Tuirudishe Tanganyika Kwanza - Kiini cha Suluhisho

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,460
39,928
Je Zanzibar ni Nchi au si Nchi?

Na. M. M. Mwanakijiji

Nadhani hapa mgogoro wa lugha si wa lazima kabisa.

a. Zanzibar si nchi kwa maania ya sovereign State kama vile Tanzania Bara si nchi. Kuna nchi moja nayo inaitwa TAnzania (ambayo nguvu na mamlaka ya sovereignty yamo).

b. Hii haina maana kuwa huko nyuma Zanzibar haikuwahi kuwa nchi, ndiyo iliwahi kama vile Tanganyika ilivyowahi kuwa nchi. Hili halina ubishi. Zilipokuwa nchi hizi mbili zilikuwa na madaraka sawa ya nchi na uwezo sawa kama nchi. Nguvu hizi za nchi unaweza kuzisoma vizuri katika Azimio la Uhuru la Marekani la 1776.

c. Zanzibar hata hivyo ni Taifa (Nation, State). Mara nyingi tumekuwa tukizungumzia Nations kwa maana ya nchi lakini hasa nation ina maana ya watu wenye historia yao inayowajumuisha pamoja na kuwatofautisha na jamii nyingine. Na ndipo hapa hata neno "State" linapokuja.

Kuna kitu kinaitwa "Arab Nation", huu ni mfano mzuri wa kitu ambacho kinakubalika kuwepo lakini si nchi iliyopo. NI jamii ya watu. Na ni katika maana hii utakuta majimbo ya Marekani kwa mfano ya Magavana wake, Mahakama zake (hadi za Juu) na Majeshi yake (yanayoitwa National Guards).

d. Hivyo Zanzibar ni Taifa kwa maana hii ya pili, kwamba walipopoteza nchi yao kwa kuungana na Tanganyika hawakupoteza utaifa (Statehood with limited sovereignty). Hivyo ndio maana wakaendelea kuwa na Rais, Mahakama, Jeshi (KMKM) na Baraza lao la Kutunga Sheria. Kuwepo kwa vitu hivi hakunamaana Zanzibar kama nchi imerudishwa.

e. Hivyo basi ukiangalia sana utaona kuwa baada ya kuungana mambo makubwa mawili yalitokea ambayo ni kiini kwa kiasi kikubwa cha matatizo tuliyonayo katika Muungano:

Kwanza, Tanganyika ilipoteza nchi na ikapoteza Taifa. Hivyo hakuna nchi ya Tanganyika kama vile hakuna nchi ya Zanzibar, lakini pia hakuna Taifa la Watanganyika ingawa lipo Taifa la Wazanzibar.

Pili, Upande wa Tanganyika ambao walipoteza nchi na taifa lao wao wakavishwa hiki tunachokiita Muungano. Sasa tatizo la Muungano ulivyo sasa ni kama walivyosema ni kama "koti". Sasa koti linatakiwa kuvaliwa na mikono miwili ili likae vyema.

Wakati Zanzibar limeingiza mkono wake sawasawa upande mmoja, Bara inataka kuvaa mkono wake inakatazwa inaambia litundike shingoni tu lakini wakati huo huo mkono mmoja unaweza kuingia hadi katika ule wa Zanzibar na hivyo kunatokea hali ya kubanana. Zanzibar inasema "unanichukulia upande wangu" na bara wanasema "sasa mbona mimi nakatazwa hata kuingiza mkono uliowazi upande wangu?

Hivyo utaona basi koti halijavaliwa sawasawa na hivyo hata kutembea inakuwa matatizo. Hiki ndicho kinachoitwa kero za Muungano.

e. Hizi kero za Muungano zinaonekana sasa kwenye maneno. Zanzibar ni nchi au si nchi? Hili siyo swali sahihi! Swali linapaswa kuwa je katika mfumo wetu huu wa sasa Zanzibar na Bara bado ni nchi na zina utaifa wao? Jibu nimeshalitoa hapo juu.

Ni kwa sababu hiyo, basi utaona kati ya vitu vya kwanza ambavyo vinaweza kufanyika bila kuleta madhara makubwa ni kurudishwa kwa jina la Tanganyika kuelezea Tanzania bara, na hivyo kurudisha Utaifa wa bara japo kuwa haturudishi nchi.

Bara ikishakuwa na utaifa wake tunawarudishia limited sovereignty kwa kuamua kuwa Waziri Mkuu anakuwa ni Waziri Mkuu wa Bara ambaye ni mtendaji. Yaani anapigiwa kura kama kawaida. Tukishafanya hivyo, Bara na wenyewe wanaunda Baraza lao la Wawakilishi na kuwa na mfumo wao wa mahakama, na hili linafanyika kwa kutengeneza parallel judicial system ambapo una State Judiciary kama ilivyo Zanzibar lakini unapia Union Judiciary.

Katika kufanya hivi vyote Serikali ya Muungano bado inakuwa ndiyo sovereign. Sasa mtu anaweza akafikiri nilichosema ni serikali tatu. Hapana, nilichoonesha ni kuendelea na mfumo ule ule wa serikali mbili kwa maana unaserikali ya State na serikali ya Union.

Mahusiano kati ya hizi States mbili (Zanzibar na Tanganyika) yanakuwa katika misingi ya mahusiano ya kidugu ambapo uraia hauko wa Zanzibar au Tanganyika bali wa Tanzania lakini wananchi wake wanaweza kuendelea kujiita Wazanzibari au Watanganyika bila haja ya kujisikia wanausaliti Muungano.

Bila ya shaka utaona vinafanana sana na mfumo wa Marekani. Ndiyo kwa sababu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafanana zaidi na Muungano wa Marekani kuliko nchi nyingine nyingi, kwani States za Marekani zilipokuja kukaa chini na kuungana zile Original 13 zilikuwa ni nchi kamili. Ndiyo maana hata wakati mwingine tunapoyaita "majimbo" ya Marekani siyo tafsiri sahihi, kwani siyo Provinces kama za Afrika ya Kusini bali ni "States" ndani ya Muungano wao, na kila siku tangu waungane wamekuwa wakishughulika kuimarisha.

Naamini na sisi tunaweza kuumirisha muungano wetu kwa njia nyepesi na Rais, hasa tukianza na hili la kurudisha jina la Tanganyika kwanza, na kumrudisha Waziri Mkuu wa Tanganyika na Baraza lake la Mawaziri na Baraza la Wawakilishi.

NB: NImeandika nikiwa namjibu mtu kwa hiyo kuna mambo ambayo nikiamka bila ya shaka nitapanua kidogo, kuyafafanua na kuyaendeleleza. huu ni mwanzo tu.
 
Kuna tafauti gani kati ya madai yako ya kutaka kuibua Tanganyika iliyomezwa kwenye muungano na "madai ya Kihaini' ya wazee wa Pemba walioomba wasaidiwe Pemba yao iwe na uhuru kama walivyosema kwenye barua, ombi lao la "creating an environment for the formation of a federal state in Zanzibar" ?

Umefanya uhaini?
 
Katika kufanya hivi vyote Serikali ya Muungano bado inakuwa ndiyo sovereign. Sasa mtu anaweza akafikiri nilichosema ni serikali tatu. Hapana, nilichoonesha ni kuendelea na mfumo ule ule wa serikali mbili kwa maana unaserikali ya State na serikali ya Union.

Je katika mfumo huo, Watanganyika na Wazanzibar watatakiwa kuchangia gharama za muungano sawa kwa sawa au Mmoja atatakiwa atoe fungu kubwa zaidi?

2:Vipi kuhusu gharama za kuendesha serikali ya Tanganyika(state), je watanganyika wataweza kuhimili gharama mbili, zile za kurun serikali ya state ya Tanganyika na wakati huo huo wachangie fungu la kuendesha serikali ya Union?
 
  • Thanks
Reactions: Bon
Kuna tafauti gani kati ya madai yako ya kutaka kuibua Tanganyika iliyomezwa kwenye muungano na "madai ya Kihaini' ya wazee wa Pemba walioomba wasaidiwe Pemba yao iwe na uhuru kama walivyosema kwenye barua, ombi in "creating an environment for the formation of a federal state in Zanzibar" ?

Umefanya uhaini?

Ooohhhhhhh. The smell of serikali ya majimbo. Huu mjadala uko huku pia http://ashawazenj.blogspot.com

Naunga mkono hoja

Asha
 
Zanzibar ni Nchi hili halina mjadala wala haja ya kupigishana makelele.Kwa mfano rahisi tu Nchi zinapoungana kila kitu huondoka nikimaanisha serikali na hata jina la Nchi ,sasa japo Nyerere alionekana mjanja lakini kwa hili alizidiwa ,yeye kwa ujuaji anaoujua mwenyewe alikubali kuiua Tanganyika na kuiwacha Zanzibar intact (Serikali yake ,majeshi yake).
Anaesema Zanzibar si Nchi huyo anajipendekeza kwa mafisadi ,ni bora ikadaiwa na kurudishwa Tanganyika ili mafisadi wasambaratishwe.
 
Je Zanzibar ni Nchi au si Nchi?

Na. M. M. Mwanakijiji

Nadhani hapa mgogoro wa lugha si wa lazima kabisa.

a. Zanzibar si nchi kwa maania ya sovereign State kama vile Tanzania Bara si nchi. Kuna nchi moja nayo inaitwa TAnzania (ambayo nguvu na mamlaka ya sovereignty yamo).

b. Hii haina maana kuwa huko nyuma Zanzibar haikuwahi kuwa nchi, ndiyo iliwahi kama vile Tanganyika ilivyowahi kuwa nchi. Hili halina ubishi. Zilipokuwa nchi hizi mbili zilikuwa na madaraka sawa ya nchi na uwezo sawa kama nchi. Nguvu hizi za nchi unaweza kuzisoma vizuri katika Azimio la Uhuru la Marekani la 1776.

c. Zanzibar hata hivyo ni Taifa (Nation, State). Mara nyingi tumekuwa tukizungumzia Nations kwa maana ya nchi lakini hasa nation ina maana ya watu wenye historia yao inayowajumuisha pamoja na kuwatofautisha na jamii nyingine. Na ndipo hapa hata neno "State" linapokuja.

Kuna kitu kinaitwa "Arab Nation", huu ni mfano mzuri wa kitu ambacho kinakubalika kuwepo lakini si nchi iliyopo. NI jamii ya watu. Na ni katika maana hii utakuta majimbo ya Marekani kwa mfano ya Magavana wake, Mahakama zake (hadi za Juu) na Majeshi yake (yanayoitwa National Guards).

d. Hivyo Zanzibar ni Taifa kwa maana hii ya pili, kwamba walipopoteza nchi yao kwa kuungana na Tanganyika hawakupoteza utaifa (Statehood with limited sovereignty). Hivyo ndio maana wakaendelea kuwa na Rais, Mahakama, Jeshi (KMKM) na Baraza lao la Kutunga Sheria. Kuwepo kwa vitu hivi hakunamaana Zanzibar kama nchi imerudishwa.

e. Hivyo basi ukiangalia sana utaona kuwa baada ya kuungana mambo makubwa mawili yalitokea ambayo ni kiini kwa kiasi kikubwa cha matatizo tuliyonayo katika Muungano:

Kwanza, Tanganyika ilipoteza nchi na ikapoteza Taifa. Hivyo hakuna nchi ya Tanganyika kama vile hakuna nchi ya Zanzibar, lakini pia hakuna Taifa la Watanganyika ingawa lipo Taifa la Wazanzibar.

Pili, Upande wa Tanganyika ambao walipoteza nchi na taifa lao wao wakavishwa hiki tunachokiita Muungano. Sasa tatizo la Muungano ulivyo sasa ni kama walivyosema ni kama "koti". Sasa koti linatakiwa kuvaliwa na mikono miwili ili likae vyema.

Wakati Zanzibar limeingiza mkono wake sawasawa upande mmoja, Bara inataka kuvaa mkono wake inakatazwa inaambia litundike shingoni tu lakini wakati huo huo mkono mmoja unaweza kuingia hadi katika ule wa Zanzibar na hivyo kunatokea hali ya kubanana. Zanzibar inasema "unanichukulia upande wangu" na bara wanasema "sasa mbona mimi nakatazwa hata kuingiza mkono uliowazi upande wangu?

Hivyo utaona basi koti halijavaliwa sawasawa na hivyo hata kutembea inakuwa matatizo. Hiki ndicho kinachoitwa kero za Muungano.

e. Hizi kero za Muungano zinaonekana sasa kwenye maneno. Zanzibar ni nchi au si nchi? Hili siyo swali sahihi! Swali linapaswa kuwa je katika mfumo wetu huu wa sasa Zanzibar na Bara bado ni nchi na zina utaifa wao? Jibu nimeshalitoa hapo juu.

Ni kwa sababu hiyo, basi utaona kati ya vitu vya kwanza ambavyo vinaweza kufanyika bila kuleta madhara makubwa ni kurudishwa kwa jina la Tanganyika kuelezea Tanzania bara, na hivyo kurudisha Utaifa wa bara japo kuwa haturudishi nchi.

Bara ikishakuwa na utaifa wake tunawarudishia limited sovereignty kwa kuamua kuwa Waziri Mkuu anakuwa ni Waziri Mkuu wa Bara ambaye ni mtendaji. Yaani anapigiwa kura kama kawaida. Tukishafanya hivyo, Bara na wenyewe wanaunda Baraza lao la Wawakilishi na kuwa na mfumo wao wa mahakama, na hili linafanyika kwa kutengeneza parallel judicial system ambapo una State Judiciary kama ilivyo Zanzibar lakini unapia Union Judiciary.

Katika kufanya hivi vyote Serikali ya Muungano bado inakuwa ndiyo sovereign. Sasa mtu anaweza akafikiri nilichosema ni serikali tatu. Hapana, nilichoonesha ni kuendelea na mfumo ule ule wa serikali mbili kwa maana unaserikali ya State na serikali ya Union.

Mahusiano kati ya hizi States mbili (Zanzibar na Tanganyika) yanakuwa katika misingi ya mahusiano ya kidugu ambapo uraia hauko wa Zanzibar au Tanganyika bali wa Tanzania lakini wananchi wake wanaweza kuendelea kujiita Wazanzibari au Watanganyika bila haja ya kujisikia wanausaliti Muungano.

Bila ya shaka utaona vinafanana sana na mfumo wa Marekani. Ndiyo kwa sababu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unafanana zaidi na Muungano wa Marekani kuliko nchi nyingine nyingi, kwani States za Marekani zilipokuja kukaa chini na kuungana zile Original 13 zilikuwa ni nchi kamili. Ndiyo maana hata wakati mwingine tunapoyaita "majimbo" ya Marekani siyo tafsiri sahihi, kwani siyo Provinces kama za Afrika ya Kusini bali ni "States" ndani ya Muungano wao, na kila siku tangu waungane wamekuwa wakishughulika kuimarisha.

Naamini na sisi tunaweza kuumirisha muungano wetu kwa njia nyepesi na Rais, hasa tukianza na hili la kurudisha jina la Tanganyika kwanza, na kumrudisha Waziri Mkuu wa Tanganyika na Baraza lake la Mawaziri na Baraza la Wawakilishi.

NB: NImeandika nikiwa namjibu mtu kwa hiyo kuna mambo ambayo nikiamka bila ya shaka nitapanua kidogo, kuyafafanua na kuyaendeleleza. huu ni mwanzo tu.

Hili jambo halipas kuwa ni hoja ya kulumbaniwa sana. Na ninashangaa hata wasomi nao wanakuwa wanakuna vichwa kwa hili. Hebu fanyeni analysis ya hili jambo. Nashukuru mtu wa kijiji kwa mawazo yako haya yanaweza kuwa ni basis ya hiyo analysis. Zanzibar ni nchi na ni Taifa kama ilivyo Tanganyika. na Tanzania ni Nchi na Taifa kama ilivyo Zanzibar na Tanganyika. Isipokuwa Zanzibar ni Nchi na Taifa shirikishi la Tanzania. Tanganyika ni Nchi na Taifa kivuli la (ya) Tanzania. Haya hapo- chambueni. Lakini kwa ufupi tu U-nchi na U-taiafa haufi madhali umekuwa na uhai. Hivyo si sahihi kuwa u-nchi na U-taia wa Mataifa ya Zanziba na Tanganyika umekufa wakati wa kuunda nchi na Taifa la Tanzania pale 1964. Zanzibar imeingia katika u-shirikishi. na Tanganyika imeingia katika u-kivuli.
 
Mimi siku zote nimekuwa nikiwaza kwamba, kama ni suala la utaifa basi utaifa wa Tanganyika na utaifa wa Zanzibar urudi na kila mmoja abakie na sovereignty yake na Muungano uitwe wa United Republic of Tanganyika and Zanzibar.

Sasa kwanza itabidi katiba zote mbili zipitiwe upya na itungwe katiba mpya ya Muungano na ambayo ni ya sovereignty kwamba itaongoza Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Pili Bunge litakuja kutokana na uongozi wa katiba hiyo na bunge hili Parliament Sovereignty litakuwa na maamuzi yanayohusu sovereignty ya Muungano bila kuathiri bunge la taifa la Zanzibar ambalo hupanga mambo ya Zanzibar tu.

Pia hili bunge la Muungano lilasimamia mambo yote ya msingi likiwemo la foreign policy ambayo ziku zote ni la Sovereign state na sio nation tu.

Ikiwa hivyo basi, hata pasi za kusafiria zibadilishwe na ijulikane hata kule UN na duniani kote kwamba sasa kuna United Republic of Tanganyika na Zanzibar kama "sovereign state".

Pia suala la Muungano litakuwepo kwa basis ya mataifa haya mawili ku-share bahari, bandari, jeshi na polisi.

Kwa kuwa tatizo la kubinywa lipo Zanzibar basi iachiwe baraza lake la wawakilishi ili litoe maamuzi ya taifa la Zanzibar kuhusu maendeleo yake yakiwemo yale ambayo yanaguza kitu kinachoitwa Muungano kama sera ya mambo ya nje.

Huo ndo mtazamo wangu.
 
Nakubaliana na ushauri wa Mwanakijiji kuwa suluhisho ni moja nalo kuweko na Tanganyika ndani ya Muungano wa Tanzania kwani ndipo patakuwa na usawa. Iwejesehemu moja ya Muungano imiliki mambo yote ya Kiserikali(soveregnity) ikitumia jina la Tanzania na sehemu moja isiwe na uhuru wa kutumia shughuli za Kiserikali.
Katika kuangalia kero za muungano wengi wa wananchi wa Tanganyika hueleza suala la Zanzibar kuwa na Serikali na Tanganyika kukosa Serikali lakini hawaoni kuwa hakuna haja ya kudai serikali kwani kila kitu cha Tanganyika kinafanywa kwa mgongo wa wa Serikali ya Muungano na hivyo hakuna kipingamizi chochote kwa shughuli yoyote inayohusu Tanganyika kufanyika. Kinyume na Zanzibar wao hawawzi kufanya chochote kilicho nje ya visiwa bila ya kupata ruhusa kutoka kwa Serikali ya Muungano au kwa jina jengine Serikali ya Tanganyika.
Hali ya sasa isingekuwa mbaya kama ilivyo sasa kama Watanganyika wangekuwa na Fikra za Muungano na udugu kwa mkubwa juu ya mdogo na badala yake wengi wa Viongozi wa Muungano (Tanganyika) wana fikra za kikoloni juu ya Zanzibar wanachotaka kuiona Zanzibar haiondoki kwenye makucha yao na ndio maana wanaziba kila njia ambayo Zanzibar ingeweza kujinasua kwenye makucha ya Tanganyika. Wanahakikisha kuwa Zanzibar inabaki katika utegemezi wa Tanganyika kwa muda wote hivyo kuizibia njia zote za mawasiliano na watu wa kuisaidia Zanzibar. Zanzibar haina mali asili kama Tanganyika na hivyo huitaji muingiliano na nchi za kigeni kama bandari huru, mahusiano na mashirika ya kimataifa na nji8a nyengine kama hizo. Kama viongozi wa Tanganyika wasingekuwa na roho ya wivu wa mkubwa kwa mdogo wake wangeiachia Zanzibar kutafuta njia za kujiendeleza kwani maendeleo ya Zanzibar ni sifa kwa Tanzania (Tanganyika)
Hivyo basi kama Watanganyika wana lengo la kuifanya Zanzibar iache utegemezi na badala yake iwe mshiriki katika Muungano basi na irejeshwe Tanganyika formerly na baadae kuwepo Serikali ya Tanzania lakini sasa ipo Zanzibar na Tanganyikaq ilijivisha koti la Tanzania.
 
Sioni mtu kuwa mjinga kama kusema Zanzibar haipo,wandugu Zanzibar haikuzimwa na hila za Nyerere lakini Tanganyika ndio haipo ,hili mkilitaka au msilitake ,mimi inaniuma sana sana kuona Tanganyika haipo na imeondolewa katika ramani ya dunia labda kwenye vitabu vya Historia,hivi sijui waTanganyika tumefikwa na masaibu gani mpaka tukawakubalia watu wawili wale wapatane kwa maslahi yao binafsi yaani Karume na Nyerere ,japo Nyerere alizidiwa na Karume ,sisemi kama nipo usingizini ila kwa maneno ya wazee wenye busara wanaona hata kifo cha Karume kilitokana na Nyerere ,kwani Karume alikuwa na Jeuri ya kwao Malawi,kisa kimoja ambacho kilimkasirisha Mwalimu Nyerere ni pale alipokwenda Zanzibar na hakuteremka alibakia kwenye chombo halafu akampigia simu karume kumwambia nipo kwenye chombo njoo tuzungumze karume akamjibu mwenye mavi hufuata choo ,sasa wewe umikuja na haja zako ni wajibu wako kunifuata mimi na sio mimi nikufuate wewe hapo mwalimu akageuza boti na kurudi Tanganyika ,tokea hapo picha zikawa haziendani.Hicho ni kisa ambacho kilimpelekea Karume kutolewa roho ili kulinda maslahi ya Tanganyika. Sina uhakika wa habari hio ila huwa kunahadithiwa.
Kwa kweli jambo la muhimu ni kuirudisha Tanganyika ili mzizi wa fitna uondoke na hili linawezekana kabisa.
 
Kwa maoni yangu suluhisho ni tuwe na serikali tatu ama serikali moja, hili la serikali tatu ni muafaka na naliunga mkono zaidi, itabidi tuwe na muundo wa serikali mbili ambazo zitakuwa na legal system, constitution na parliament zao na Serikali kuu ya muungano iundwe kwa kuzingatia katiba na sheria za serikali hizo mbili. Muungano ni nguvu lakini inategemea maamuzi na utekelezaji wa shughuli za huo muungano, ili muungano uwe na nguvu hakuna budi pande zote zinazohusika ziwe na mamlaka sawa, wananchi wapewe haki sawa bila kubagua mkoa, kanda gani wametokea na mchango gani mkoa, kanda umechangia katika kupatikana MAPATO ya taifa, MAPATO ya taifa yawanufaishe wananchi wote! Ukiangalia historia Muungano wa Marekani ama Muungano wa Britania ndio uliozipa nchi hizo nguvu walizonazo, narudia kusema umoja ni nguvu na ndio sababu huku Ulaya wanazidi kuupanua Umoja wa Ulaya ili uwe na nguvu zaidi kushindana na Umoja wa Marekani ama Uchina. Ni kweli panapo muungano wowote lazima kutakuwa na hitilafu, kinachotakiwa kufanyika ni kuzijadili kasoro zilizopo na zitafutiwe suluhisho mara moja kwa manufaa ya Taifa, mfano Muungano wa Britania na Ireland ya Kaskazini(United Kingdom of G.Britain & N. Ireland) una matatizo yanayofanana na ya kwetu, Waingereza wanadaiwa kuwameza Wa-skoti, wa-welsh na wa-irishi, kuanzia katika usawa na haki, kwenye kugawa mapato ya nchi hadi uwakilishi katika bunge na vyombo vya sheria nk, lakini hapohapo haya mataifa matatu ya Scotland, N.Ireland na Wales wana bendera zao,wana bunge na kwa upande wa Scotland hata pesa yao? Kuna Scottish Parliament, N. Ireland Assembly na Welsh assembly, hapo hapo Waingereza hawana assembly ama parliament ya kuangalia maslahi ya Uingereza peke yake bali wana chombo cha jumla kiitwacho House of Commons, kuna kelele nyingi zinatoka upande wa Uingereza kwamba wao ndio shina la uchumi wa UK lakini haina uwakilishi na inanufaisha UK nzima badala ya England peke, na wale wa Scotland na Wales wanalalamika kuwa wanaburuzwa, kila kitu kinaamuliwa England, kwa hio na tusome kutoka kwa hawa wenzetu (UK na USA) na tuchukue yale mazuri toka kwao tuya-adopt katika katiba yetu na tuchunguze yale mapungufu yao ili tusiangukie huko. Ni hayo tu.
 
Kwani CUF wanaposema suluhisho ni serikali tatu mlifikiria nini ? Naona kuna haja ya kuinadi sera hii ya CUF kwa Watanganyika wote ambao bado wamengangania Tanzania ,CUF inaidai Tanganyika kutokana na mfumo wa sera yao na ndipo wengine wanapojiuliza kama CUF ikishika madaraka Zanzibar na CCM kuendelea kuifisidi Tanganyika nini matokeo yake ? Naona matokeo ni serikali tatu tu CCM wakitaka au wasitake kazi itakuwa kwao kujipapatua kwani faida wanayoipata CCM ni kuzishika hatamu za Dola na hivyo kuweza kufisidi kila kitu mpaka wamefika Ikulu kufanya sehemu ya biashara zao binafsi ndipo wahafidhina wakasema Zanzibar hakuna fisadi japo si kweli.
Tanganyika sasa ni lazima itiwe maji ili izinduke maana kwa wakati huu tunajua kuwa haikufa bali ilizimia.
 
Kuna tafauti gani kati ya madai yako ya kutaka kuibua Tanganyika iliyomezwa kwenye muungano na "madai ya Kihaini' ya wazee wa Pemba walioomba wasaidiwe Pemba yao iwe na uhuru kama walivyosema kwenye barua, ombi in "creating an environment for the formation of a federal state in Zanzibar" ?

Umefanya uhaini?

..it's a matter of time, tanganyika itarudi!
 
Mimi siku zote nimekuwa nikiwaza kwamba, kama ni suala la utaifa basi utaifa wa Tanganyika na utaifa wa Zanzibar urudi na kila mmoja abakie na sovereignty yake na Muungano uitwe wa United Republic of Tanganyika and Zanzibar.
Huo ndo mtazamo wangu.

Mimi bado ninatetea mfumo wa sasa kuwa ni sahihi kabisa na unaofaa. Hongera kwa walioubuni. Utaifa na Sovereignity haviondoki wala havifi. Hivyo Zanzibar haikupoteza utaifa wake wala sovereignity yake kwa kuingia Muungano. na Tanganyika haikupoteza vile vile vitu hivyo kwa kuingia Muungano. Hata jina halikupotea ila limebadilishwa matamshi tu, Kwani nahakika kuwa na wewe unaitaja kila mara Tanzania Bara (hiyo ndiyo Tanganyika) Aina ya Muungano unaopendeklza wewe haifai ukizingatia vitu unavyotaka kuunganisha Zanzibar na Tanganyika (ambapo Zanzibar kwa hali yoyote ile kieneo, ki-utajiri, ki rasilmali, ) si jui ni marangapi kwa Tanganyika. Aina hiyo yafaa labda pengine kwa Tanganyika na Kenya)Tatizo la Tanzania kwa hivi sasa ni la utekelezaji wa sura na muundo huu tuliouchagua. Na tuangalie mapungufu yaliyopo. Mfumo wa Serikali Tatu hauwafai Wazanzibari. Lakini hawataki kuangalia suala hili kwa undani. Wao mara nyingi huangalia upande wa haki zao tu (kuwa wakiwa katika Serikali tatu basi watazipata inavyostahili) Sawa. Lakini hawafikirii kuwa kuna haki na wajibu. Jee wajibu wao wataweza kuutekeleza vizuri katika mfumo huo wa Serikali tatu. Hilo Jeshi watashiriki vyema?. Watawapata wapi watu wa kuwaingiza Jeshini kulinda mipaka katika kiwango sawa na patner wao. Jee gharama za kukimu vitu hivyo vya pamoja watazipata wapi na kutoa kwa kiwango kinachitakiwa kiuuwiano. Hili suala wananchi tunahitaji taaluma ya kutosha. Wasomi tusaidieni.
 
Zanzibar ni Nchi hili halina mjadala wala haja ya kupigishana makelele.Kwa mfano rahisi tu Nchi zinapoungana kila kitu huondoka nikimaanisha serikali na hata jina la Nchi ,sasa japo Nyerere alionekana mjanja lakini kwa hili alizidiwa ,yeye kwa ujuaji anaoujua mwenyewe alikubali kuiua Tanganyika na kuiwacha Zanzibar intact (Serikali yake ,majeshi yake).
Anaesema Zanzibar si Nchi huyo anajipendekeza kwa mafisadi ,ni bora ikadaiwa na kurudishwa Tanganyika ili mafisadi wasambaratishwe.

..zanzibar haina majeshi, ina vikosi. in other words, zanzibar has no army but a number of militia groups.
 
Kwani CUF wanaposema suluhisho ni serikali tatu mlifikiria nini ? Naona kuna haja ya kuinadi sera hii ya CUF kwa Watanganyika wote ambao bado wamengangania Tanzania ,CUF inaidai Tanganyika kutokana na mfumo wa sera yao na ndipo wengine wanapojiuliza kama CUF ikishika madaraka Zanzibar na CCM kuendelea kuifisidi Tanganyika nini matokeo yake ? Naona matokeo ni serikali tatu tu CCM wakitaka au wasitake kazi itakuwa kwao kujipapatua kwani faida wanayoipata CCM ni kuzishika hatamu za Dola na hivyo kuweza kufisidi kila kitu mpaka wamefika Ikulu kufanya sehemu ya biashara zao binafsi ndipo wahafidhina wakasema Zanzibar hakuna fisadi japo si kweli.
Tanganyika sasa ni lazima itiwe maji ili izinduke maana kwa wakati huu tunajua kuwa haikufa bali ilizimia.

Mheshimiwa Mwiba kulikoni? Sera zako za CUF baki nazo mwenyewe. Wazanzibari hawataki Serikali tatu hata siku Moja. Na wala hawataki Serikali Moja. Kama ni Muungano na uwepo basi ni kwa mfumo huu wa sasa. Mwiba - Mwiba- Kisiwa chako cha Pemba na Unguja yake vinaingia mara ngapi katika eneo la Tanganyika. Wewe unaona haki yako tu mbele (kwani umezoea kutoa madai ya haki kila mara) Lakini usisahau wajibu. Wajibu utakaokuwa nao. Wajibu Zanzibar itakayokuwa nayo katika mfumo huo wa Serikali tatu. Amka Mwiba -na acha jazba za Upemba.
 
Mimi bado ninatetea mfumo wa sasa kuwa ni sahihi kabisa na unaofaa. Hongera kwa walioubuni. Utaifa na Sovereignity haviondoki wala havifi. Hivyo Zanzibar haikupoteza utaifa wake wala sovereignity yake kwa kuingia Muungano. na Tanganyika haikupoteza vile vile vitu hivyo kwa kuingia Muungano. Hata jina halikupotea ila limebadilishwa matamshi tu, Kwani nahakika kuwa na wewe unaitaja kila mara Tanzania Bara (hiyo ndiyo Tanganyika) Aina ya Muungano unaopendeklza wewe haifai ukizingatia vitu unavyotaka kuunganisha Zanzibar na Tanganyika (ambapo Zanzibar kwa hali yoyote ile kieneo, ki-utajiri, ki rasilmali, ) si jui ni marangapi kwa Tanganyika. Aina hiyo yafaa labda pengine kwa Tanganyika na Kenya)Tatizo la Tanzania kwa hivi sasa ni la utekelezaji wa sura na muundo huu tuliouchagua. Na tuangalie mapungufu yaliyopo. Mfumo wa Serikali Tatu hauwafai Wazanzibari. Lakini hawataki kuangalia suala hili kwa undani. Wao mara nyingi huangalia upande wa haki zao tu (kuwa wakiwa katika Serikali tatu basi watazipata inavyostahili) Sawa. Lakini hawafikirii kuwa kuna haki na wajibu. Jee wajibu wao wataweza kuutekeleza vizuri katika mfumo huo wa Serikali tatu. Hilo Jeshi watashiriki vyema?. Watawapata wapi watu wa kuwaingiza Jeshini kulinda mipaka katika kiwango sawa na patner wao. Jee gharama za kukimu vitu hivyo vya pamoja watazipata wapi na kutoa kwa kiwango kinachitakiwa kiuuwiano. Hili suala wananchi tunahitaji taaluma ya kutosha. Wasomi tusaidieni.

..labda uwaongopee watoto wa vidudu!

..tanganyika haipo! zanzibar ipo. halafu,zanzibar si nchi, nchi ni tanzania!

..mfumo pekee utakaoweza kufanya kazi vizuri ni wa serikali moja na majimbo kadhaa. hili litabezwa sana ila ndio dawa yenyewe.
 
We are supposed to move forward on this issue. No need to come back, useless. There are more serious issues which we need to be discussing! Wanasiasa watoto na wadogo ndio wanatakiwa kujadili issue hii! Sidhani kama Tanganyika ikirudi ufisadi utapungua, Sidhani kama Zanzibar ikiwa na full autonomy itakuwa na mabadiliko yoyote ya kubadilisha hali ya yakhe, sana sana tunaona kuchinjana kukitokea au Salmin ataurudi na kuendesha udikteta. So no need, let us just move forward.
 
Mkuu,

Wazo lako ni zuri ila mkuu naona hiyo haitakuwa suluhisho la matatizo yetu ya muungano.
Tatizo kubwa hapa ni umasikini uliopindukia na hali duni za wananchi wetu!
Ili kukabiliana na hali hii suluhisho siyo kuwa na serikali mbili au tatu au nne au tano! suala hapa ni kuangalia jinsi ya kuondoa umasikini miongoni mwa wananchi wetu period!

Wengi wanafikiri kuwa na mfumo kama wa Marekani basi utaondoa au kurekebisha matatizo ya muungano nchini mwetu,si kweli.Marekani wanayo historia yao na sisi tunayo historia yetu.Wao walikuwa na slavery hapo mwanzo hivyo kuweza kujilimbikizia mali na uwezo kwa kuwatumia slaves katika uzalishaji,ujenzi wa miundo mbinu na kadhalika na hivyo kuweza kuhimili gharama kubwa za uendeshaji na uundaji wa serikali yao mpaka ilipofikia sasa.Ni majuzi tu (1963) ndipo walipoamua kuwa na civil rights! hivyo ingawa slavely ilipigwa marufuku kitambo kidogo lakini unyonyaji ulikuwa unaendelea na hivyo kuzipa serikali za majimbo faida kubwa na nguvu za kujiendesha.
Waarabu wanayo mafuta na hivyo kuweza kuhimili gharama za uendeshaji wa serikali na mifumo mbalimbali kwa hiyo sidhani kama sisi tunao wigo mpana namna hiyo.

Kwamba tuwe na states mbili( Tanganyika na Zanzibar) na serikali moja ya muungano.Kila state iongozwe na waziri mkuu na pia tuwe na raisi mmoja ambaye ndiye atakuwa mkuu na kiongozi wa serikali ya muungano.Kwa haraka haraka hii inaonyesha kuwa inaweza kuwa ni suluhisho la kero ya muungano lakini hebu tujiulize haya yafuatayo:

Moja,Zanzibar siyo united kama wengi wanavyofikiri yaani Zanzibar kwenyewe kuna matatizo kati ya Pemba na Unguja.Tena kuna wapemba ambao wanataka Pemba itambuliwe kama nchi au kwa hapa tunaweza kuiita state kamili.Hivyo basi nionavyo mimi huenda tukaja ishia kuwa na states tatu yaani Unguja,Pemba,na Tanganyika.Je tutakuwa tupo tayari kwa hilo? vipi na watu wa Mafia nao siku moja wakiamua kuwa na state yao tutawanyima??maana kama Pemba ikikubaliwa kuwa state kamili sioni kwanini Mafia wanyimwe! wapi tunachora mstari?
Pili,Ni wazi kabisa gharama za uendeshaji wa system hii utakuwa ni mzigo mkubwa kwa wananchi! kwa kuwa tutahitaji kuwa na serikali ya muungano yenye bunge la muungano,jeshi la muungano,mahakama ya muungano,na kadhalika! halafu pia hivyo vijiserikali vya states,je mkuu tutaweza kuhimili hivi vishindo? mimi naona tutakuwa tunatumia pesa nyingi kuendesha serikali na siyo kuzitumia kuleta maendeleo kwa wananchi.

-Wembe
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom