Tuisaidie jamii iache tabia ya kulaumu na kutowajibika

Masanja

JF-Expert Member
Aug 1, 2007
4,210
2,000
Wakuu,

Hebu leo tuwache makinikia na story za Lowassa pembeni tujadili kitu tofauti.

Mimi kuna hili jambo linanitatiza sana kwetu sisi Waafrica na Watanzania haswa. Tabia ya kupenda kulaumu watu wengine kwa makosa au mapungufu yetu wenyewe. Imekuwa ni tabia sugu. Ni nadra sana ukute Mtanzania anachukua kile wazungu wanaita personal responsibility for his or her mistakes. Ni kwanini?

Mfano, hata nyumbani baba akishindwa kutimiza wajibu wake kama mume au mzazi lazima ana mtu wa kumsingizia. Rafiki au ndugu ukimpa mtaji wa biashara akashindwa, ana mtu wa kumsingizia kwa kushindwa kwake (hata kama unajua kabisa mtaji alihonga au alikunywa Pombe!). Mtoto akifeli mtihani hata kama kila kitu alikuwa nacho lazima ana mtu wa kumrushia mpira.

Kijana akisoma mpaka chuo kikuu akakosa kazi anakuwa na mtu tayari wa kumrushia mpira (in most cases serikali). Tabia hii imeenea mpaka kwa viongozi wetu wakubwa nchini kama wakurugenzi, mawaziri nk. Mtu/kiongozi akila rushwa/kaiba hela za umma au akaharibu akipelekwa mahakamni ni witch-hunt na kisasi (hatasema kwamba kweli niliiba!), Hata mtu akipewa uRais. Akishindwa ku-deliver ana kitu cha kusingizia (most cases wanasema mfumo a.k.a system!). Tatizo ni nini? Kwanini ni Watanzania wachache sana wanaweza ku-admit kwamba wameshindwa na ni makosa yao?

Kipi kifanyike? Kwa nini ukishindwa au ukaharibu sehemu iwe kazini, ndoa, shuleni nk usisimame u-take personal responsibility? Useme nimekosea. Uombe msamaha (au uadhibiwe) maisha yaendelee? Yaani tumefika sehemu tumekuwa kizazi cha ulalamishi na uongo kwa kuona kwamba maisha yetu ni jukumu la watu wengine (serikali, wazazi au ndugu wenye uwezo kiuchumi).

Kwanini? Ni kawaida kukuta kijana mwenye nguvu kabisa (sometimes alishindwa/aliacha shule) akilalamika kwamba so and so hawajanipa mtaji. Unakuta mtu ana nguvu na elimu lakini analalamika kwamba hajafanikiwa kwa sababu yeye ni mtoto wa Mkulima au baba yake hakuwa na uwezo. Au Mzee ana nguvu zake safi lakini anaishi maisha ya ajabu ulevi/uzinzi nk ukimuuliza anakwambia mwanangu/wanangu hawanisaidii! Au huyu huyu mzee alikamata pension yake akanywa pombe, akahonga, leo maisha yanampiga anasema ndugu/wanangu hawanisaidii.

Mimi naona si sawa. We need to do something. Wengi tunazidi kuwa maskini kwa sababu tunabeba mizigo ambayo siyo ya kwetu au hatustahili kubeba. Mimi naona hii tabia ndo imesababisha tunazalisha viongozi wa Hovyo hovyo! Hata akipewa uongozi hajui aufanyie nini. Hajui wajibu wake.

Mwisho wa siku tunakuwa na viongozi walalamishi na waongo kama waliowachagua. Kipi tufanye tusaidie watoto wetu wawe kizazi cha kuwajibika na kutambua kwamba maisha yao ni jukumu lao? Wachukie uongo na ulalamishi? Na zaidi waelewe kwamba crime doesn't pay? Wakishindwa wajue wameshindwa wao na si kwasababu ya mtu mwingine?

Masanja
 

Yodoki II

JF-Expert Member
Oct 17, 2014
5,269
2,000
Hii ni tabia inayochangia sana kudumaza maendeleo ya nchi zetu. Watu wanajiona kutokuwa na wajibu wowote.
 

Mkaruka

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
15,092
2,000
Mfano sisi Chadema tumeshindwa kwenda ikulu sababu kubwa ni MWENGE na KATIBA.
 

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,480
2,000
Aiseee,ni kweli kabisa hii.Kila mtu ana mtu wa kumsingizia tayari yupo akilini.
 

sayoo

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
4,115
2,000
Ni kwel aisee hii tabia cjui itatoka lin kwetu cc watanzania
 

MZEE MKUBWA

JF-Expert Member
Jun 24, 2017
3,966
2,000
Sio kazi rahisi kutake personal responsibilities kwa sababu tunapenda kujiona tuko sahihi muda wote ndio maana tunapeleka lawama kwa watu wengine
 

Inna

JF-Expert Member
Jan 13, 2017
11,076
2,000
Hiyo ni attitude iliyojengeka kwa waafrika wengi itaondoka pale mtu atakapojitambua anatakiwa awajibike vp na sio kukaa kumtegemea mtu

Raha yetu ni kulalamika kuliko kutekeleza wajibu
 

kiduni

JF-Expert Member
Jun 26, 2015
256
250
Wanasema hatujui wajibu wetu hata tunalotakiwa kutimiza wenyewe tunasema sababu Mungu, uchawi au utamtaja mtu inaonyesha akili zetu haziko sawa
 

kirikou1

JF-Expert Member
Nov 8, 2016
4,072
2,000
Wengi tuneangukia upande wa Walter Rodney anasema yote haya ni matokeo ya ukoloni. Lakini hatujiongezi kua hats huko ulaya na marekani wametawaliwa pia.
Nadhani hii attitude ipo kihistoria zaidi, karibu mataifa yote Afrika ndivo yalivo si wananchi si serikali
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
43,871
2,000
Mkuu hii kasumba ni kweli kabisa inatokea miongoni mwetu, na hii ni kwa sababu asili ya binadamu hapendi kukosolewa na kusingiziwa..muda wote anataka aonekane msafi hata kama amekosea vipi..Kukubali kosa na kuchukua majukumu huwa hataki kabisa..!

ila mkuu asante kwa elimu yako..nimepata cha kujifunza
 

jubilant

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
306
500
Hiyo imeshakuwa kama culture yetu Watanzania.
Kwangu ni oja kati ya tabia ninazozichukia sana, binafsi huwa nawafundisha wananngu na wale wanaonizunguka kuwa wakweli na kukubali wajibu na kuwajibika
 

Password

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
779
1,000
Hii tabia ni ngumu sana kuiacha kwasababu inajengeka tangu utotoni,unakuta mzazi anampiga mtoto wake halafu anambembeleza kwa kumpa juisi anywe,kisha anamuuliza nani kakupiga unashangaa litoto linamnyooshea kidole mtu mwingine. Hapa ndo tabia ya kusingizia inapoanza.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom