Tujadili hili! Ni ipi nafasi ya vijana?


K

kibebii

Member
Joined
Nov 5, 2009
Messages
80
Likes
1
Points
15
K

kibebii

Member
Joined Nov 5, 2009
80 1 15
Habari wana JF,

Niwape hongole wale waloshinda katika uchaguzi na niwape pole walioshindwa kwa sababu zozote zile.

Pamoja na matokeo na idadi ya kura zilizotangwazwa, nimepata mshtuko mkubwa sana niliposikia kuwa vijana wachache sana waliojitokeza katika zoezi la kupiga kura. Nasema nimesikia kwa sababu mimi si mkazi wa Igunga ila napokea taarifa kupitia vyombo vya habari. Napata maswali mengi mno kuhusiana na mustakbali au mwelekeo wa jamii yetu na nchi kwa ujumla kama vijana wetu hawatakuwa na ari ya kushiriki katika mambo muhimu yanayoathiriri maisha yao na maisha ya vizazi vyao. napata shida pia katika kuangalia mwelekeo wa vyama vya siasa, kama waliweza kuwashawishi halaiki ya watu kwenda kwenye mikutano yao walishindwaje kuweka mikakati ya kuhakikisha vijana wanapiga kura? nasema hivi kwa sababu naamini pamoja na wajibu wa vyombo vingine vyama vya siasa navyo vina wajibu mkubwa wa kuhakikisha vijana wanashiriki na wanakuwa mstari wa mbele kuwakumbusha wazee wao na hata kuwashika mkono kuwasindikiza kupiga kura.

Kilichoonekana kupitia vyombo mbalimbali ni wazee tena wengi wao hawajui kusoma na kuandika na wengine hawajui kiswahili hao ndio wanajua umuhimu wa kwenda kupiga kura na sio VIJANA!!!!, KULIKONI?
 

Forum statistics

Threads 1,236,702
Members 475,218
Posts 29,267,045