kibogo
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 9,739
- 4,732
Wana JF wenzangu.
Tumemuona na kumsikia Mgombea wa CCM Dr. John Pombe Magufuli akitoa ahadi ya Elimu Bure kuanzia Chekechea hadi kidato cha nne yaani form four, nimejitahidi kutafakari sana na nimeishia na hitimisho kuwa ahadi hii ni ya kutuadaa Watanzania kwani kiuhalisia gharama halisi za elimu kwa mtanzania ni zile za elimu ya juu yaani vyuo vikuu.
kwani tumeshuhudia karibu kila kata hapa nchini ina shule ya sekondari na watoto wanasoma na kumaliza kidato cha nne bila shida kwani gharama ni ndogo na wazazi wengi wanazimudu lakini tatizo uanzia pale mtoto anapofaulu kwenda kidato cha tano kwani bado tuna shule chache za High level hivyo gharama uongezeka kama vile nauli na matumizi mengineyo hivyo baadhi ya wazazi ushindwa kuwapeleka watoto wao kuendelea na masomo na kwa wale ambao uweza kuwapeleka na kwa bahati nzuri wakafaulu kuingia vyuo vikuu hapo ndipo hasa gharama halisi za elimu uonekana kwani gharama huwa si chini ya Tsh.million 4 hivyo kwa wale wasio na uwezo ndio maisha uanza kuharibikia hapo na isitoshe mikopo wengi wao hukosa.
Kwa hiyo nahitimisha kwa kusema kuwa hii ahadi ya elimu bure ya CCM na Magufuli ni changa la macho kwani haitakuwa na msaada wa kumsaidia mtanzania kwani gharama halisi za elimu zipo kwenye vyuo vikuu.