Tuijenge CHADEMA kwa ukombozi wa mtanzania

STEIN

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
1,770
552
Ndugu zangu wana JF, na wapenda maendeleo kwa ujumla.

Napenda kutanguliza shukrani zangu kwenu kwa ushiriki weni huku kwenye mijadala ya humu JF na naomba tuendelee na mjadala huu.

Naomba tujadili namna nzuri ya kuijenga chadema kwani imeonekana ni Tumaini jipya kwa wanyonge, wapenda haki na wenye uchungu na rasilimali za nchi hii.

Kwanza kabisa nawashukuru viongozi wote wa chadema kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wabunge wa chadema kutoka 11, 2005 hadi 48 ya mwaka huu hii inatia faraja pamoja na kwamba maeneo mengi chadema haikutendewa haki, maana hata kwenye chama tawala chenyewe hakuna haki sembuse wananchi na chadema kutendewa haki? ni jambo la kusikitisha.

Jambo la pili ni kuwapongeza wananchi kwa kuielewa chadema inataka kuwafanyia nini na kujitolea kulinda kura za chadema kwa nguvu zao wenyewe kwani kukaa kwenye kituo cha kupiga kura siku tatu mfululizo bila fujo ile hali wanajua matokea na wanasubiri yatangazwe bila kuchakachuliwa. Kwa hili nawapongeza tena viongozi wa chadema kwa uvumilivu maana wangekuwa hawana uchungu na nchi hii wangewashawishi wananchi wakafanya vurugu baada ya matikeo kuchakachuliwa kama Kibaha mjini, Segerea etc. tuliona jinsi wagombea walivyo watuliza wananchi. Kwa hilo nawapongeza.

Pia nawapongewa wana CCM kwa kuwaangusha watu kana kina Karamagi, Mramba, Marmo, Batilda, Mpesia etc. maana chadema wenyewe wasingeweza kuwatoa kwenye nafasi zao, ni baada ya kuunganisha nguvu zao pamoja ndio hayo yakawezekana. Ni matumaini tutazidi kuwaunga mkono wana CCM pale watakapotaka kumtoa kiongozi wanayemdhani hafai, na mafisadi wanataka kumweka kwa nguvu kama walivyofanya kwa Shibuda na Iringa mjini.

Mwisho naiomba chadema ihakikishe inaweka uongozi imara kwa kila mkoa, Wilaya na hadi Kijiji, ikiwezekana watumie muda mwingi kuwaelekeza wananchi ni jinsi gani Elimu bure, Afya bure, Makazi bora yanavyowezekana ili kila kiongozi wa CCM ashinikizwe katika kila ngazi kutekeleza hayo. Maana 2015 si mbali kutoka sasa ili Chadema isiwe na kazi tena ya kuelimisha watu bali kazi ya kulinda kura na mbinu zingine za kulinda ushindi.

Binafsi nashauri Operesheni "Elimu Bure,Afya Bure na Makazi Bora yanawezekana " ianze mara moja baada ya kuwashukuru wananchi kwa kuwachagua.

PEOPLES pOWER

 
tehehehe tehetehehetehe tetehetehehehe ikomboeni kilimanjaro yenu kwanza kabla hamfafikiria kuikomboa bumbwini yetu
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom