Elections 2010 Tuipime hotuba yaa Kikwete ya leo November 18 2010 bungeni

mzungukichaa

Member
Nov 8, 2010
57
27
Wadau...tuipime hotuba hii ya mweshimiwa kwa uchakachuaji bungeni.. Mi nimesikiliza suala la michezo limenipa kichefuchefu..
'Tumeleta makocha wazungu kufundisha michezo...' hivi hii ni akili au mgango :A S cry:
 
Hivi mnaleta kujadili vitu vya mtu ambae tuna-conclusion ya kuwa ana matatizo chungu nzima. mwenzenu akili yake iko likizo na sasa anatumia za vilaza wa bongo wakina Makamba, Rostam, Ridhiwan na Salm.

Haya shauri yenu, kama mnapotezaz muda mkidhani mnajadili hotuba ya Raisi naskitika kuwambia mnajadili mawazo ya watu na wala sio hoja za anayeitwa raisi.

Mnakumbuka wakati wa hotuba ya wafanyakazi, watu wakadhani raisi kasema kumbe wahuni kadhaa wamemdanganya na kufanya mzee wa watu (samahani kwa wale ambao kwao ni kijana) aongee pumba.
 
Ni hotuba nzuri na iliyokidhi vigezo vyote ambavyo vinatoa mwelekeo wa serikali yake kwa 201-2015, hakuna alicho acha kwenye hotuba yake hii. Amezungumzia utawala bora, Muungano, Michezo, Maslahi ya watumishi serikalini, Ushirikiano wa kimataifa,Wajibu wa Bunge, Muundo wa baraza lake la mawaziri na watu wenye sifa gani, Ukusanyaji wa mapato ya serikali nk.
 
Amethink twice -hakuna kipya kingunge ndani, megji ndani, lowasa ndani rostam ndani yaan wizi mtupu -hivi nini kipya na kati ya hotuba ya 2005 na 2010 usanii mtupu -kweli mgando
 
Nashukuru mungu amemaliza bila kuanguka ingawa vikohozi vya apa na pale vilikuwa haviishi.
Naona dk wake alimshauri awe anagonga maji frequently
 
Naona dk wake alimshauri awe anagonga maji frequently

:nono:
Hii ya maji mi inantia shaka:Hali ilikuwa hii hii siku ile ya 'mdahalo' aitiviii.

Lazima kuna kitu. Sisemi ila hata mi ilianz ivi ivi, nikaambiwa hiyo ni safi. Maji ni mazuri kwa afya, baadae dk akasema una ......... Ndio manaake
 
Hotuba nzuri! maskini Tanzania! Kagoda? Takukuru kumsafisha Chenge wasifiwe?!!!!!!!!
We may remain stagnant in this poverty quagmire kama tutaendelea kuwa na thick brain kiasi hiki?
 
Hotuba ya JK bungeni leo haina tofauti na hotuba zake wakati wa kampeni-ahadi kibao-meli kubwa, international airports, hosptiali za rufaa nk!!!!!!!!!! Ni ndoto kwa za mchana kweupe kwa sababu:-
1) Wafadhili watasimamisha misaada kutokana na ushahidi utakaotaolewa na CDM kuhusu wizi wa kura za watanzania!!!!!!!!!!.
2) Fedha zitakazokusanywa humu nchini hazitatosheleza budget requirements za JK, EL, RA, AC, + other hidden fisadis kujaza mifuko yao ya ufisadi-kufidia matrilion walizohonga wakati wa kampeni!!!!!!!!!!!!
3) Hiki ni kipindi cha JK cha mwisho, hatajali mtasema nini!!!!
4) Nchi haitatawalika kirahisi kwa sababu ya matokeo ya hayo hapo juu (1-4)!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

NB: Mwaka 2005 JK alikuwa kipennzi cha wengi vijana na wazee!!!!!!!!!. Safari hii JK ni adui mkubwa wa vijana walio wengi ambao ndiyo walioathirika na wizi wa kura uliofanywa na JK!!!!!!!!!!! Ni kipindi cha mageuzi ya mfumo dhalimu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Maneno ya taarabu yalikuwepo pia...sijaona kipya zaidi ya ahadi zile zile za kampeni!!!
 
At least umesema hotuba ya Kikwete, ungeweka Rais wala nisingefungua kusoma, in General nothing new & expect nothing, nothing from JK, nadhani hata ulimwona dhamira yake inavyomsuta, hana confidence, as usual kashamchagua Meghji kashfa kibao, full usanii period
 
What new for thieves? Tunategemea Atakubali Kuunda Commission ya Kuchunguza Uchaguzi na Kamati Nzima ya Uchaguzi.
 
Rais Kikwete anachonifurahisha pale anaposema serikali yake imefanikiwa kwa kwenda Marekani na Ulaya kuomba. Anahalalisha safari zake za nje zimesaidia nchi.Taifa linaendelea kuwa ombaomba nawe unasijifu. Mfano rahisi, mtu una familia alafu unawaeleza watu mafanikio ya familia yako ni kuwa umeenda kwa majirani na wamekupa misaada na mikopo. Tanzania inaweza kufanikiwa ikiwa kama Raid Kikwete akipunguza matumizi makubwa ya serikali ikiwa safari zake na viongozi wenzake kukagua miradi kila siku.Aunde serikali ndogo, na ahakikishe hawa wawekezaji wa nje wasipewe kipaumbele kama wawekezaji wazawa. Pia mianya ya rushwa ambayo ye anaijua vizuri kwa kuwachagua walewale walioshindwa kina Lowasa, Mramba, Meghji. Mfano mzuri chukualia Shamsi Nahodha, ni mjumbe wa baraza la wawakilishi-mshahara anakula, mgumbe wa kuteuliwa-mshahara anakula, akipewa uwaziri-mshahara mwingine. Ni bora wangekua watu wengine kwani pangekua na ajira 2 zaidi. Kikwete alisoma uchumi wa wapi au ndo degree za kupewa kwa kuwa unaisifu TANU na CCM
 
At least umesema hotuba ya Kikwete, ungeweka Rais wala nisingefungua kusoma, in General nothing new & expect nothing, nothing from JK, nadhani hata ulimwona dhamira yake inavyomsuta, hana confidence, as usual kashamchagua Meghji kashfa kibao, full usanii period

Mr president....niko makini sana na semi zangu....maana ukweli haufichiki kwamba hakuwa na uwezo wa kushinda kihalali...so hata mi SIMTAMBUI KAMA RAISI WA TZ . Ukisikiliza hotuba ya huyu mtu kwa kweli unagundua kwamba huyu jamaa ana ufinyu mkubwa wa kupambanua mambo .....Mara nyingi hotuba zake ni za tumefanya hivi bila evidence. Na ni wepesi sana wa kuchukua mipango ya wahisani kuweka kama sera zao au effort zao za kusaidia nchi.. Wanachukua road maps za benki ya dunia na wahisani wengine na kusema wao ndo wanatekeleza.....hivi anadhani watanzania bado ni wajinga kiasi cha kushindwa kupambanua mambo ? I am very ashamed of this guy....
 
Wadau...tuipime hotuba hii ya mweshimiwa kwa uchakachuaji bungeni.. Mi nimesikiliza suala la michezo limenipa kichefuchefu..
'Tumeleta makocha wazungu kufundisha michezo...' hivi hii ni akili au mgango :A S cry:

Imekaa kama zile hotuba zake za mikutano ya kampeni - ame-copy na ku-paste kutoka kwenye hotuba zake zilizopita!!
 
ni hotuba nzuri na iliyokidhi vigezo vyote ambavyo vinatoa mwelekeo wa serikali yake kwa 201-2015, hakuna alicho acha kwenye hotuba yake hii. Amezungumzia utawala bora, muungano, michezo, maslahi ya watumishi serikalini, ushirikiano wa kimataifa,wajibu wa bunge, muundo wa baraza lake la mawaziri na watu wenye sifa gani, ukusanyaji wa mapato ya serikali nk.

katika hotuba yake kikwete ametuthibitishia kuwa hajui nini chanzo cha umaskini wa tanzania kama alivyopata kuwajibu waandishi wa habari wa nchi moja ya ulaya. Tatizo lililopo hapa nchini ni ukosefu wa usimamizi wa watendaji wa serikali kuu na zile za mitaa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa ni ya kuhakikisha kiasi kidogo cha raslimali fedha kinchotengwa kwa sekta mbali mbali kinatoa matokeo yanayolingana na thamani hiyo.

hilo hakuligusia katika hotuba yake ya jana na badala yake aliendelea kutaja ongezeko la mgao wa fedha kwa sekta mbali mbali, ambapo ni furaha wa watumishi katika sekta hizo ambao sasa watakuwa na raslimali fedha nyingi zaidi za kufanyia ufujaji kama ilivyokuwa katika kipindi cha 2005-2010.

kwa maoni yangu naona alikuwa anatimiza wajibu kuwa alihutubia na kufungua bunge kwa sehemu kubwa ya hotuba hiyo kujaa kuusifia utendaji wa kipindi kilichopita kana kwamba yuko katika kampeni badala ya kutuonyesha kuwa anafahamu changamoto zilizopo katika serikali yake na hatua za kuzikabili.
 
1. To build a solution that works, it is valuable to know what does not work.

2.
Aid programs that give things away offer temporary alleviation at best. At worst they create dependency and damage the local economy. Giving things away is unfair. Who decides who gets the gift and who does not? It is also unsustainable. What happens when the donor leaves? Giveaways make sense in response to a humanitarian crisis, but they are not a long-term or sustainable solution to poverty.

These two mesages are for Kikwete who does not know where to start to solve Tanzanians problems, hoping that aids will solve our problems but at the same time he is not aware the route causes of the problems he his willing to solve!
Pato la taifa ni sh 400billion kwa mwezi, based on these data pata la taifa kwa mwaka ni takribani 4.8 trinion, bajeti ya Tanzania mwaka 2010-2011 ni trioni 11. Rais makini angegusua ni jinsi gani ya kukabiliana na deficit budget ya namna hii. Jamani kama kuna mtu alipata kusikia akiongelea suara la deficit budget katika speech yake anijuze!
The man is not serious at all! Wait you will see! Maji kila sehemu! I am 12km from the state house but no pipe water! Will that be possible! We still have a long way to go and to reach where we want to go will only be possible if we decide by action just as they did CHADEMA MPs to find our owns ways out of CCM, otherwise tutaendelea na usanii uleule. Byv the way yesterday it was not a campaign day, but I wonder why ccm are still campaigning?
 
Nashukuru mungu amemaliza bila kuanguka ingawa vikohozi vya apa na pale vilikuwa haviishi.
Naona dk wake alimshauri awe anagonga maji frequently

Hapana mkuu, ukweli ni kwamba yale maji wamemix na GIN, aina ya GORDON, ili awe anapoteza hisia za kuanguka, hawa madokta wetu ni noma, ni kama walivyomshauri Aman Karume, awe anagonga kwanza John Walker, Black label, si unamuonaga kila anavyohutubia jinsi anavyoyoyoma, huwa nacheka sana nikianza kumwangalia, na wewe uwe unamchek kwa makini utagundua kitu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom