Tuitafakari kauli hii katika mazingira ya Kisiasa Tanzania

IsangulaKG

JF-Expert Member
Oct 14, 2010
706
385
Mojawapo ya jambo ambalo limekuwa likizungumzwa katika wakati wote wa Msiba wa Mandela ni muono kwamba, Mandela alitambua kuwa uhuru wa watu wa Africa Kusini hautapatikana kwa njia za kisiasa pekee katika mazingira ya serikali ya kidhalimu, hivyo akalazimika kuangalia njia mbadala ikiwa ni pamoja na chama chake kuanzisha jeshi na yeye kupita nchi tofauti ambako alitafuta uungwaji mkono pamoja na kupata mafunzo ya kijeshi. Suala hili aidha 'limepotezewa' baada ya kuzungumzwa au limezungimzwa kinafiki.

Tafakari hapa ni kwamba katika mazingira ya Tanzania chini ya uongozi wa CCM, itawezekana kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kura pekee au kuna njia mbadala zinahitajika? Najua wavivu wa kufikiri watakuja na negativity zao but tunaposema 'njia mbadala' si lazima vita!
Nawasilisha!
 
Last edited by a moderator:
hapo mvivu wa kufikiria ni wewe mkuu,what is democracy?njia mbadala ni ipi kama sio vita?
 
CCM ni walaini kama ice cream... kwa "kulambwa" tu wataisha, haina haja ya uma. Kwa kura CCM wataondoka.
 
Tupiganie Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba inayotokana na Wanainchi wenyewe na si Vyama vya Siasa hapo tutaweza kuiondoa CCM kwa njia ya KUPIGA KURA TU.
Zaidi ya hapo mbadala utakuwa ni VITA jambo ambalo siliafiki na tuombe Mungu tusifike huko.
 
Njia mbadala ni kuwaacha waendelee kutawala ama sivyo kwa heri au kwa shari ni kitu kimoja, they have to go.
 
mojawapo ya jambo ambalo limekuwa likizungumzwa katika wakati wote wa msiba wa mandela ni muono kwamba, mandela alitambua kuwa uhuru wa watu wa africa kusini hautapatikana kwa njia za kisiasa pekee katika mazingira ya serikali ya kidhalimu, hivyo akalazimika kuangalia njia mbadala ikiwa ni pamoja na chama chake kuanzisha jeshi na yeye kupita nchi tofauti ambako alitafuta uungwaji mkono pamoja na kupata mafunzo ya kijeshi. Suala hili aidha 'limepotezewa' baada ya kuzungumzwa au limezungimzwa kinafiki.

Tafakari hapa ni kwamba katika mazingira ya tanzania chini ya uongozi wa ccm, itawezekana kuiondoa ccm madarakani kwa njia za kura pekee au kuna njia mbadala zinahitajika? Najua wavivu wa kufikiri watakuja na negativity zao but tunaposema 'njia mbadala' si lazima vita!
Nawasilisha!

hapana mkuu bado tunaweza kutumia sanduku la kura kuwaondoa kikubwa hapa ni kuendelea kutoa elimu ya uraia kwa wananchi wetu
 
Mojawapo ya jambo ambalo limekuwa likizungumzwa katika wakati wote wa Msiba wa Mandela ni muono kwamba, Mandela alitambua kuwa uhuru wa watu wa Africa Kusini hautapatikana kwa njia za kisiasa pekee katika mazingira ya serikali ya kidhalimu, hivyo akalazimika kuangalia njia mbadala ikiwa ni pamoja na chama chake kuanzisha jeshi na yeye kupita nchi tofauti ambako alitafuta uungwaji mkono pamoja na kupata mafunzo ya kijeshi. Suala hili aidha 'limepotezewa' baada ya kuzungumzwa au limezungimzwa kinafiki.

Tafakari hapa ni kwamba katika mazingira ya Tanzania chini ya uongozi wa CCM, itawezekana kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kura pekee au kuna njia mbadala zinahitajika? Najua wavivu wa kufikiri watakuja na negativity zao but tunaposema 'njia mbadala' si lazima vita!
Nawasilisha!

Mkuu yawezekana uko Sahihi kabisa, lakini Je hapa kwetu ni nani anaestahili kusimama na kuhakikisha nchi inakwenda vizuri? Je hao watakaokuja watakuwa na Moyo wa Utaifa kuliko waliopo au ni Sera tu wanazozitumia kutudanganya tuungane nao na wakiingia hali itakuwa ileile. Nimesema hivyo kwa sababu kuna wagombea wenye madudu kabla hata hawajaingia madarakani. Je wakiingia si tutasema bora aliyepita? Mgonjwa anayekufa kwa Malaria Leo huwa anatamani angekuwa mgonjwa atakaekufa kwa UKIMWI mwezi ujao kwa kuupenda uhai, lakini je Yupi anataabika zaidi?
 
Tafakari hapa ni kwamba katika mazingira ya Tanzania chini ya uongozi wa CCM, itawezekana kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kura pekee au kuna njia mbadala zinahitajika? Najua wavivu wa kufikiri watakuja na negativity zao but tunaposema 'njia mbadala' si lazima vita!
Nawasilisha!
Hapa Tanzania ni tofauti, sidhani CCM wanahitajika kuondoka kwa mbinu za ziada yaani zile za Medani au zinazofanana na hizo, No.

As of now CCM tayari wameshalainika kabisa; kilichobakia tu ni kuendeleza elimu ya uraia zaidi hasa kwa wananchi wa vijijini ambao hununuliwa kwa pilau, furana na siketi za CCM wakati wa uchaguzi.

Mtazamo wangu ni kwamba hawa wataondoka kwa njia ya kura tu - sasa tatizo endapo WAKIGOMA kutoka madarakani - hilo sasa ni jambo jingine na hatutaki tufikie huko.

Kwa hiyo mleta maada usiwe na wasiwawasi kwani uchaguzi wa 2010 CCM waliondolewa madarakani kwenye miji mikubwa mingi tu kwa zaidi ya 75% - sasa tunaongelea 2015 ni balaa.
 
Back
Top Bottom