Tuition za siri za Tshs 100,000 kwa mwezi st matthews! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tuition za siri za Tshs 100,000 kwa mwezi st matthews!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kimweri, Jul 30, 2009.

 1. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Nina ndugu hapo st.mathews,A level.ameniacha hoi aliponieleza kuwa St.Mathews wanafunzi wanalazimika kulipia laki moja kwa mwezi kwa somo kwa walimu wao(kwa siri shule haijui-kweli??).
  waalimu darasani wanategea hawafundishi vizuri wakijua kuwa mzazi hana jinsi atatoa tu hiyo laki moja ili mtoto wake apate elimu nzuri.

  najiuliza maswali yafuatayo.
  1.Uongozi wa St.Mathews Kongowe Unalifahamu hili?
  2.Kama unalifahamu je ni sahihi?Ada ya nini sasa?wazazi wasio na uwezo wa kutoa hizo laki moja za ziada kwa mwezi watoto wao watafaulu vipi?
  3.kwa nini wazazi hawauambii uongozi wa shule?(nategemea kufanya hivyo)
  4.kuna mzazi aliyewahi ripoti tuition hizi za kifisadi kwa uongozi wa shule?alipewa majibu gani?
  5.kwa mlio na vijana mashule mengine,utaratibu mzima wa Ada vs Tuition ukoje?

  hitimisho:
  nionavyo mie,ufisadi uko sehemu nyingi tu tanzania,kuanzia IKULU hadi chekechea.
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  tution ya nini wakati mitihani inavuja na inamwagwa online?

  baraza la mitihani kama vile wameshindwa ku catch up na dunia ya leo

  kuhusus St Mathew..well hizo tution zitahamishwa tuu nje ya shule sijui watu watalalamika wapi
   
 3. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  advantage ya hizi tuition hutokea wakati wa mitihani ya ndani ya ndani ya shule tu.edge wanayopata wasomaji huyeyuka kwenye necta etc,wote wanakuwa on same level.

  problem is:most uninformed parents have no alternative,and competition is very high so is pressure.

  hii St.Matthews ni boarding school na hii tuition ni kwa wale wanafunzi wa boarding A-Level.
  kwa rate hiyo ya laki moja,miezi 10 ni 1 million wakati ada yao ni 1.7M kwa mwaka.
  3rd party tuition is OK,and very helpful,as tuition teachers don't have a hand in influencing the situation at respective schools
   
 4. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #4
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  St mathews ni shule inayomilikiwa na mbabaishaji aliyewahi kuwa jambazi. Shule hii imewahi kufutiwa mitihani yake ya taifa mwaka 2006.

  Mwenye shule ambaye ni mwenyeji wa bukoba aliwahi kuwa mkuu wa kituo cha polisi buguruni akawa anakodisha silaha kwa majambazi.akatimuliwa kazi ghafla akawa milionea.na sasa ni mlezi wa ccm wilaya ya mkuranga na mweka hazina.
   
 5. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #5
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hii sio habari ya kisiasa.

  Kama unachukizwa si uwatoe tu huko?, shule ni kama maduka zimejaa tele!!!
   
 6. C

  Chuma JF-Expert Member

  #6
  Jul 30, 2009
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  that's not fair....!!!
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  na hao wazazi wanalipa hizo laki moja kila mwezi? halafu tunalia sisi ni maskini? somebody got some money somewhere!
   
 8. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #8
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Jina lako ni FAIR PLAYER nilitegemea ungesema kuwe na FAIR TRADE.shule ni biashara siku hizi hivyo mteja ana haki zake zinatakiwa kulindwa.

  mtu akisema Nchi yetu imevamiwa na ufisadi, jibu ni kuwa kuna nchi nyingi nenda kaishi Botswana?

  au mtu akisema shirika la Ndege la Air Tanzania lina mapungufu kadhaa kwenye huduma yao, jibu mashirika yako mengi panda Precision Air.
  akija mdau Mwingine akisema kampuni fulani ya simu ina gharama kubwa sitarajii jibu liwe kuwa makampuni yako Mengi.

  aliyeleta mada hii hapa anazungumzia wizi kama ilivyo EPA au Richmond inayojadiliwa hapa kwenye siasa.

  huko chini wewe umemjadili mama Rwakatare na kanisa lake na ukathibitisha utapeli wake wa kuchukua pesa za Yatima na wajane kutoka kwa wamarekani, hakuna aliyekuelekeza kuwa makanisa yako Mengi nenda kwa Kakobe.

  mkuu labda una hisa au ujamaa na Mmiliki wa shule ile ambaye ni tapeli na jambazi wa muda mrefu.mwaka 2005 aligombea ubunge kwa jimbo la Mkuranga,jina lake lilipofika CC wakahoji jamani CCM tumeishiwa kiasi cha kuchukua majambazi kama haya. hayo ni maneno ya Rais Mkapa aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM kwa wakati huo.jamaa akatupwa chini.

  hivi sasa amesema atajenga ofisi ya chama wilaya Ya Mkuranga ya dhamani ya milioni mia moja. wakati vyanzo vyake ni ujambazi wa silaha na wizi huu wa ada za wanafunzi. kibaya zaidi anatumi majina ya dini kama kuita shule MTAKATIFU MATHEWS.
   
  Last edited: Jul 30, 2009
 9. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #9
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  MKUU LAKI moja unashangaa wengine wanalipa dola elfu kadhaa.
   
 10. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #10
  Jul 30, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  Kwanini wazazi wanapeleka watoto wao kwenye shule yenye sifa za namna hiyo? Ni kwa sababu ya uhaba wa shule nyingine? ni kwa sababu ya ubora wa elimu, ukaribu, unafuu?
   
 11. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #11
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  KUNA SHULE HASA KWA MAANA YA ST. MFANO MARIAN GIRLS AU ST.FRANCIS IKO MBEYA,ST.ANTHONY N.K hizi ni kweli shule za kanisa na zinafuata maadili ya elimu huwezi kusikia kitu kama hicho.sasa kuna uyoga wa shule za watu binafsi zinatumia majina hayo kuwalaghai wazazi hapo ndio unakutana na shule kama ST.MATHEWS, ST MARYS n.k

  watanzania wengi sio wadadisi kama wewe Mwanakijiji au mimi.Mzazi akiona ST anajua ndio zile zile original.

  Mkuu Mwanakijiji wabunge wetu makini itakuwa na Mfanyabiashara wa mbao akajua shule hii ni ST. original au kanjanja.kuna watu wanalipa kwenye shule ambazo hazijasajiliwa na wizara.
   
 12. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #12
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  Wazazi wengi Tanzania wako desperate!gharama Za kila kitu zipo juu.hadi elimu.kwa mfanyakazi wa kawaida wa serikali hapo option itakuwa ni kupokea rushwa tu!au kutafuta semina,trip na vibonasi vya kufosi kujazia mshahara kiduchu.
  Hizo St. Za ukweli ni Kazi kwelikweli kupata!yani hata kwa kijana aliyepata division one O-Level inabidi ashindane na wenzie maelfu kugombea tena nafasi 40-50 Za hizo st.Za ukweli,matokeo yake ni hizi St.Mafisadi zinapata nafasi hake hapo.kwani mzazi anakuwa cornered na gov schools ukitoa zile chache bora zilizobaki ni mitego tu.waalimu hakuna(wanakimbilia part-time Za st.fisadi).
  Hili ni tatizo la kimsingi sasa hivi Tanzania,system nzima ya elimu imeharibiwa na wachache,matokeo hasara kwa mzazi.na mzazi gharama anahamishia kwenye rushwa popote alipo,iwe hospitali,TRA au polisi.
   
 13. M

  Mama Joe JF-Expert Member

  #13
  Jul 31, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,507
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
   
 14. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #14
  Jul 31, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Jamani huyo mwalimu haoni aibu... wazazi tunajinyima ili wanetu wsome wawe na maisha bora baadae maana huo ndio urithi pekee ambao atadumu nao maishani sasa huyu mwalimu anaye fisadi kiasi hicki haoni aibu au anagawana na mwalimu mkuu ndio maana mwalimu mkuu hawajibiki ipasavyo ni heri angefanya shs 500 kwa siku kwa mwezi ni shs1500 na kama ni mzuri akiwa na wanafunzi 40 uwongo mwisho wa mwezi ana laki zake 6 sas hii ya laki moja kwa mwezi na nisomo moja hii kweli ni kiboko.

  Halafu wanalalamika walimu wanahali ngumu kweli kwa mtajii huu utalalamika unahali ngumu kimaisha!!!!
   
 15. BornTown

  BornTown JF-Expert Member

  #15
  Jul 31, 2009
  Joined: May 7, 2008
  Messages: 1,716
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Wizara ya Elimu sijui inasemaje kuhusiana na walimu walafi wapesa kam hawa... maana wanakwenda kinyume na maadaili ya kazi. Mwalimu wa jinsi hii hatofundisha darasani ipasavyo anajua lazima wanafunzi watakuja tution tu. Walimu wa jinsi hii wawajibishwe ili kusafisha wale waovu na tubakiwe na waadilifu wa taaluma zao.

  Ukute hawa ni wale waalimu wa kupeana kiujombaujomba tu.
  Naomba jina la huyo mwalimu liwekwe adharani ili ashughulikiwe ipasavyo.

  Mbona kipindi cha nyuma wakati tunasoma enzi za Mwalimu Ndosi - hisabati, Mkichwa - fizikia hawakuwa na taamaa na walikuwa wanafundisha vizuri tu madarasani na hata tution zao hazikuwa za garama kiasi hicho
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kanda2
  Je ulikuwapo katika kikao hicho?

  Kwa hili inawezekana maana ni mkeleketwa sana wa chama cha kijani. Aliwahi hata kuwapa pikipiki makatibu tarafa/kata wote mkuranga

  Hapa ni kweli kwamba ni mwenyeji wa Bukoba na ni kweli aliwahi kuwa askari polisi, ambako alijiunga alipomaliza BA education pale UDSM. Lakini la ujambazi una hakika?
  Unamfahamu vizuri na unaweza kuliambia jukwaa ukweli halisi kuhusu huyu bwana? maana inaelekea unachanganya uongo na ukweli ili vyote vionekane kama kitu kimoja
   
 17. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #17
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  waalimu hawa wanaofanya tuition hawafundishi vizuri darasani!wanabania baadhi ya vitu vya msingi ili wale wasiosoma wajione mazoba kwenye mitihani.kwa akili ndogo ya kijana wa form 5 or 6,mwalimu huyu anawalaghai.

  tatizo ni kuwa shule hii ya St.Matthews ada ni kubwa vya kutosha tu! 1.7M,bado gharama zingine ndogo ndogo.

  sasa hawa waalimu ni muda muafakwa waache kuandamana na kuwalaghai watanzania kuwa hali zao ni ngumu kwani ni matajiri vya kutosha.

  I used to feel sympathy for teachers as ones who were on the lower end of the pyramid.BUT kwa mwenendo huu,not so much.

  ndio maana mishahara yao ya laki na nusu hawailalamikii.kumbe wana bigger sources of income.

  swali la kujiuliza watanzania,what happens when this gets out of control?!when this scammers controls our education system?
  what is left for a a civil servant who genuinely depends on TZ salary scale?
   
 18. K

  Kimweri JF-Expert Member

  #18
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 16, 2008
  Messages: 3,998
  Likes Received: 1,083
  Trophy Points: 280
  ndio tanzania yetu."kila mtu anakaba namba yake".ni msemo niliousikia toka kwa kiongozi mmoja aliyeniomba nimsaidie kutafuta Risiti za kufoji za hotelin huku ughaibunii-nilikataa maaana nisingeweza(alijua yuko TZ,kila kitu tambarare).

  asilimia kubwa ya wafanyakazi ni either mwizi,au mpokea rushwa.wakienda semina wana-inflate kila kitu,kuanzia gharama za hoteli hadi risiti feki za vitu ambavyo hawakufanya au kununua.System yetu is a complete joke.

  chukua mfano huu
  "afisa wa mikopo benki anaomba rushwa ili atoe mkopo kwa mwalimu anayeuhitaji,mwalimu anatoa,akifika kwenye eneo lake,anamtoza ada ya tuition mtoto wa banker,na polisi tuition laki moja kwa mwezi,polisi hana anaenda kusimama barabarani,anapiga bao madreva wa daladala,na waendesha motokaa kama wa-3 hivi,mmoja wao ni mhasibu.mhasibu naye kwenye eneo lake anaendeleza wembe huohuo."

  it is a circle,a dirty circle of life that is going on in Tanzania.that answers your question hela zinatoka wapi!

  Tatizo ya pesa za aina hii,watanzania Hatuna Confidence(maana hizi fedha ni za ujanja ujanja tu),na hatuna maendeleo wala plani.mtu ana-mshahara wa laki tano,Rushwa zinamuingizia milioni 2 kwa mwezi!

  wafanyabiashara wanalijua hilo!ndio maana kila kitu bei ghali,ukiona nyumba inauzwa millioni 200 una-conclude ni very few CEO's wanaoweza ku-afford that kind of a house!while the truth is almost any CIVIL SERVANT who knows his way around posta can afford a 200 million house.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Jul 31, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  100,000 per month !!??????? sh*********,je ada ni shilingi ngapi?
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Jul 31, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  1.7mil kwa mwaka:eek: tena nafasi zinagombaniwa.
  Wadanganyika ndivyo tulivyo. Mwaka kesho utasikia ni 2m na watu kimya.
   
Loading...