IsangulaKG
JF-Expert Member
- Oct 14, 2010
- 706
- 386
Mojawapo ya jambo ambalo limekuwa likizungumzwa katika wakati wote wa Msiba wa Mandela ni muono kwamba, Mandela alitambua kuwa uhuru wa watu wa Africa Kusini hautapatikana kwa njia za kisiasa pekee katika mazingira ya serikali ya kidhalimu, hivyo akalazimika kuangalia njia mbadala ikiwa ni pamoja na chama chake kuanzisha jeshi na yeye kupita nchi tofauti ambako alitafuta uungwaji mkono pamoja na kupata mafunzo ya kijeshi. Suala hili aidha 'limepotezewa' baada ya kuzungumzwa au limezungimzwa kinafiki.
Tafakari hapa ni kwamba katika mazingira ya Tanzania chini ya uongozi wa CCM, itawezekana kuiondoa CCM madarakani kwa njia za kura pekee au kuna njia mbadala zinahitajika? Najua wavivu wa kufikiri watakuja na negativity zao but tunaposema 'njia mbadala' si lazima vita!
Nawasilisha!

Last edited by a moderator: