Tuione sura ya nne ya rasimu(haki za binadamu) uhuru wa kwenda utakako!

jossamt4

New Member
Jun 18, 2013
1
0
1. Naomba Tume ya warioba iongezee maneno hapo kwenye Uhuru wa Kwenda Utakako bila bughudha, yaani iongelee kwa undani uhuru wa abiria. Hapa nchini ni tabia iliyojengekeka kwa abiria kutokuwa na mtetezi aliye kisheria. Japokuwa tunasikia kuwa kule DAR siku hizi kuna CHAKUWA, sisi huku mikoani ni kutaabishwa kila siku na wapiga debe ambao ndo wamegeuza kukaa stendi za mabasi kuwa shamba lao. Iweje Huduma za Mabasi ziendeshwe na Madalali! Iwepo marukufu ya kisheria! 2. Jamani hii, habari ya Muungano kama wananchi tunaendelea kupenda kuendelea nao kwa nini tusiwe nchi moja? Kama haiwezekani kwa nini tuendelee kubembeleza Wazanzibari ambao wamekuwa kidomo domo siku nyingi? Serikali zenu tatu mnazotaka za nini? Si kila upande ukae kivyake? 3. Pia hayo Uwepo wa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mbona rasmu haikutaja. Kwanza hawahitajiki, wamekaa kiuchonganishi, ni bora kila eneo la Kanda liwe Jimbo na liwe na Mkuu wake.
 
Wakuu wa wilaya ndio wasiwepo, ni mzigo. Na hata wakuu wa wilaya wasiwe wale waliotumikia Serikali wakastaafu. Wapatikane pia kwa kuteuliwa na kuidhinishwa na mamlaka nyingine kama vile Bunge.
 
Kuwepo kwa wapiga debe ni dalili ya udhaifu ktk usimamizi wa sheria kwa CCM!

Hata katiba ya sasa hauwatambui wapiga debe!

Hawa huenda wanatambuliwa na serikali ya CCM tu na ndo inawalinda!
 
Kuhusu suala la Muungano hatuhitaji serikali moja ila kweli kama haiwezekani bora tugawane mbao ili iondoke dhulma kwa Wazanzibari. Tumechoka kudhulumiwa kila uchao na Wabara kwa kisingizio cha Muungano.
 
Back
Top Bottom