Tuishitaki Serikali Kwa Kuhujumu Uchumi

Ibrah

JF-Expert Member
Mar 22, 2007
2,729
528
Hivi haiwezekani kufungua kesi dhidi ya Serikali kwa kuhujumu uchumi! Serikali hivi karibu ilikaririwa ikisema kuwa Mkataba wa Buzwagigate una maslahi kwa nchi. Kuvuja kwa mkataba huo kumetuonyesha kuwa hakuna maslahi ya nchi bali ni uhujumu mkubwa wa nchi na Watanzania kwa ujumla (Isipokuwa watawala).

Napenda kutoa changamoto kwa Vyama vya siasa, Vyama vya Hiyari na Wanasheria wenye uchungu uchungu na nchi yetu kutafiti na kuangalia vipengere vya kisheria vinavyowezesha kuifikisha Serikali ymahakamani kwa kuhujumu uchumi.

Naamini hapa JF kuna Wanasheria; Je, hakuna uwezekano wa kuishitaki Serikali kwa kuhujumu uchumi kwa kuzingatia huu mkataba wa Buzwagigate wenye “maslahi” kwa nchi yetu? Tusikubali ng’mbe wetu aliykonda akamuliwe maziwa, nachelea kuwa tukiendelea kufumba macho mwishowe atakufa!
 
Great idea Ibrah! Eti ndugu zangu lets see how we can do what Ibra suggests. Nashauri team pia iwe na akina Tundu Lissu et al.
 
Ibra
Are you serious? Kuishitaki serikali ya Tanzania kwenye mahakama ya TAnzania. Do you think we are in US or UK? Hii haiwezekani labda kama tungekuwa na priviledges za privy council tungejaribu lakini walioamua tuwe jamhuri walikuwa hawataki kitu kama hicho. Umeona mfano wazi kabisa wakatinwa kesi ya Dito. Aliua frist degree lakini sasa hivi anatanua tu anauza asali, huyo ni Dito tu, sasa wewe unazungumzia serikali. I think this is wastage of thoughts it is better if we think of other option of dealing with this government hiyo sahau. Mara ngapi mahakama imetoa hukumu dhidi ya serikali na haikutekelezwa. Kwa hiyo itakuwa ni kama mchezo ule ule.
 
Ibra, bongolader etal..,
Najua ni vigumu kuishitaki jamuhuri, mie mawazo yangu yalikuwa hivi:

-Kuanzisha harakati za kufanya maandamano kila kona ya nchi kupinga mikataba ya kinyonyaji na kuishinikiza serikali ivunje mikataba hiyo mara moja hasa hii ambayo haija anza kufanya kazi wa Buzwagi aka 'Kabwe Mine' Na huu wa kiwira.

-Hayo maandammano yahusishe wadau wote, wafanyakai wana harakati taasisi za dini kama walivyo kwisha anza toa matamko yao n.k

Yaani kwa kifupi yaonyeshe taswira ya wananchi wote kupinga uhujumu uchumi unao fanywa na serikali kwa raslimali zetu.

Hii mwaionaje?
 
Ibra
Are you serious? Kuishitaki serikali ya Tanzania kwenye mahakama ya TAnzania. Do you think we are in US or UK? Hii haiwezekani labda kama tungekuwa na priviledges za privy council tungejaribu lakini walioamua tuwe jamhuri walikuwa hawataki kitu kama hicho. Umeona mfano wazi kabisa wakatinwa kesi ya Dito. Aliua frist degree lakini sasa hivi anatanua tu anauza asali, huyo ni Dito tu, sasa wewe unazungumzia serikali. I think this is wastage of thoughts it is better if we think of other option of dealing with this government hiyo sahau. Mara ngapi mahakama imetoa hukumu dhidi ya serikali na haikutekelezwa. Kwa hiyo itakuwa ni kama mchezo ule ule.

Don't worry Bongo; its just a beginning remember the end shall not come without the beginning. Tujaribu bwana ili Watawala wajue na dunia ijue kuwa WTZ tumechoka; tunaweza kubadilisha historia ya nchi hii. Zamani nania alijua kuwa serikali inaweza kushitakiwa na kushindwa mahakamani? Mtikila alipoishitaki serikali kuhusu mgombea binafis Jaji Lugakingira alimpa ushindi, nani alitarajia kuwa ingekuwa hivyo? Demokasia ya kweli haiji hivi hivi, ina gharama kubwa na huwezi kujua Jaji ana uchungu gani na nchi hii.

Nani alitegemea kuwa Mkataba wa Buzwagi ungevuja na kusambazwa mitaani kama njugu? Jiulize nani aliyeuvujisha na aliupataje? Wananchi leo hawaelewa chochote Mawaziri wanazunguka wakiutetea Mkataba wa Buzwagi wanazomewa! Vivyo Hivyo; Mahakama ikishindwa kutoa hukumu ya haki nayo TUTAIZOMEA! Ujumbe utakuwa umefika na itakuwa ni somo kubwa; usijeshangaa kusikia hata Jaji wa hiyo Kesi akenda kusomea hukumu Uingereza kuwa serikali imehujumu uchumi! Si unamkumbuka yule kamanda wa kupambana na ufisadi Kenya? Alienda kuwataja mafisadi Uingereza kwa usalama wa maisha yake.
 
kuwazomea haitoshi,kuwakataa kabisa na mapambano yanatakiwa yaanze katika uchaguzi unaokuja wa madiwani..wakose viti vyote
 
Nguvu ya Umma ndio suluhisho, hakuna cha kwenda mahakamani kupoteza mda, mtandao una-influence kubwa sana kwenye mahakama, cha msingi ni maandamano, television na radio zitumike kuwapasha watu ukweli halisi, wananchi wafaham kwamba maisha waliyonayo si waliyopangiwa na Mungu ila wananyonywa na watu wachache, pia wafanyakazi wa Dar wanaotaka kukatwa mishahara yao wafahamishwe kuwa pesa watazotumia mawaziri kwenda kupiga porojo nchi nzima zinaweza jenga kiasi kikubwa cha madarasa hayo yanayosemwa, Waziri kama ghasia atasema nini mbele ya wananchi,

Time has come for people to change,
 
I think we should use Mkono & Mkono International lawyers (FISADI LAWYERS) to sue the Government. They will be cleaned properly..............Teh TEH TEH...........................
 
I think we should use Mkono & Mkono International lawyers (FISADI LAWYERS) to sue the Government. They will be cleaned properly..............Teh TEH TEH...........................

Nimeghadhabika wakuu nisameheni,

Kuna sehemu nimeona hata sikumbuki jamaa kazungumzia nyenzo moja ambayo nadhani ni nzuri sana,

Ile ya kutumia spray nyekundu kuandika neno FISADI kwa magari ya hao mafisadi, Yaani ikifanyika move kama hiyo.. mtu kaegesha gari sehemu akija rudi akute neno kuuuubwa fisadi, hasa hasa watu kama Kara...

Nadhani itasaidia kuwatia pressure wakose amani ya kutanulia hizo peremende walizo hongwa kwa kuhujumu raslimali zetu!
 
Jamani, naomba tuwe "serious" khs hili. Naomba huu mjadala uendelee, ikiwezekana usisitishwe. Tufanye zaidi ya haya tuyafanyayo ili tutimize wajibu wetu kwa manufaa ya Taifa, sasa na kwa vizazi vijavyo.
Swali: Tufanyeje zaidi ili sauti ya umma iwe na nguvu?
 
Tuendelee kwanza kuamsha ari ya watanzania kwanza ,ili hata kama tukifungua kesi wawe tayari wako na maelezo ya kutosha juu ya huu ufisadi na madhara yake kwao binafsi.
 
Tuendelee kwanza kuamsha ari ya watanzania kwanza ,ili hata kama tukifungua kesi wawe tayari wako na maelezo ya kutosha juu ya huu ufisadi na madhara yake kwao binafsi.
Sawa kabisa,ila hilo la kesi ni possible?I mean mashtaka vs serikali mahakamani kwamba ijiuzulu?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom