamba mawaziri 21 kupungua hakujapunguza gharama kwasababu tu makatibu waliopungua ni watano.

Tukumbuke makatibu ni wengi lakini hawajaongezeka bali wamepungua kulinganisha na awamu ya nne.
 
Back
Top Bottom